Hasheem Thabeet, kijana anayetarajiwa kujiunga na ligi maarufu ya NBA hapo mwakani amerejea nyumbani Tanzania kwa mapumziko ya majira ya joto (summer). Hasheem ambaye anasomea masomo ya Saikolojia katika chuo kikuu cha Connecticut pia anachezea timu ya kikapu ya chuo hicho maarufu kama UConn Huskies.Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 16 Februari mwaka 1987. Nini matarijio yake, anasemaje kuhusu maisha ya Marekani na anajisikiaje kuondoka nchini kama mtu wa kawaida tu na kurejea na umaarufu alionao? Tarajia mahojiano yetu na Thabeet Hasheem hivi karibuni.

Pichani juu ni Hasheem Thabeet akiwa na mama yake mzazi (Rukia Manka) mara baada ya kuongea na waandishi wa habari jijini Dar hivi karibuni.Picha kwa hisani ya Michuzi.

Feedback / Comments

11 Responses to “Hasheem Thabeet ndani ya Dar!”

  1. Comment by Big L on June 17th, 2007 9:45 pm

    Jamani, hii sio mchezo .. Huyu ndio atakuwa mbongo wa kwanza ndani ya NBA.I just wish him all the best (Hasheem)

  2. Comment by diana on June 28th, 2007 8:28 am

    on behalf of tanzanian we are so happy and proud of you. good luck and may God be with you .

  3. Comment by mboni on August 4th, 2007 5:08 am

    We are all so proud of you, well done and may god be with you all the way.

  4. Comment by Mkereketwa on December 17th, 2007 4:26 pm

    He jamani, huyu hashimu nilisomaga naye Mlimwa primary Dodoma. ama kweli umdhaniae sie, ndiye. Alivyokuwaga mchafumchafu miguu imejaa vumbi, kamasi linamtiririka kutwa nzima. Hivi sasa yukolevel ya kina Shaq O’nel,duh jamani jamani jamani.Kweli bahati zina wenyewe jamani

  5. Comment by amina on February 29th, 2008 5:43 am

    we mkereketwa usijifanye unamjua sana

  6. Comment by baddy on May 13th, 2008 11:20 pm

    Hashimu ameamua kurudi chuoni, kwa hiyo tutasubiri hadi mwaka ujao kabla ajiunge na ligi ya nba. Hongera Hashimu, na nawahimiza wachangia kadha waache kumwonea wivu na kujidai kwamba wanamjua ilhali hawana mbele wala nyuma.

  7. Comment by Usijifanye Mjuaji on July 8th, 2008 6:27 am

    “He jamani, huyu hashimu nilisomaga naye Mlimwa primary Dodoma. ama kweli umdhaniae sie, ndiye. Alivyokuwaga mchafumchafu miguu imejaa vumbi, kamasi linamtiririka kutwa nzima.”

    Wewe sikiliza mbona wabongo tunapenda sana kujufanya kila mtu tunamjua??
    Sasa huu ni ujinga na sijui ni kwa nini mmeruhusu maoni ya mpuuzi huyu yawepo muda wote huo

    Wewe ni mjinga sana actually………we utabakia kusemaga maneno ya kipuuzi tuuu

  8. Comment by Matty on November 15th, 2008 6:43 am

    nyie nanyie lol!kwani kitu gani kumjua??watu wanawajua hao mawaziri sembuse this young dude!

  9. Comment by benjamin on December 5th, 2008 8:03 am

    hallo mi ni benjamin nayo furaha kubwa pia kumwona mtanzania mwenzangu akiwa anapeperusha bendera ya nchi yetu Tanzania nchi ya watu.nachotaka kusema tu sisi watanzania Mungu ameweka kitu cha tofauts sana ndani yetu tusiwe watu wa kujidharahu hata kidogo.tubadiri kusema kwetu alafu tujione sisi ni wa thamani sana.hashimu mimi nimekuwa naye tangu udogo wetu tumecheza pamoja na kusoma ktk shule moja ila nilimtangulia darasa moja.nimefurahi sana .Mungu adhidi kumwinua zaid.

  10. Comment by yn on March 24th, 2009 12:27 am

    thats cool big boy!!,just be serious n look foward to make it right!!,safari kuelekea mafanikio bado ipo so you need to be serious!!,hope u will make it!! wish ya a nice journey in basketball!!

  11. Comment by big tymer on August 26th, 2009 10:37 am

    big up bro” may god bless ur way,jus leave the haters shoutin.u rock. b cool n polite wabongo hawachelewi kuharibu dream ya mtu then wakakuita umefulia, jiepushe na ugomvi wa aina yoyote bro,

Leave a Reply