Kituo cha televisheni cha Chanel O jana kimetangaza majina ya wanamuziki na video zao za muziki waliochaguliwa kuwania tuzo ya 2007 Channel O Spirit of Africa Music Video Awards. Jumla ya wasanii 46 kutoka nchi 12 za Afrika ndio wameingia katika fainali hizo.
Kutoka Tanzania, msanii Juma Nature kutoka kundi la Wanaume Halisi ndiye msanii pekee aliyefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho. Ameingia kupitia video ya wimbo wake ujulikanao kama Mugambo. Kura za watazamaji na wapenzi wa muziki ndio zitaamua mshindi. Kwa orodha kamili ya waliochaguliwa,nchi wanazotokea na jinsi ya kumpigia kura Juma Nature bonyeza hapa. BongoCelebrity inamtakia Juma Nature kila la kheri.!
Feedback / Comments
3 Responses to “CHANEL O SPIRIT OF AFRICA VIDEO AWARDS”
Leave a Reply


sending...
Hongera sana Nature.Nakutakia kila la kheri ushinde uiweke bongo kwenye ramani.
Juma, Kweli tumekubali mambo yako yametulia ” keep it up” Watanzania tujitokeze kwa wingi kumpigia kura Juma Nature: Kwani UMOJA NI NGUVU!!!!!
jitahidi usafi kakaa