Kama wewe ni mtanzania, unaishi au umeshawahi kutembelea Ulaya ya Kaskazini(Northern Europe) sio ajabu ushawahi kusikia jina la kundi la muziki linaloitwa Mighty 44. Jambo ambalo inawezekana hulijui ni kwamba kiongozi wa kundi hilo ni Rummy Nanji, kijana wa kitanzania ambaye amekuwa akiwakilisha huko Ulaya Kaskazini kwa miaka chungu mbovu sasa na kujizolea sio tu umaarufu (celebrity status) bali kuthibitisha kwamba watanzania wana vipaji vya kila aina na nafasi ikijitokeza wanafanya vitu visivyo vya kawaida. Tizama mojawapo ya kazi zake hapa chini.Muziki anaouipiga hapa ndio haswa unaozimiwa huko Ulaya. BongoCelebrity hivi karibuni inatarajia kufanya mahojiano rasmi na Rummy Nanji.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

Feedback / Comments

24 Responses to “RUMMY NANJI”

  1. Comment by Miss. on July 11th, 2007 3:38 pm

    Watanzania kazi nzuri. Atleast our name should be out there. We need more people like this, but one thing I would love to say is, Please Tanzanians who are out there far away from home, be proud of who you are, Let people know that you are Tanzanian. be proud of your language, Don’t let Kenyans take over the Swahili language, we are the only nation who speaks swahili as a national language, tukionana tu hatuulizani kabila wala nini, why can’t we advertise Tanzania? kazi nzuri Bongocelebrity.

  2. Comment by magdagibbz on July 12th, 2007 1:07 am

    hivi ni kweli huyo bwana anauraia wa tanzania ? na kama ni kweli miaka yote hiyo alikuwa wapi kujitamabulisha kama mtamzania ?
    jamani msipende kubababikia watu kwa sababu ya mafanikio walio nayo sasa mnalazimisha eti huyo ni mtanzania huo utanzania wake hauna maana kwetu sisi wabongo kama miaka yoote hiyo ameona ni aibu na haaifai kujiuza kama mtanzania
    acheni kubabaikia watu na huo mziki siyo identity ya tanzania hata kidogo tengenezeni identity yenu original ya kitanzania kisha muitoe kimatatifa na siyo kimatatifa uchochoroni kwenye vifangsheni vya wabongo hiyo itakuwa ni kutwanga maji kama vile sas tunavyosikia baadhi ya wanmuziki wa bongo flava wakienda huko ulaya wakirudi ni kujisifia tuu na hali ukimwuliza mauzo yako ya records vipi jibu lake ni kichekesho kwenye masoko ya muziki yanyoeleweka wanamuziki wa tanzania hawapo tuache misifa na kudakia dakia watu eti mtz ooh mtz ooh mara sisi bab kubwa
    my brothers tusijisifie wacheni ulimwengu utusifie hapao tutasema wabongo ki muziki ni bab kubwa

  3. Comment by Joel Mabura on July 12th, 2007 8:53 am

    SIONI ANACHOKIFANYA HAPA!MBONA MIAKA YOTE HIYO HAJASIKIKA!NA ULAYA GANI YUPO?MBONA HII VIDEO YENYEWE
    AHIONYESHI MAADHI YA MZIKI WA KITANZANIA!!!!! HUYU ANADANGANYA WATU!KAAMUA KUFYATUA VIDEO NA KUTUDANGANYA!
    WADANGANYIKA! HATUDANGANYIKI TENA

  4. Comment by Ryhmson Kazia on July 12th, 2007 9:35 am

    Hii ni kwa watoa maoni namba mbili na namba tatu hapo juu.Kwanza kabisa acheni jealous.Habari za uraia wake wewe zinakuhusu nini?Muziki ni muziki tu,huo muziki wenye mahadhi ya kitanzania ni upi.taarabu au lizombe?Mimi nipo hapa Finland na nitakwambia kitu kimoja,Nanji ni mwanamuziki mwenye jina kubwa na anayejivunia utanzania wake.Kama wewe humjui au hujawahi kumsikia google jina lake utaona jinsi mchizi anavyotesa na anavyouweka mbele uraia wake.Kwa sababu gazeti la Kiu au Ijumaa halijaandika habari zake labda ndio maana unadhani anautangaza uraia wake kwa kujificha.Heko bongo celebrity kwa kututambulishia watu kama hao wanaopeperusha bendera yetu nje.Na wanamuziki wa bongo flava endeleeni hivyo hivyo.Ipo siku bongo flava itapigwa katika kila jukwaa la kimataifa.Huwezi kimbia kabla ya kutambaa.Ebo!

  5. Comment by Laila on July 12th, 2007 10:32 am

    Ryhmson umesema kweli. Watanzania wengi walio nchi za nje wooote wanaomba uraia wa nchi walizokuwepo ili waweze kudumisha maisha yao. Na ndio maana kuna kurupushani za kuomba Tanzania iwe inaruhusu kuwa na raia mbili. Mbona hata hiyo bongo flavour nayo ina coppy wanamuziki wa nje, hivi ktk interviews zote za hapa bongo celebrity wanamuziki wote ukiwaauliza nani unapenda kufanya nae kazi wanasema oooh Jay Z, Beyonce, P didy, n.k, rudi msome interview za waimbaji wetu, hamna hata mmoja aliesema angependa kuimba na Khadija Kopa, au Twanga pepeta. leo tunakaa hapa ku criticize Rummy, atleast yeye ameamua to be one of them so he can sell within the Earope, na kujivunia kuwa yeye ni mtanzania. Sasa wewe magdagibbz, jaribu kuwaambia wanamuziki wetu wa bongo wawe proud of who they are not to want to become who they are not.

  6. Comment by gabriel on July 12th, 2007 10:39 am

    Rhymson,angalia mtanzania mwenzangu mimi sina wivu na huyo bwana suala la wivu linaingai vipi hapa mtu anapotoa maoni hna maana kwamba anawivu suala la uraia wake niliuliza ili nipata ekufahamu kama yeye ni mtanzania mwenzangu kweli kwani mtu mweusi anapokuwa nje ya nchi utamjuaje apotoka kama hatokueleza uraia wake? kuna watu weusi wengi tuu hapa nyumbani TZ lakini hawana uraia wetu na hivyo si watanzania pia ni kweli kama ulivyosema mimi ni wale ngumbaru wanosoma magazeti ya kiu na ijumaa sijawahi kusikia habari zake hata siku moja
    pia hata gazeti letu la kijiji hapa njombe halijawahi kuandika habari zake na bahati mabya sina tv huku nilipo umeme hakuna sasa sijawahi msikia huyo bwana
    kuhusu bongo flava ninachofahamu mimi ni kwamba huo sio mziki kabisa na kama ni mziki kwa maoni yangu si muziki wa tanzania kusema kiswahili pekee haitoshi kuita muziki eti ni wa tanzania nafahamu pia si ngoma za asili labada ningeuita urban youth music lakaini hata ktka definition hiyo pia hauana elements zozote za tanzania
    bongo flava wanatwanga maji tuombe uzima utyadhihirisha haya siku moja hata hivi sasa hapa nyumbanai kila mtu anaona jinsi ganai inavyoanza kuchukua nose dive

  7. Comment by Kipaso on July 12th, 2007 2:11 pm

    RUMY NANJI?!!!HAJULIKANI!!!NAUNGANA NA MTANZANIA MWEZANGU Magdgadibbz kuwa kinacho hongerewa ni kuwa sio urahia tu hinajulikana kuwa labda ni GABACHOLI fulani aliyezaliwa BONGO TZ!hilo atubishi lakinitunapokuja katika maswala ya mziki wa bongo flava na bongo dansi kuna wanamziki wetu wamejitoa muhanga katika kuhusamba wanamziki wa kizazi kipya kama vile SUGU,PROF JAY,LADY JAY D AKA BINT MACHOZI,TID,JUMA NATURE,MR NICE na wale wa dansi kama vile Msondo ngoma,Sikinde DDC Miliman park, the ngoma africa band,Twanga pepeta n.k Lakini huyu Gabacholi Nanji alikuwa wapi wakati wenzie wanatoka jasho kuhitangaza mziki ya tanzania?au kwa kuwa sasa hivi jina la tanzania zuri kimziki kila mtu anataka kuwa mojawapo wa kula matunda ya celebrity?tusibishane ?hakuna mda wakupoteza sisi walalahoi tunajuwa wanamziki walio nyumbani na pia wanamziki wa tanzania walio nje,habari zao tunazisoma na tunasikia mahojiano na nyimbo zao katika radio za hapa na nje.
    HAFAGILIWI!GOBACHOLI HAPA NI WABONGO NA BONGO CELEBRITY

  8. Comment by Baraba on July 12th, 2007 2:33 pm

    Kipaso,
    Rummy Nanji sio mhindi au gabacholi kama unavyowaita.Ni mbongo,mweusi mwenzetu.Ni mtoto wa Gerezani Kariakoo mtaa wa Lindi.Sema lingine.

  9. Comment by Kipaso on July 12th, 2007 2:50 pm

    BARABA!
    sipo katika kumpaka matome Rummy Nanji !lakini nipo katika ukweli wa mambo(a)Ndio unataka kuniambia mtaa wa Lindi Str.Gerezani,kariakoo hakuna magabacholi?wewe Baraba unahijua vema karikakoo walivyojaa gabacholi?ndio kusema kuwa RUMMY NANJI,ni jina la kisukuma au kizaramo? au kwa kuwa Tanzania tamu sasa mpaka gabacholi wote wanataka kuwa wazawa?tuongee mengine,msiseme mziki ni mziki bongo falava au mziki wa kizazi kipya unajulikana na mziki wa dansi unajulikana lazima uwe mziki wa kitanzania kuhipeperusha bendera ya bongo na kuingia katika celebrity ya nchi yetu ya tanzania lazima uhitngaze mziki ya tanzania hiwe ya asili,dansi,kizazi kipya au rusha rohoo.namalizia kuwa kariakoo kuanzia mtaa wa lindi,somali,kungani au somali kipande wapo gabacholi wa kumwaga.tusibishane tuongelee mziki wa bongo

  10. Comment by SEIFU KAPERA on July 12th, 2007 3:07 pm

    Ndugu watoa maoni,
    Kinachojadiliwa hapa sio uraia wa hasili awe mdosi au mzaramo,lakini kama ni rummy nanji anayeongelewa hapo juu ni wa Lindi street hapa kariakoo,basi kijana huyu anayo asili ya kigabacholi hili msibishane sana!na mara nyingi sana hawakuwa wanachanganyika!bali walikuwa wakijinasi kuwa wao ni wadosi hapa Gerezani.Labda watoa maoni tumukubali Rummy ni mtanzania mwenzetu na tumpe moyo kama tunavyowapa moyo wanamziki wengine wa tanzania waliopo nje.
    swala la uraia na hasili lisiwekwe mbele sana kwani halijengi.

  11. Comment by Maia on July 12th, 2007 3:43 pm

    Duu Kam huyu nae alikuwa anajiita mdosi nyumbani lazima kulikuwa na mahojiano makubwa. Mbona anaonekana kama Mbongo halisi, au kadomea sana kwenye damu ya ubongo??

  12. Comment by deo cashmoney on July 13th, 2007 5:25 am

    Mimi naishi miaka kibao ulaya hadi ksho ni mtanzania.nyinyi mnaosema utanzania huko wapi au mziki wa kitanzania wa huyu jamaa huko wapi?nyinyi mnazani kwa kuchoka hapo juani mlipo,sijuhi mabibo au kimara hiyo ndiyo kujua mziki wetu???na kwanza nani anapiga mziki wa kitanzania tena bongo.??hupi mziki wa kitanzania?Kiamba mbeta..toka morogoro imekufa.mdundiko na malimba..kimya.mnazani taharabu mziki wa kitanzania?wa kiarabu..acheni hizo.watu kuwa na urahia wa uraya ni maisha na atulii kama tanzania haitaki watu kuwa na raia mbili hawataki..lakini sisi ni watanzania hizi ni karatasi tu tusisimame foleni za kuomba viza ubalozini..huyo mjomba ni mwanetu na kwake tutaendelea kiasi fulani..karibu bongo mdosi.

  13. Comment by dj tom in japan on July 13th, 2007 7:56 am

    ok, sasa hivi nimetoka kutoa comments zangu kuhusu miss kinondoni, sasa hebu semeni nyie mnaosema eti kwanini tuwe na mhindi? sasa simnaona wenyewe jinsi wenzetu weupe wanavyotuthamini? je nao wambague huyu bwana?….
    kuweni wastaarabu…acheni hizo!!!!
    mtanzanie miye bwanaaaa

  14. Comment by Simon Kitururu on July 13th, 2007 8:42 am

    Watu weusi hulalamika sana kuhusu ubaguzi.Lakini kunakale kamsemo kuwa ukinyoshea mtu kidole kimoja ,kuna vinne vinaunyonshea wewe.

    Hivi kuna mtu anakumbuka kwanini bendi tuziitazo za kitanzania kama Sikinde , ziliitwa Jazz Band?
    Ukitaka kumkosoa mtu kuwa hana uzalendo kimziki.Nenda kasikilize bendi uipendayo halafu jiulize mzikiwake asili yake yote ni ya Kitanzania?Hivi Wewe kama mtanzania unahisi asili yako halisi ni wapi ndanin ya bara la Afrika?Wangoni tutawafuata mpaka Sauzi Afrika…wewe?

    Hivi gitaa ni chombo cha Tanzania?Kinanda je? Je, muziki wako wowote uupendao unachombo kisicho cha Kitanzania?Je, nikisema kuwa kama mzikiwako hautumii vyombo vya kiasili vya Kitanzania umeathiriwa ki…Utasemaje?

    TUACHENI UBAGUZI USIO NA MAANA!

  15. Comment by gabriel on July 13th, 2007 12:54 pm

    simon kitururu karibu sana bwana .kwanza napenda nianze kwa kumpongeza huyo bwana rammy mimi kile kitendo tuu cha kujaribu (irrespectively) kwamba ni aina gani ya muziki anapiga ni hatua kubwa kwa sababu mimi siwezi hata piga marimba tuu achia mbali gitaa.hongera zake
    lakini tunapaozungumzia mziki wa kitanzania sina maana ni ngoma za utamaduni (traditional dances ) au wengine huziita forlk music nk hivyo ulivyotaja hapo juu vinahusiana (nahisi)na muziki wa kiutamaduni
    mimi nazungumzia mziki wa kisasa wa kitanzania (ORIGINAL) amabao mtu akiusikia anajua bila kuuliza tu kwamaba ah! huo ni mziki wa bongo mathalani, mziki wa bendi za akina vijana jazz wakati wa maneti,msondo ,mlimani, bima lee,washirika, miduara nk yoote hii inatumia vyombo vya kisasa lakini ni wa kwetu na siyo wa kikongo .kiwest afrika,siyo kwaito ,siyo hip hop ni mziki originaly wa kwetu
    vionjo vyake ni vyetu .
    bongo flava kweli kwa mirindimo tuu ni mziki wa kufurahisha siwakatishi tamaa wasanii wake wamefanya kazi lakaini nataka kuelezea maoni yanagu binafsi
    mimi sikubaliani na wanaosema bongo flava ni mziki wa tanzania ni mziki fake siyo original kwa sababu ikisikiliza utasikia baadhi yao wanapiga hip hop kama ya wamarekani japo kuwa hawaifikii ile original ya wamarekani ,wengine wanapiga kwaito ilhali hawaifikii ile kwaito original ya south africa ,wengine wanapiga ragga ana reggae lakini ukisikiliza utaona ni ubabaishaji wanajaribu kuwafikia wenyewe ambao dance hall,ragga na reggae ni mziki wao kiasili. mziki wanapiga staili ya zouk lakini wanakwambia hiyo ndio bongo flava mziki wa tanzania ,wanapiga charanga,calypso wanakuambia huo ni mziki wa tanzania au r&b ya kimarekani wanaimba kiswahili na kusema eti ni mziki wa tanzania , mbaya zaidi hata bendi zetu sasa zinaanza na zingine zilishaanza zamani kupiga mziki wa kikongo mfano twanga pepeta ,mchinga sound,hata msondo sasa wameanza nao (inasikitisha )hizi bendi wanajitahidi kweli kuiga staili ya wakongo ya mziki
    haya kwenye mziki wa dini siku hizi napo ndio kabisa wanajaribu kuiga wa-south frika au mambo ya ndombolo the question is WHRE IS OUR OWN KIND OF MUSIC ?

    hata kama ni urban music mimi nasema bado tunapaswa tufanye kile kilicho chetu originally kwani nchi nyingi tu wana urban popular music lakini ukisikiliza unajua kabisa kwamba huu ni wa nchi fulani mfano wa karibu ni wa kwaito ya afrika ya kusini ule ni urban ,au popular music lakini ina identity yao kamilifu wala ubishi

    similarly
    mziki wa kongo wala hau-ulizi mara mara mbili unajua tu huo ni wa congo au ukisikia techno soukous wala huulizi unajua kabisa huo ni wa congo kinshasa na congo libreville
    kwa maoni yangu nafikiri wenzetu wamefanikiwa sana kimataifa katika maana halisi ya kimataifa kwa sababu distributors wa labels kubwa au wasambazaji ,promotors wa kimataifa au promotors wa festivals za kimataifa wanavutiwa na aina ya mziki wanayopiga kuwa ni original sikiliza muziki ya akina:

    oliver mtukudzi ,bueno vista sociale club,awilo ,mafikizolo,angelique kidjo,hugh masekela ,50 cent,tupac,beyance,anu malik(hindi)ali fateh khan, ismail lo,afrikando,bob marley,third world,lucciano,
    wenge bcbg,extra musica , nickel buck,keny rogers,andrea boccheli,guns and roses nk haya ni baadhi tuu ya majina ya wanamuziki wachache ambao ukisikiza miziki yao utajua huo mziki ni wa nchi gani au asili yake ni wapi au ni aina gani ya mziki utaitambua tuu kwa urahisi

    pia ninaamini kwamba kama hao promotors wa kimataifa wakitaka aina fulani ya mziki wataenda kutafuta na kumpromoti yule anayepiga huo muziki kiasili na siyo mtanzania anayejaribu kuiga huo muziki ndani ya jina la bongo flava. mfano kama wanahitaji kwaito wataenda kimantiki afrika ya kusini na wala si tanzania au kama ni sebene na ndombolo iwe ya yesu au ya kidunia watampromoti yule aliye original na bora ambaye ni wakongo wenyewe lakini si twanga pepeta au k-Lynn
    haya ndio maoani yangu kuhusiana na suala la mziki wa kitanzania lakini nasupport mziki wetu na wasanii wetu wanaofanya juhudi za wazi kuweka mziki wa kitanzania (original)ktk ramani
    sijawahi mimi kusikia ati mtu anaendelea kwa kutegemea kukopi kazi ya snaa ya mtu mwingine kama yupo basi mnieleimishe
    pia tuache misifa ,tusijigambe kwa sababu ya mziki wa kukopi wa kuiga tujigambe kwa kilicho chetu tuwasupport wanmuziki wetu hapa nyumbani hasa wale wanaohangaika usiku na mchana kupiaga na kuendeleza mziki wenye identity ya kitanzania
    tukubaliane kutokukubaliana nakaribisha mawazo tofauti
    akhsante

  16. Comment by mpenda mziki wa bongo on July 14th, 2007 8:43 am

    Napenda kukujibu bwana Simon Kitururu,mtu kama wewe uapojaribu kutoa maoni jaribu kuhangalia sana vinginevyo utajikuta unajiharibia jina na heshima yako.
    Kwanza sisi wengi tulio nyumbani,tusependa kuburuzwa au kulazimishwa kufagilia kitu kama mziki usio katika mtazamo wa kitanzania haswa kwa kipindi hiki cha mageuzi ya utamaduni,pia lazima uje kuwa siku hizi sisi watanzania tunajua kusema HAPANA na tuna maana hiyo HAPANA.
    (3) Swala la bendi ulizozitaja kuwa mziki wao hauna maadili ya kitanzania kama wasanii wa bongo flava nk.
    ndio lakii wasanii hawa wanaujumbe kwa walio wengi hapa nyumbani na tunawakubali kwa mchango wao na ni wenzetu sasa usitulazimishe kumkubali mtu ambae hatuhuoni mchango wake katika utamaduni na mziki wa kitanzania.
    (4)Kuhusu bendi ulizozitaja kuwa zinahishia na majina JAZZ,na bendi kama vile twanga pepeta,sikinde hata hiwe msondo,utake usitake bendi hizi zilizo hapa nyumbani ndizo zinatubuludisha walalahoi,sina maana kuwa tuna zibagua bendi za watanzania mlio nje lakini
    tutasikilza aina gani ya mchango na mziki wao katika kuhitangaza Tanzania,msiwe kukaa kwenu ughaibuni kukawa ndio kigezo cha kutulazimisha tukubali hoja au kila mnachokisema!BONGO CELEBRIY KWA WABONGO WANAOHIFANYIA KITU BONGO SIO KWA KILA MTU ,na kuhusu
    Ubaguzi hapa watanzania halisi hatuhujui ubaguzi hila wenzetu wenye asili ya kihindi na hata walichanganya damu kidogo huwa wanapenda kujimega pande na kuta wao kuwa superiol kwa sisi wananchi tulio wengi
    mfano wakati wasanii wetu wanahimarisha BONGO FLAVA wenzetu hawakupenda mafanikio ya watoto wa walalahoi bada yake waliamua kuanzisha BONGOBANGLA hili mradi kuwepo uhindi fulani.jaribu kutia hakili

  17. Comment by Simon Kitururu on July 14th, 2007 12:48 pm

    Hivi Mziki ni nini?
    Duh!
    @Gabriel+Mpenda Mziki wa Bongo.
    Nimeelewa msemalo.Naheshimu Msemalo.
    Topiki kubwa hii!Ni rahisi kutoeleweka.AU?

    Haburuzwi Mtu lakini.

    Nachojaribu kusema kwa sentensi fupi ni kuwa, Kama uzuri ulipo jichoni mwa mtu. Sikio vilevile liko kichwani kwa mtu, kuelewa pia kuko ubongoni mwa mtu. Kila mtu anachake.

    Katika mfano wangu ambao haukueleweka, labda niseme kuwa Usimkane mtu ubongo kwa sababu tu ya ukurasa mmoja ambao hauwezi kumuelezea mtu kisawasawa, muonekano mmoja, Mziki fulani apigao…nk
    Duh!

  18. Comment by gabriel on July 14th, 2007 4:15 pm

    simon kitururu ,baba nimekubali umeshinda nakubali kushindwa . ama kweli hapa iko kazi .
    big up mlimani,msondo na che mundugwao nk
    down ,down with pikaso wa plastiki

  19. Comment by mpenda mziki wa bongo on July 15th, 2007 9:27 am

    Simon kitururu,inabidi ukubai kuwa umeshindwa,na katika swala unalojaribu kulizungumuzia juu ya utashi wa kuelewa,labda tatizo hili lipo!ni hivi mheshimiwa.
    (a)sisi walalahoi wa jua kali bongo hatuujui ubaguzi na
    wala huyo mwananchi mwenzetu hatumvui utaifa wake,bali wenzetu hao walio na asili ya ki asia huwa wanajibagua na kutubagua,sasa mbegu hizi zilipondwa na wenzetu zimekuwa sumu katika jamii yetu
    (b)mziki hapigao ni chaguo lake kwetu sio shida hili mradi anapata mkate wake huko aliko
    (c)bongo celebrity!mziki kitu gani?!mziki unaweza kulitambulisha na kulitangaza taifa kwa maana hii mziki ni kioo na ni nembo kwa jamii
    (d)Kitururu wapo watanzania wengi wanaohitangaza bongo huko ughaibuni kama vile watangazaji wa radio mbali mbali,wanamziki na beuty queen warembo lakini!tusingependa tuburuzwe kuwakubali hata kama wanafanya utumbo.
    Kauli zenu umlio ughaibuni mziangalie kabla ya kutoa maoni

  20. Comment by deo cashmoney on July 18th, 2007 7:03 am

    ubaguzi upo..kama sio mtanzania wa kwali astahili kuwa miss tanzania.ulaya au india nani ampe mweusi umiss????bongo amkeni sio ubaguzi Imeshaandikwa…black with black….

  21. Comment by Mkoba on July 22nd, 2007 1:44 am

    Huyo Rummy anatengeneza mziki wa kizungu kuwauzia wazungu, kama yeye ni mkazi wa ughaibuni, leo nyie mnampigia kelele ooh sio mbongo ni muhindi, hapigi mziki wa kitanzania,sasa mnataka atengeneze bongo flava atamuuzia nani huko uzunguni?,hiyo cd yake aliotengeneza sio kwa ajili ya soko la afrika au kwa waafrika, ni kwa wazungu wenye hela ya kununua cd ughaibuni na sio kwenu mnaojifanya wazalendo sana na kuishia kuburn mziki kila siku. kama uhindi au uarabu na kazaliwa kariakoo sidhani kama anajijutia kuwa na asili hiyo, na wala sidhani kuwa anaukana utanzania wake, nina uhakika kuwa anajithamini kwa jinsi alivyo. Nyie mnaosema kuwa ooh wahindi wa kariakoo wanatudharau sie walala hoi, wee kama huishi pale kariakoo au hujulikani mitaa ile ofcourse hata huyo mlala hoi wa mitaa ile atakuchunia pia.
    They say: “DONT JUDGE THE BOOK BY LOOKIN´AT ITS COVER”
    Get to know the person before you talk rubbish about him, labda utakuta uzalendo zaidi ndani kuliko wewe unaejifanya mzalendo sana. Watanzania wengi tu waliokwenda kutafuta maisha bora ughaibuni hawana nafasi ya kufanya kile wanachotaka, kama huyo RUMMY hana ubavu au chance ya kuimba sindimba au taarabu anatengeneza kisumni chake kwa kuimba rock n roll wee kauka tu usikonde, ni vibaya kama akijitangaza kuwa yeye sio mtanzania yungali ni mtanzania. Chungeni haya maoni yenu mnayotoa humu yasilingine na ya wakenya. Kumbukeni Tanzania hatuna ukabila.

  22. Comment by Mwaju on September 5th, 2007 1:37 am

    anayesema kwa kuwa ulaya na india hawajawahi kuwapa weusi umiss basi nasi tusiwape umiss wasio waafrika ni mbaguzi usilipe baya kwa baya lipa baya kwa jema,India waafrika watoke wapi mbona mara nyingi tumeona marekani na ulaya kuna mamiss waafrika wanawakilisha nchi zao miss world,kama kupinga akapinge bungeni kwanza,weupe weusi wote ni watanzania,watanzania hatutataki ubaguzi,hoyce temu kama alitoa mtamshi ya kumbagua miss tz 07 anafaa apewe adhabu ya kunyang’anywa passport au nyingine sheria inayoruhusu,dunia nzima itasoma kwamba watz WABAGUZI KITU AMBACHO TUMEPINGA MIAKA YUOE HATUTAKI UKABURU

  23. Comment by Mama Malaika on September 15th, 2007 10:05 am

    Hongera yake…. hapa UK anasikika na muziki wake wazungu wanaupenda sana.

  24. Comment by LIKOKO ZE MASSIVE on September 18th, 2008 6:37 am

    ebwana huyu mtu mzima yuko shikopa ile mbaya na anajina kubwa ile usipime its time wa kumpa shavu huyu man bcoz yuko frengwa kila idara.

Leave a Reply