Mbunifu wa mitindo maarufu kutoka nchini Tanzania,Mustafa Hassanali, ni miongoni wabunifu wa mitindo 77 kutoka mabara 6 ya ulimwengu wanaotarajiwa kushiriki katika maonyesho ya mavazi yajulikanayo kama ARISE Magazine Fashion Week(AMFW) yanayotarajiwa kufanyikia jijini Lagos nchini Nigeria mwezi ujao.
Maonyesho ya mwaka huu yatafanyikia katika viwanja vya hoteli maarufu na ya kifahari ya Federal Palace Hotel ya jijini Lagos yataanza Siku ya Jumanne tarehe 6 Machi na kumalizika Jumapili ya tarehe 11 Machi (Tuesday 6th March-Sunday 11th March). Haya yanafuatia yale ya mwaka jana ambayo yalishuhudiwa na zaidi ya wageni 5,000 wakitazama ubunifu kutoka kwa wabunifu 51 uliowekwa jukwaani na wanamitindo 81.
Mustafa Hassanali ni mbunifu wa mitindo pekee kutoka nchini Tanzania anayetarajiwa kushiriki katika maonyesho hayo ambayo yanazidi kujipatia umaarufu.Orodha kamili ya wabunifu wa mitindo wanaotarajiwa kushiriki katika maonyesho hayo ni;
Adama-Paris (Senegal/France), Amine Bendriouich Couture and BS (Germany/Morocco), Amrapali (India), Angelo Van Mol (Belgium/Ghana), Be-Grey (Nigeria), Bestow Elan (UK/Ghana), Bridget Awosika (Nigeria), Buki Akib (UK/Nigeria), CHICHIA (UK/Tanzania), Christie Brown (Ghana), CLAN (Nigeria), David David London (UK), Davida (Nigeria), Duaba Serwa (Ghana), Ejiro Amos Tafiri (Nigeria), Eki Orleans (UK/Nigeria), Frank Osodi (Nigeria), Funlayo Déri (UK/Nigeria), Gavin Rajah (South Africa), Gloria Wavamuno (Uganda), HOUSE of DIVAS (Nigeria), House of Farrah (Nigeria), House of Nwocha (Nigeria), ICONIC INVANITY (Nigeria), Imane Ayissi (France/Cameroon), Jacob Kimmie (UK/South Africa), Jewel by Lisa (Nigeria), Kastle Designs & Treasure Chest (USA/Ghana), Kaveke (Kenya/UK), Kevan Hall (USA), Kezia Frederick (UK/St.Lucia), Kiki Clothing (Ghana), Kinabuti (Italy), Klûk-CGDT (South Africa), Koke (Botswana/India), Korto Momolu (USA/Liberia), Lanre Da Silva Ajayi (Nigeria), LaQuan Smith (USA), Laurenceairline (France/Ivory Coast), Loza Maléomsho (USA/Ivory Coast), Madam Wokie’s Couture (Sierra Leone), Mai Atafo (Nigeria), Maki-Oh (Nigeria), Mataano (USA/Somalia), Meena (Nigeria), Mustafa Hassanali (Tanzania), NKWO (UK/Nigeria), Odio Mimonet (Nigeria), Okunoren Twins (Nigeria), Osman (UK), Paul Hervé ELISABETH (Martinique), Poisa (Kenya), Re Bahia (UK/Nigeria), Sandra Kennedy (Jamaica), Sandra Muendane (Mozambique/Portugal), Sunny Rose (Nigeria/UK), Taibo Bacar (Mozambique), the Vessel. By Lois (USA/Jamaica), Tiffany Amber (Nigeria), Timo Welland (USA/South Africa), Tsemaye Binitie (UK/Nigeria), U.Mi-1 (UK/Nigeria), Virgos Lounge (UK/Nigeria), Viv La Resistance (Nigeria), William Okpo (USA/Nigeria) and Zekaryas Solomon (Eritrea/UK).
BC inapenda kumpongeza Mustafa Hassanali kwa mafanikio haya na juhudi zake katika kuitangaza Tanzania kupitia mitindo na ubunifu.Kila la Kheri.
Zilipotufikia taarifa juu ya mapatano na makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Mbeya Mjini,Mh.Joseph Mbilinyi(Sugu) na Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba,tuliketi chini na kuzitafakari.Tulipochekecha na kuweka bayana mambo kadhaa,tuliwatafuta baadhi ya wasanii ili kutaka kupata maoni yao juu ya makubaliano na mapatano hayo.Hivi ndivyo walivyotuambia;
PROFESSOR JAY: Ni jambo jema sana kwa sanaa yetu kuwa na lengo moja na umoja ndio tegemeo letu la mwisho kabisa katika kutatua matatizo yetu.Kama kweli wameamua kwa dhati kutoka mioyoni mwao na bila kushinikizwa na mtu au hali yeyote basi ni hatua kubwa sana mbele katika hizi harakati zetu za kumkomboa mwanamuziki na sanaa ya Tanzania dhidi ya umasikini uliokubuhu na katika utetezi wa HAKI na MASLAHI yake! Wito wangu wawaambie na wafuasi wao nao wayamalize ili tufungue ukurasa mpya kikamilifu.
MwanaFA: No Comments
CHIDI BENZ: Nafikiri ni kitu kizuri kama baada ya hapo,may be, ukiwa ndio mwanzo wa mazuri.Nasisitiza kuna wanaoumia na kuna ambao walishaumia.Huu si muda wa wao kushindana na kusababisha wengine washindane.Ni afadhali kila mmoja abaki na la kwake endapo kuna unafiki katika Muungano.Kama ni kujenga,tujenge kwa sababu hatuwezi ishi milele lakini tunaweza kuendeleza vizazi kwa kutumia nguvu na wakati ambao tunao. La Familia.
FID Q: No Comments
Picha maarufu kwa wiki hii(na wiki zijazo) na bila shaka inayopendeza kwa wengi na vile vile kutopendeza kwa wengine ni hiyo hapo juu inayowaonyesha Mbunge wa Mbeya Mjini, Mh.Joseph Mbilinyi aka Sugu akipeana mkono na Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba huku kitendo hicho kikishuhudiwa na Waziri wa Vijana,Habari,Michezo na Utamaduni,Mheshimiwa Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu jijini Dar-es-salaam hivi leo. Mkono huo au mikono hiyo ni ishara kutoka kwa wawili hao kwamba wameamua kuweka tofauti zao zilizodumu kwa takribani miaka miwili pembeni na kufungua ukurasa mpya.
Nimeanza kwa kusema picha inayondeza kwa wengi na vile vile kutopendeza kwa wengine kwa sababu ninapoandika hapa tayari gumzo kubwa lishaanza hususani katika mitandao jamii (Facebook na Twitter ikiongoza)ambapo kuna uhuru wa aina yake wa kujielezea.Kuna ambao wanahisi kusalitiwa huku wengine wakihisi kuwa na nguvu mpya na ari mpya kama ile aliyoingiaga nayo Kiongozi Mkuu wa nchi hii.
Sisi hapa BC, tumeipenda picha hiyo. Tunaamini kwamba mwisho wa siku,sisi wengine tunaombea zaidi amani na upendo.Hilo ni la msingi sana wakati huu na hata wakati ujao.Kuna umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana.Hata kama hampatani,basi kuwa na nia ya kutafuta jinsi ya kufanya kazi na kufanikisha jambo fulani.
Here is the new track from an upcoming artist Blacka who resides in Morogoro.He features Domokaya,from one popular duo of Mandojo na Domokaya.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
CREDITS
Song ; Shamba La Bibi
Artist ; Blaka feat Domokaya
Created and Composed Blaka
Instrumentation By Pfunk @Bongo Records Studios 2011
Leo hii ukiulizia models kutoka Tanzania wanaofanya vizuri katika ulimwengu wa kimataifa katika suala zima la uanamitindo,bila shaka majina mawili ndio yatakuwa ya kwanza.Flaviana Matata na Herieth Paul. Nchini Tanzania,Flaviana anajulikana sana.Kila mara huwa anatembelea Tanzania na ana mambo kibao anafanya ikiwemo vitu kama Flaviana Matata Foundation. Herieth hajulikani sana nchini Tanzania.Anaishi Ottawa nchini Canada.Hizi hapa ni baadhi tu ya picha zao wakiwa kazini.Hii ilikuwa katika London Fashion Week iliyomalizia mwishoni mwa wiki hii.
Video ya wimbo Mawazo kutoka kwa msanii Diamond imetoka.Neno lililopo ni kwamba ilikuwa inasubiriwa kwa hamu sana.Kisa?Wakati wa kutengenezwa kwa video hii,kiliibuka kitu ambacho baadae kilisababisha gumzo lingine.Ilisemekana kwamba Diamond na Jokate(miongoni mwa warembo wanaopamba video hii) walionekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida. Wenye kujua mambo wakanadi kwamba wawili hao,bila shaka walikuwa wameanzisha kajisafari ka mapenzi.Moja jumlisha mbili ikawa kumi.
Maneno yalipomfikia Wema Sepetu(girlfriend wa Diamond kwa wakati huo) kumi ikawa kumi na mbili na mwisho wa mapenzi yao ukawa umeanza kujongea.Kipindi hicho hicho Diamond akaachia wimbo mwingine akiuliza ampende nani(song title:Nimpende Nani).Udaku ukashika moto.Mengi yakaongelewa nk.
Sasa ni wakati wa kuitazama video yenyewe.Hii hapa chini.Binafsi nimeipenda hususani muonekano na quality yake.Pamoja na hayo Diamond hajaonyesha kama ana mawazo kikweli.Ukiwa na mawazo na ukiwa unatamani kunywa pombe,bila shaka wajua inavyokuwa! Maudhui yamepotea kidogo.Lakini kwa ujumla,it’s a good video.
Mbunifu wa Mitindo,Manju Msita,akiwa kazini kwake.
Ni siku ya Jumamosi,nipo jijini Dar-es-salaam tayari kabisa kwenda kuonana na miongoni mwa wabunifu wa mitindo (Fashion Designer) mahiri kabisa hapa nchini, Manju Msita. Tofauti na siku zingine za Jumamosi,leo hakuna msongamano mkali wa magari barabarani.Hii si kawaida sana kwani siku hizi jiji la Dar-es-salaam lina sifa mbaya ya kuwa na foleni zisizokwisha.
Kwa muda nimekuwa nikiwasiliana na Manju.Hatujawahi kuonana.Sina hata hakika kama yeye ameshawahi kuona picha yangu.Mimi nishawahi kuona yake kutokana na ukweli kwamba Manju ni mbunifu maarufu,sio tu nchini Tanzania bali katika ukanda mkubwa wa Afrika.
Ofisi au karakana(workshop) ya Manju ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Smart Africa,kampuni ya masuala ya mitindo na ubunifu anayoiongoza Manju,zipo maeneo ya Chang’ombe.Zamani palikuwa na kituo kikubwa cha sanaa cha Mikono Arts.
Nawasili maeneo yale na kupokelewa vizuri na kila mtu.Manju ana timu nzuri.Wapo vijana, wa kike na kiume,wenye uchangamfu wa ajabu.Namkuta Manju ameketi huku kajiinamia.Mkononi kashikilia pencil.Mara moja nachungulia anachokifanya na kuona wazi alikuwa akichora.Anaacha anachokifanya na kusimama kunikaribisha.Manju anapenda utani.Mara moja tunaanza mazungumzo ya kawaida huku nikiwa na shauku ya kuanza kufanya kilichonipelekea(mahojiano). Anakuja dada mmoja na kwa sauti ya unyenyekevu ananiuliza kinywaji ninachotumia.Naagiza maji ili panapo kuanza kwa mazungumzo,koo lisije kunikauka.Maji yanawekwa mezani,naanza kuweka koo langu sawa.
Kabla ya kuendelea mbele,Manju anaomba anipe kwanza tour ya ofisi yake na kunitambulisha kwa watu wake.Kila kona ya ofisi yake imepambwa kwa nakshi za kiafrika au zenye utambulisho wa kiafrika.Natizama michoro ya magauni,nageukia kule na kuona magauni,mashati nk.Haya naambiwa mengine yanauzwa na mengine yanasubiri wenyewe kuja kuchukuliwa.
Tunarejea ofisini kwake.Hapo nagundua kwamba kuna mziki laini unaimba.Muziki wa kiafrika.Nasikia sauti ya Habib Koite.Kisha namsikia Oliver Mtukudzi.Tunaendelea kusikia muziki kwa mbali na mazungumzo yetu yanaanza kama ifuatavyo;
BC: Unakumbuka ulianza lini safari yako ya kuwa mbunifu wa mitindo?Nini au nani alikuvutia kuingia katika fani hii?Ni mambo gani ya msingi ambayo ilikubidi ujifunze mara moja pindi ulipofanya uamuzi wa kuwa mbunifu wa mitindo?
Ni kinadada wa African Stars.Picha kwa hisani ya John Bukuku.Unapoiangalia na kuweka sawa mipangilio ya kimavazi,je wamepatia?
Vijana wa muziki wa kisasa,(nipo sahihi kuwaita hivyo?),mnajua zaidi kuhusu muziki wa leo.Ninachokijua mimi ni kwamba vijana mnajitahidi,wanajitahidi.Kuna mapinduzi ya taratibu.Bado utumwa upo lakini ipo siku utaisha.Sieleweki,sitaki unielewe.Kwanini?
Ninachotaka kukwambia ni kwamba kuna ingizo jipya.Hapa ni Linex(huyu bwana alikuwa na Birthday Bash majuzi tu) akiwa amemshirikisha Diamond Platnumz ambaye ni mkali mwingine wa uimbaji.Wimbo unaitwa Nitaificha Wapi.Usikilize hapo chini
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Jumamosi hii,katika Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam,Timu ya Soka ya Yanga inatarajia kujitupa uwanjani kupambana na timu kali ya Zamaleki kutoka nchini Misri katika mchezo wa raundi ya kwanza kuwania Kombe la Klabu Bingwa Afrika.Mchezo huo utakuwa unapigwa katika kilele cha timu hiyo yenye makazi yake Jangwani ikiwa inasheherekea miaka 77 tangu kuanzishwa kwake.
Sasa kama unavyojua,hapa nchini ukiongelea soka lazima uwataje Simba na Yanga.Habari zilizopo mtaani zinapasha kwamba mashabiki wa timu ya Simba yenye makao yake makuu pale Mtaa wa Msimbazi Kariakoo,wameshanunua jezi kibao za timu ya Zamalek kwa nia ya kuishangilia kwa nguvu timu hiyo kutoka Misri itakapokuwa inamenyana na watani wao wa jadi hiyo siku ya Jumamosi.
Mashabiki mbalimbali wa Simba wamesema wao wataishangilia Zamalek.Hawatojali suala la utaifa.Hilo haliwahusu na zaidi wanasema kwamba hii ni kulipiza kisasi kwani Yanga waliwahi kuvaa jezi za TP Mazembe(Ya DRC) ilipokuja kumenyana na Simba.
Kama kuna ukweli katika hili,basi ujue kazi ya kuwashawishi wananchi wawe wazalendo kwa timu zao za nyumbani na hata timu ya taifa(huwa ikiwa na wachezaji wengi wa Simba basi Yanga wanasusa na vice versa) lina safari ndefu.Je,wewe msomaji,ushanunua jezi yako?Tuambie


sending...
















