MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

Iwe umemsikia redioni,kuonana naye mtaani,kazini au kupata bahati ya kuhudhuria kwenye shughuli yeyote ambayo Gardner G.Habash alisimama kama MC, utakubaliana nasi kwamba ni kijana mwenye kipaji katika kitu anachokifanya,utangazaji na usimamiaji wa shughuli (MC).

Kabla jua halijazama na mpaka kiza kinapoingia,kupitia radio ya Clouds Fm,sauti ya Gardner huanza kuwasindikiza maelfu kwa maelfu ya watanzania wanaokuwa wanarejea majumbani kwao baada ya siku nzima ya kazi na kutafuta riziki. Wanapofika nyumbani huwa hawaachi bali huendelea kuwaliwaza kwa habari za burudani, sinema nk huku akicheza miziki ya aina mbalimbali inayoendana na wakati uliopo. Kwa sababu kipindi chake kinaitwa Jahazi na yeye ndio muendeshaji, unaweza kumuita Captain.

 

 

Lakini wangapi wanajua ilikuwa vipi Gardner akaingia kwenye utangazaji? Unalijua neno ambalo karibuni kila siku iendayo kwa muumba yeye hulitaja? Na je unajua yeye ni manager au mshauri wa wanamuziki wangapi wa muziki wa kizazi kipya? Anasemaje kuhusu kuwa manager wa msanii au wasanii na wakati huo huo kuwa mtangazaji redioni? Katika mahojiano haya,Gardner anaweka bayana yote yaliyotajwa hapo juu na mengineyo mengi. Fuatana nasi;

BC: Kama kawaida tungependa kuanza na historia ya maisha yako kwa ufupi. Ulizaliwa wapi,lini, ukasomea wapi na mambo kama hayo.

GH: Nimezaliwa Tanga barabara ya nne tarehe 17/03/1973. Nyota yangu samaki. Nimesoma Changa (msingi), Popatlal (secondary) Dar School of Accountancy (elimu ya juu). Pia nimepitia jeshini Ruvu JKT katika ile National Service. Halafu ndio nikaanza pilika pilika za kazi.

BC: Nini kilikusukuma kuingia kwenye kazi ya utangazaji? Katika familia yako kuna mtu mwingine yeyote ambaye ni mtangazaji au alikuwa mtangazaji?

GH: Katika familia yetu hakuna mtangazaji wala muimbaji na kama wapo basi siwafahamu na ningependa tufahamiane nao.Binafsi nilikuwa napenda kuwa na umaarufu wa kufahamiana na watu mbalimbali, lakini sikujua nitafanya kazi gani ili nifikie lengo hilo. Niliuza duka, counter ya bar katika disco na kadhalika, lakini sikuona njia mpaka nilipomuona Othmani Njaidi akitangaza ITV, ndio nikagundua kuwa nahitaji kuwa mtangazaji. Baada ya hapo ndo ikawa historia.

BC: Kama DJ unafanya maandalizi gani kabla hujaanza kipindi? Hapa nazungumzia jinsi unavyopanga cha kusema,kuchagua miziki utakayopiga,commercials,jingles mambo kama hayo.

GH: Naipanga shoo ya Jahazi kwa mtindo wangu ila nasaidiana na waandaaji kupata shoo kamili. Mfano script na jinsi ya kuongea napanga mwenyewe, nadhani hapo ndo kipaji changu kilipolalia. Muziki nasaidiwa na DJ Nelly, promos za kipindi natendenezewa na DJ Venture, matangazo napewa na idara ya masoko na hata watangazaji wenzangu na viongozi wangu wakipata jambo wananirushia katika Jahazi. Kwakweli tunafanya kazi kama team. Ni raha sana.

BC: Kwa faida ya watu ambao hawajawahi kuingia au kuiona studio ya utangazaji, unaweza kumuambia ni aina gani ya vifaa vinavyotumika au unavyovitumia wewe kama mtangazaji?

GH: Inabidi waje hapa Clouds FM waone wenyewe, au waongee na Daudi (Mr Delicious) ndio mtaalamu wetu katika vifaa.Kijana mdogo lakini mtundu sana.

BC: Kwa maoni yako, ni elimu ya aina gani au kiasi gani mtu anahitaji ili kuwa mtangazaji mahiri?

GH:Elimu ya kwanza ni ile inayotoka kwa mungu, kipaji. Ukishang’amua unacho kipaji basi jitokeze bila woga, jaribu chochote mpaka wadau wakuone.Pili fanya kazi na sio udengue kisa una kipaji na ukubali kuelekezwa na kujifunza kila siku. Pia ni muhimu kusoma ukiwa na hali au uwezo.

BC: Unadhani ili mtu awe mtangazaji au DJ mzuri, ni mambo gani anatakiwa ayazingatie zaidi?

GH: Ni lazima ujiandae kabla ya kuingia katika shoo. Kama utaongelea jambo basi hakikisha unalifanyia uchunguzi wa kina na pia unakusanya mukhtasari wa shoo yako. Iwe ni kuhusu burudani, jamii au siasa,ni muhimu sana kuandaa points na sio kubwabwaja tu.

BC:Je unakumbuka ilikuwa wapi na ilikuwaje siku ya kwanza uliposimama au kukaa mbele ya kipaza sauti huku ukijua kwamba “you are on air” na maelfu ya watu wanakusikiliza?

GH: Ilikuwa katika kipindi cha Bambataa, Mheshimiwa Amina Chifupa (alale pema peponi) ndiye alinitambulisha rasmi namshukuru sana alinisaidia sana katika kazi. Nakumbuka alisema nisalimie waskilizaji nami nikatamka ‘asalaam waleikhum wasikilizaji’ .Sitasahau hilo.

BC: Lipi kuhusu kazi yako ya utangazaji unalipenda zaidi na lipi unalichukia?

GH: Clouds FM inanipa nafasi kuandaa matamasha hivyo nakutana sana na artists wakubwa wa Tanzania na nje ya Tanzania kama Koffi Olomide, Shaggy na wengineo wengi. Pia watanzania wananithamini sana na kunialika katika mambo mengi. Pia nimejuana na watu wengi wakiwemo viongozi wa nchi, sababu ya hii kazi. Naipenda sana kazi yangu.

Jambo linalonikwaza katika kazi hii ni kwamba bado vyombo vya habari Tanzania tuna uoga wa kukosoa panapostahili. Naona tunakosoa wasanii tu, lakini kuna madakrari, wanasiasa, nk. Wanakosea na twaogopa kusema.

BC: Ni watangazaji gani wa zamani na hivi sasa unaopenda kazi zao?Kwanini?

GH: Namba moja wangu ni Charles Hilary, ana sauti ya radio, ana mzaha unaofurahisha katika radio, na pia lafudhi nzuri ya kiswahili.Charles Hilary anasikilizika hata atangaze chochote. Navutiwa pia Taji Lihundi, ana busara. Pamoja na Othman Njaidi (kwa sasa yuko USA). Kwa upande wa nje ya Tanzania navutiwa na Casey Cassam (mstaafu wa american top 40) na Walt Baby Love. Hao ndo nimekuwa nawafuatilia sana.

BC: Tangu umeanza kazi yako ya utangazaji ni wimbo gani ambao unadhani umeucheza katika vipindi vyako mara nyingi kuliko yote? Kwanini?

GH: Nafikiri nimecheza nyimbo nyingi mara nyingi lakini nakiri kuwa wapo wasanii ambao nawapa mchango mkubwa zaidi. Mfano Matonya (sababu ni mfano mzuri kwa msanii mdogo, alitoa albamu mbili na hakufanikiwa lakini hakukata tamaa mpaka albamu ya tatu akatoka). TID (sababu nadhani ni perfomer mkali Tanzania). Banana (sababu nadhani ni male vocalist mkali Tanzania) na Lady Jaydee (sababu ni female vocalist mkali Tanzania na pia ana kiswahili fasaha katika nyimbo na pia anachoimba kinagusa hisia za watu moja kwa moja)

BC: Je kuna wimbo wowote ambao unakumbuka kuucheza ulipoanza kazi ya utangazaji na bado unaucheza mpaka hivi leo?

GH: Hata sikumbuki.

BC: Nchini Tanzania kumekuwepo malalamiko kadhaa kutoka kwa baadhi ya wasanii kwamba watangazaji kama wewe, wanapokuwa ndio tena mameneja wa baadhi ya wasanii (wewe ni meneja wa baadhi yao) kunakuwepo na upendeleo fulani kuhusu air time mnayompa msanii fulani kulinganisha na mwingine. Unaliongeleaje suala hili? Unadhani kuna madhara yeyote yanayotokana na watangazaji kuwa pia mameneja wa wasanii?

GH: Nadhani mtu yoyote anayo nafasi ya kufanya kazi yoyote bila kujali jinsia au yuko wapi. Cha msingi ni awe na uwezo kiutendaji. Siku hizi waandishi ndio waandaaji wa mashindano ya urembo katika vitongoji hapa Tanzania, je wasipewe nafasi kisa wao ni waandishi? Wacheza mpira ndio wanakuwa makocha, watu mbalimbali maarufu wanagombea viti katika siasa nk. Nafikiri tusichague sura bali tuangalie mwenye uwezo apewe nafasi afanye kazi aliyochagua. Kama kuna ubaya fulani wa mtangazaji kuwa meneja wa sanaa, basi tuuseme ili yafanyike marekebisho.Mimi binafsi nasimamia baadhi ya kazi za wasanii kama Lady Jaydee, Mr Blue. Pia natoa mchango wa ushauri kwa wasanii wengine hapa home kama TID, Ferooz, Mandojo & Domokaya, Q-Chief… nk

Ukweli ni kwamba msanii anapewa upendeleo kutokana na hadhi, mafanikio na ukubwa wake. Mfano Michael Jackson na Akon wote ni artists wazuri, lakini MJ anaweza kupata attention zaidi ya Akon sababu ya nguvu aliyonayo. Na hata katika nyimbo zipo zinazopendelewa zaidi kutokana na uzuri wake na nguvu ya msanii kwa jamii. Msanii mzuri lazima atatoa wimbo mzuri na lazima utapigwa zaidi kwa sababu hata wasikilizaji wanapenda kusikia kitu kizuri na sio ilimradi tu. Hiyo ipo kote duniani na sio katika muziki tu.

BC: Unapokuwa haupo studio au katika maandalizi ya aina yoyote ile kwa ajili ya kipindi chako huwa unapendelea kufanya nini?

GH: Nakuwa home katika tv au theatre katika movie.

BC: Malizia sentensi ifuatayo tafadhali:

BC: Msemo au neno ninalolitumia sana kila siku ni………..
GH: Umeona Bwana.

BC: Unatoa ushauri gani kwa mtu yeyote anayetaka kufanya kazi ya utangazaji?

GH: Usiige, gundua hisia yako, sikiliza sana wenye uwezo ili ujifunze. Sifia zaidi kuliko kukosoa kwani tuko katika hatua za kujenga bado. Na mwisho promote vipaji na bidhaa za nyumbani.

BC:Asante sana kwa kutupa muda wako. Tunakutakia mafanikio mema katika kazi zako.

GH: Shukrani kwenu pia.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

28 Responses to “NDANI YA JAHAZI NA GARDNER G.HABASH”

  1. Comment by Zaynab on August 2nd, 2007 1:35 am

    Nimefurahi kusoma kutoka kwa Gadna! Huwa nafurahia kusikiliza vipindi vyote anavyoendesha. Ukweli ana kipaji cha kuvuta hisia za wasilikilizaji wake. Nimefurahi pia anamsifia Lady JD kwani kwa upande wangu she is the best natumaini ataendelea kumpa support na pleeeease Gadna dont break her heart!!!!!!! Nampenda sana sana Lady JD. Yani namzimia kichizi.

  2. Comment by Sarah Bairu on August 2nd, 2007 4:53 am

    Nimependa kumuona gadna napenda anavyotangaza na nilimpenda zaidi baada ya kuamua kumchukua jumla kipenzi chetu Jidee na kuwafunga midomo wambea nawapenda wote na naomba kifo ndio kiwatenganishe keep it up boy

  3. Comment by toxeeq on August 2nd, 2007 7:33 am

    i really like you gadner,ur one of the people that i respect the most.yeah nobody is perfect but we have to look in ones contribution to the society.Big up brother!!

  4. Comment by bessy on August 2nd, 2007 8:45 am

    this is such a good explainations.. the guy is very good. i thing he is the best thing on radio for now. i wish u could ask him more questions about his wife lady jd.

  5. Comment by millard on August 2nd, 2007 9:19 am

    neno moja tu, NAMKUBALI
    Captain ana zaidi ya KIPAJI, VOCO imetulia flowing nzuri, HAKIKA kajaliwa KIPAJI. inshort jamaa YUKO FIT ile mbaya!

  6. Comment by nsia on August 3rd, 2007 4:04 am

    Gadner, ur a great radio presenter..and u have an amazing voice, captivating and very entertaining.
    salute!

  7. Comment by Asia on August 3rd, 2007 2:31 pm

    Duh, wt cn i say bou ds dude ryt here?
    namkubali c kipole pole.. UNAONA BWANA!
    sauti nzuri, lafudhi nzuri na mtiririko ndo usibonyeze m2 mzima… yani u r hot more than fire..!
    ninachoamini una zaidi ya KIPAJI na najua wajua kama unajua kuwa una kipaji na najua wajua jinsi ya kuki2mia na kututeka mashabiki wako…!
    we tumuvuzishie tu hayo majahazi na kwa hakika twaenjoy!
    kip t up swahiba…!

  8. Comment by Neema on August 5th, 2007 11:18 pm

    Gadna interview ni nzuri, ila mimi naona it’s not fair for other artists. By saying that I mean for those who you are not managed. I do believe one person can do two jobs perfect, but I still believe to be a manager of artists and at the same time a Dj who decide what songs should be played in his show, most obviously you’ll be bias, thinking of your own income, the more they succeed the more YOU succeed. For that I think being a manager at the same time a DJ it’s kinda unfair for those you are not managed. Just my point of view.

  9. Comment by Maisarah on August 6th, 2007 3:54 am

    Gadna is great always playing different songs sidhani kama kwenye kipindi chake anapiga nyimbo za watu anaowasimamia so is not a bad thing to have two responsibilities as long as unafuata procedure za kazi yako

  10. Comment by KIK on August 7th, 2007 4:43 am

    UKO JUU KIJANA NA BORA umewakata mkilimi

  11. Comment by KakaPoli on August 8th, 2007 8:47 am

    Muungwana mi namkubali kwa 100% Na napenda kuwasiliana na yeye, so Jr. kama hutajali muungwana GH anitwangie tu hapa 0715 253 653.

  12. Comment by Matilda on August 8th, 2007 11:58 am

    Ohh yes!Namkubali G wa H.Huwa anamvuto wa kusikilizwa na watu.

  13. Comment by Anna on August 8th, 2007 9:55 pm

    I do appreciate your work brother keep It up and don bother what other people say about your work!!!!Good job Gardner

  14. Comment by Buxom Lady on August 9th, 2007 6:29 am

    ANAKUBALIKA!NAMKUBALI Sana sana! Keep it up.. Jaribu TV kaka Waweza kuwa Ryan wa American pop idol/E News one day..Inshaallah!

  15. Comment by jey on August 15th, 2007 7:04 am

    kwa kweli namkubali sana Gadner naweza kusema ni mmoja wa watangazaji ambae huwezi kuboreka hata ukimsikiliza asubuhi hadi jioni haboi.anajua nini audience wake wanataka ana lugha ya kushawishi umsikilize hata kama ulikuwa umechoka keep it up.

  16. Comment by anny mwiya on August 15th, 2007 12:13 pm

    yap!!! jamaa anatisha nampa big up sana tuu kaza buti ma man…. your rally smart endelea hivo hivo.. na jide please dnt hurt her!!!! cthao……

  17. Comment by anny mwiya on August 15th, 2007 12:28 pm

    ola tudo bem….epa vc e d mas n tem de falar mas so vo dizer vc e baabuuu kubwa sana ……obrigado tem vir ai mozambique par pasear……

  18. Comment by Sanshau on August 29th, 2007 5:32 am

    Jamaa yuko feet sana, ana kipaji cha hali ya juu sana.kwa kweli anakubalika na yuko makini,sio mtu wa blaa blaa wala majungu.

    Keep it up Brother

  19. Comment by ANNA G on September 5th, 2007 6:55 am

    Yeah for real i do appreciate the guy is good and he know how to face the audince.Keep i up men.
    Salute!

  20. Comment by ukende on September 6th, 2007 10:03 am

    i appriciate u man, keep it up.unaweza tena sio kipolepole…

  21. Comment by anny mwiya on September 6th, 2007 12:13 pm

    about me anny yaani jamaa ni smart wa smart!!!muombe mungu akulinde milele na milelee your really man………..all the best!!!my friend life its hard and ur tryng a lots to do your best!! just keep it up and GOD HE GOING TO HELP YOU ALWAYSSS FOREVER NDA EVER JUST DO IT NON STOP FOREVER NAD EVER!!!!! Mungu atakulinda milele na milele au sio bwana!! KEEP IT UP FOREVER AND EVER!!!! GOD BLESS YOU MY FRIEND!!!!! THANXXXXXXX

  22. Comment by amina on October 30th, 2007 7:29 am

    umeona bwana,,,,namuaminia huyo

  23. Comment by Raiya on June 10th, 2009 5:01 am

    I do appreciate u guy ur good looking wow.

  24. Comment by med on June 11th, 2009 12:09 pm

    poa kaka nakukubali sana nakumbuka uliokoa kipaji cha inpert haroun babu na gangwe mobb safi man cdhani km kuna msanii atakae thubutu kukulaumu eti aujaibeba bongo freva na wasanii wake kaka.umeona bwana naipenda sana hii umeona bwana full kaka umeona bwana.kuna ki2 k1 ningependa uwaeleze hawa ndugu zote wachungaji wasichanganye dini na siasa naona wanatumiwa sasa. nitakupa stori vzr time nyingine unaona bwana.

  25. Comment by Victor on November 11th, 2009 10:01 am

    Kazi nzuri ndungu mtangazaji.Kila la heri

  26. Comment by aishou on February 21st, 2010 9:01 am

    mm ni ni mrundi na mtangazaji wa hapa buja tena napenda sana kusoma glob zako .so mm nampa hongera sana huyu gadna kwa kazi zake

  27. Comment by aishou on February 21st, 2010 9:02 am

    napenda sana kazi zake

  28. Comment by Frank Boniface on March 2nd, 2010 12:35 pm

    Bro we ni mkali sana i really appriciate your job.

Leave a Reply