MBARAKA MWARUKA MWINSHEHE!

Iwe ulizaliwa enzi za uhai wake au baada ya kifo chake, jambo moja ambalo wote tunafanana ni kwamba ukisikia muziki wake sio ajabu utatikisa kichwa, kutabasamu, kucheza au kurukaruka. Ukishaguswa na muziki huo sio ajabu ukajiuliza swali gumu; kwanini mungu akamchukua Mbaraka Mwaruka Mwinshehe baada ya ile ajali ya gari nchini Kenya tarehe 13 Januari mwaka 1979? Angelikuwa hai nani asingependa kusoma mahojiano yake? Inasemekana Mbaraka Mwinshehe alikufa kutokana na kuvuja damu nyingi na asipatikane wa kumchangia damu ili kuokoa maisha yake. Alifia hospitalini Mombasa.

 

Hayati Mbaraka Mwinshehe akicharaza gitaa na kuimba!

Uwezo wake wa kutunga nyimbo, kupanga muziki na kudonoa gitaa hauna mfano wake mpaka sasa. Ukimsikiliza leo unaweza dhani kapiga gitaa hilo juzi kumbe ni miaka chungu mbovu iliyopita. Kizuri zaidi ni kwamba upigaji wa gitaa hakufundishwa na mtu bali yeye mwenyewe. Akiwa bado kijana mdogo kabisa alicheza muziki uliokuwa unajulikana kwa jina la “kwela”(asili yake Afrika Kusini) na bendi iliyojulikana kama Cuban Branch Jazz.

 

 

 

Mbaraka Mwinshehe akimvisha mke wake, Amney Shadad, pete ya ndoa. Hiyo ilikuwa tarehe 17/3/1972 mjini Morogoro.
Mbaraka alianza kujitengenezea jina kwenye medani ya muziki wakati alipokuwa mmojawapo ya wanamuziki waliokuwa wanaunda bendi maarufu ya Morogoro Jazz kati ya mwaka 1964 mpaka 1973. Baadaye ndipo alipoanzisha bendi yake mwenyewe iliyojulikana kama Super Volcano mwaka 1973. Alidumu na kutamba na Super Volcano mpaka mauti ilipomfika miaka sita baadaye. Kuimba alijifunza kutoka kwa Salum Abdullah, mwanzilishi wa Morogoro Jazz ambaye baadaye alijiengua na kwenda kuunda Cuban Marimba Band.

Hii hapa ni baadhi tu ya miziki ya Mbaraka Mwaruka Mwinshehe ambayo inatufanya tuendelee kumkumbuka daima. Lala pema peponi.

 

SHIDA

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 

 

EXPO 70’s PART I

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 

EXPO 70’s PART II

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

 

 

Mbaraka akifanya vitu vyake huku amezungukwa na mashabiki wake.Tizama walivyotulia wakipata ujumbe.

 

Jogoo la shamba linaweza wika mjini?

Endelea kupumzika pema peponi Mbaraka Mwinshehe.

Picha kwa niaba ya Michuzi. Miziki shukrani zimwendee Steve Mugiri.

 

 

 

 1. gabriel, 22 August, 2007

  kwanza nashukuru kwa kuleta hii habri ya star mtanzania halisi ambaye alikuwa mstari wa mbele kupiga na kuendeleza muziki wenye identity ya kitanzania na vionjo (mapigo) vya tanzania originally na siyo mambo ya kikongo
  hakika tungekuwa na wanamuziki wenye moyo na vision kama ya marehemu mbaraka basi wacongo na wengine wangekuwa wanajivuna kwa kuiga mziki wetu na siyo sisi kufuata fuata wao kwa kuiga vionjo ,mitindo na mpaka namna ya uimbaji na madoido utasikia watu wanatajana majina ,mara pededjee,na ala zile za kitanzania siku hizi wanaiga za kikongo completetly tena wasivyo na aibu wenyewe wanajivuna kwamba wanapiga sebene tena sebene ya nguvu,loh!
  ukija bongo flava ndio kabisa aibu tupu
  wasanii tufuate nyayo za wazee wetu mbaraka mwishehe,mlimani saida karoli,msondo ,bima lee,washirika,chee mundugwao,maneti, na wengine wengi tuu amabao usiku na mchana waliupenda utanzania na kupiga mziki wenye vionjo vya kwetu na siyo vya kuiga mziki amabao uliweza simama peke yake na mtu wa tamaduni tofauti akiusikilza tuu anaweza kuidentify na siyo kushangaa kwamba mziki gani huu wa tanzania mbona ni kama wa kenya ,mbona ni wenge muzika hao au mbona ni hip hp ya marekanai ,au mbona ni kwaito hiyo!
  tuache kuiga ,tusijione bora kwa kuwa wenge muzika wa tanzania ,au mafikizolo wa tanzania au mariah carrey wa tanzania .ni lini jamani tutaamka na kuwa na chetu wenyewe na tjivunie !
  amkeni
  kazi ya sanaa ni creativity hata hao tunaoiga walicreate kwanza hawakuiga

 2. gabriel, 22 August, 2007

  mwandishi naomba uniruhusu ni toe maoni yangu kuhusu ulichosema hapao juu kwamba mungu alimchukua mabaraka mwinshee.
  hivi,naomba nikuulize haya maswali .

  ni kweli kwmba mungu anachukua watu kwa kuwaua katika ajali kama hiyo ya mabaraka ni mungu gani huyo anawapenda watu eti akitaka uende kwake anakuua? tena cha kushangaza huyo mungu amemwua mbaraka mwishehe kinyama kama hivyo ,mmh! ili tuu amchukue aende kwake

  umeshawahi kufikiri ni kwa nini mungu awachuke watu kutoka duniani (sehemu aliyotutengenezea ili tuishi)
  ili waende wapi kisha wachukua ?
  hivi doesn’t it make sense to you kwamba mungu na uwezo wake woote wa kialmity anauwezo wa kuumba kila aina ya mtu anayetaka au anyempenda yeye yaani kama ni mbaraka mwinshehe basi anaweza kuwaumba hata milioni moja kwa malengo na kazi anayotaka yeye na sioni kwa nini mungu huyo aje achukue mtu hapa duniani na hali yeye anauwezo wa kuumba,mbali zaidi anakuua kwanza kinyama halafu ndio anakuchukua,
  hivi ni kweli mungu akikutaka anakuua kwanza? je kuua ni sifa mojawapo ya mungu ?
  what sense would it make kwamba mungu alimpenda sana mbaraka mwishehe kwa hiyo akapanga ajali ya kinyama ya gari ili amwue tena kinyama kama ulivyoandika ,kisha hapo sasa ndio amchuke aende kwake

  hivi mimi sifahamu bwana mwandishi ,kazi ya mungu ni kuua? au kifo ni kazi ya mungu? kama ndio hebu nifahamishe ni nania mwenye kazi ya kuumba,kulinda,kuponya,kufariji,kuto maisha kwa wandamu.is it mungu au shetani?
  mimi nilipata kusikia mahali kwamba mtu akifa anarudi k mavumbini sijui kama una ka idea na hili? na kama hii ni kweli sasa mungu alimchukua mbaraka mwinshehe ili aende wapi huko?
  pia nilisoma mahali kwamba mungu alitengenza dunia ,ulimwengu kwa ajili ya mwanadamu aishi humo afurahie maisha na kumtukuza yeye sina uhakika kama ni kweli juu ya hili lakani kama ni kweli je ni kwa nini sasa mungu huyo aliyemtengenezea mwandamu mahali pake pa kuishi akuchukue tena nisichokielewa anakuchukua kwa staili ya ku-kuua kama maremu mabaraka sasa sijui anakupeleka wapi
  mwandishi naomaba kiungwana tuu unifahamishe only if you have a little idea of justifying kwamba mabaraka alichukuliwa na mungu
  asante sana

 3. Bob Sankofa, 24 August, 2007

  Hii ndiyo picha yangu ya kwanza kuiona yenye taswira ya Mbaraka. Alikufa mwaka moja kabla ya mimi kuzaliwa, nimekulia kwenye nyumba ya wapenda muziki na toka nikiwa mdogo nilikuwa nikisia sana jina la Mbaraka Mwinshehe na kusikia kazi zake lakini sikuwahi kuona taswira yake. Hii ni ya kwanza katika miaka 27. Asante Bongo Celebrity.

  Pamoja!

 4. Farida, 24 August, 2007

  Nadhani kuna kila sababu ya kumkumbuka Mwinshehe,muziki wake haushi hamu hata kwa watoto watakozaliwa,Wanamuziki jaribuni kuiga mfano wake siku zote mtakuwa mpo juu hata kama hamtakuwepo duniani you will be remembered by next and next generation.Thax Bongo Celebrity tumemjua vizuru gwiji la muziki.

 5. stambuli, 29 August, 2007

  Nashkuru kwa kutuwekea hiyo picha hapo juu,naungana na muungwana aliyetangulia kwa kukiri kwamba hata mimi ni mara yangu ya kwanza kuona wajihi wa mbaraka mwishehe,ni mmoja wa wapenzi wa nyimbo zake tangu nilipopata fahamu ktk dunia hii,huwa namfananisha na Jabali la muziki-Mar.Marijani Rajab kwa kweli uwezo wa kutunga,kuimba,kupiga ala ya muziki na kupangilia muziki ulikuwa ni wa hali ya juu.Nyimbo zao hazichuji utafikiri albamu imetoka leo.Keep it up_bongo Celebrity

 6. ndesanjo, 01 September, 2007

  Ukiacha muziki ambao aliuweza (kuandika mashairi, kupanga vyombo, na kudonoa hilo gitaa), nimegundua pia kuwa alikuwa anajua kuvaa. Na pia alikuwa na “jicho,” si unaona picha ya mwenzi wake?

  Asanteni kwa kutukumbusha hazina moja ya taifa letu.

 7. Ally, 07 September, 2007

  Ebwana ndio mi mwenyewe sijawahi kuona picha ya huyu bingwa mi sinikadhani savimbi hahaha dah baab kubwa mi namkubali sana nyimbo zake mi mwenyewe bwa mdogo lkn nazikubali kama zimepigwa jana nyimbo ujumbe bwana japo ule mdundo ukiusikia unajua tena hii kitambo!ndio mzee.

 8. kabukalilo, 23 October, 2007

  sijui hata nianzeje,lakini niseme tu kuwa nyinyi mna AKILI za ziada,yani mna akili pita kiasi kwa jinsi mlivyofikiria hatimaye kuamua kuitoa historia na picha za Mbaraka Mwinshehe,hakika mimi binafsi napenda na ninasikiliza sana miziki ya Mbaraka lakini sijawahi muona katika picha mana alikufa miaka miwili kabla sijazaliwa, kwahiyo hii ni mara yangu ya kwanza kuiona picha ya mbaraka,aisee!! kumbe kidogo alifanana na mzee jangala huyu muigizaji maarufu na mkongwe hapa nchini,

  nimefurahi na nimewapenda sana mzidi na mzidi,naamini kama mmeweza ya Mbaraka basi mnaweza kutuonyesha ya Nico Zengekala wa iliyokuwa Juwata Jazz

 9. Freddy Macha, 01 November, 2007

  Wakati nikisoma kidato cha tano Mzumbe mwaka 1973; ndiyo mara ya kwanza kukutana maso kwa maso na Mbaraka Mwinyishehe. Alikuwa na desturi ya kuja kupiga shuleni kwetu na bendi yake. Ikifika haftaim alikuwa akituachia vijana (enzi hizo nikipiga na bendi ya shule iliyoitwa “Earthquakes”) vyombo ili tujifae. Akitupa moyo.
  Mara ya kwanza kabisa, basi kupanda jukwaani na bendi, ilikuwa kwa ihsani ya marehemu Mwinyishehe, Simba wa Morogoro, msanii, asilia Mtanzania, fahari ya Wabongo. Mtunzi. Mpenda watu. Pongezi na heko kwa kutuletea habari zake…

 10. Oganzo, 10 November, 2007

  Ahsante sana kwa kutukumbusha mwimbaji huyu ambaye alipendwa Afrika nzima. Ningependa kusikia baadhi ya nyimbo zake. Huku nilipo, sina jinsi ya kusikia nyimbo hizi ila kupitia kwa Bongo celebrity. Pongezi na Heko!!

 11. Qasem Al-Majita, 12 December, 2007

  Kama alivyo Pele kwenye soka la dunia, Muhammad Ali kwenye ndondi za dunia, Shaaban Robert kwenye fasihi ya Kiswahili, Mbaraka anabaki msheherekewa (celebrity) wa nyakati zote. Alipiga gitaa na kuimba – kitu amvacho wachache wa bongo flava wanadiriki kufanya. Kwanza Bongo flava nini kama siyo maadili ya kutuelekeza kupoteza utamaduni wetu. Naungana na mdau Gabriel hapo juu anayeshauri tufuate mifano ya kina Mwinshehe, Saida Karoli, Maringo na wengineo.

  Maringo – uko wapi? Udumu (Ndolela…)

 12. Mkabahati, 15 January, 2008

  Jamani,
  Sijui niseme nini kuhusu huyu Super staa wetu. Well, mi nilisikia nyimbo za Mbaraka for the fist time on a long journey from Dar to Botswana tulikua kati kati ya Zambia huko. Nakumbuka i asked my dad a lot of questions about the guy..wimbo wake wa mtaa wa saba really stood out. Since then nina cds mbili za his hits which i listen to on my lazy days. Thank you so much Michuzi for bringing our Morogoro Legend back..we all miss him soo much. I bet huko aliko he’s doing live shows 24/7! By the way aliacha watoto hata..?

  Stay blessed.

 13. Mama wa Kichagga, 16 January, 2008

  AMA KWELI KIFO KAUMBIWA MWANADAMU! BAADA YA MIAKA 60 NA SISI WOTE HAPA BC TUTAKUWA TUMEKUFA WOTE! TUISHI KWA HAKI NA AMANI HAPA TWAPITA TU NI KITUO CHA DALADALA HIKI TUSIJISAHAU JAMANI!

  Sauti, nyimbo na maadili yaliyomo kwenye tungo alizoacha huyu shujaa wetu, Mazalendo na mwanamapinduzi Mbaraka Mwinshehe vitadumu milele na ni kielelezo cha mchango wake kwa jamii ya watanzania ndani na nje ya nchi.

  Wakati umefika sasa tubadilike wote na tufanye kazi kwa faida ya vizazi vijavyo! Naamini wapo wazalendo wengi sana Bara na Visiwani waliokuwa na vipaji hivi na ambao hatuachi kuwakumbuka mara tusikiapo zilipendwa (bado zinapendwa haswa).

  Wazo langu hapa ni uwezekano wa kuwa na MAJUMBA YA MAONYESHO MBALIMBALI (Jumba la historia ya taifa, NK NK), liwe kubwa kwelikweli na tuhifadthi mambo haya yote kuanzia mimea, wanyama wetu tulionayo, tamaduni zetu, watu maarufu.

  Shughuli zinazoweza kufanyika ni pamoja na:

  a: kwanza kabisa maeneo haya yasiwe na kiingilio ili kumpa nafasi kila atakaye kuingia/kutembelea asiwe na kikwazo

  b: watu binafsi watengewe maeneo ya biashara na walipishwe kodi ili mapato yatumike kuendeleza mradi husika

  c: Biashara za vyakula mbalimbali/restaurants, maduka ya nguo na vitu mbali mbali za KITANZANIA TU JAMANI NA SIO VINGINEVYO KWANI HII ITAKUWA NI SEHEMU YA UTAMADUNI WETU, MADUKA YA BIDHAA ZA MUZIKI, MADUKA YA VITABU VYA HADITHI NA SIMULIZI ZA KITANZANIA NA WATU MAARUFU WALIOLITUMIKIA HILI TAIFA KM BABA, MWANAMAPINDUZI, MUWAZI, MZALENDO, …………..& MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE, MWANAMKE WA SHOKA BIBI TITI MOHAMED, MBARAKA MWINSHEHE NA WENGINE WOTE WALIOTEMA CHECHE ZA MAENDELEO HAPA NCHINI NA TAARIFA ZAO KAMILI. PIA HATA WALE WALIOFANYA VIBAYA TUNAWEKA HISTORIA ZAO ILI VIZAZI HADI VIZAZI VIJIFUNZE!

  FAIDA ZA MIRADI YA NAMNA HII NI PAMOJA NA:

  1. Kubooresha utalii (sio kila mtu anataka kwenda mbugani bwana)

  2. Kuwa kama vituo vya Elimu kwa wanafunzi na watafiti, wageni

  3. Kuwa na maeneo ya kutembelea siku za week-end kwa wakazi

  4. Kutengeneza ajira (wahudumu ndani ya mradi)

  5. Kuongeza mapato – ya sekta mbalimbali km uandishi, uimbaji-kanda, watu binafsi(biashara) nk

  6. Kuwa na mahala pa mapumziko kwa kuchangamsha akili wananchi ili kupunguza “Mifadhaiko (Stress) ya maisha” na kujenga mishikamano ya familia (matembezi ya familia).

  7. Kuhifadhi historia yetu

  JAMANI NAONA NIISHIE HAPA MAANA NIKIWAZA SIKUBALIANI NA HII HALI YA UMASKINI NA MFADHAIKO WA AKILI TULIONAO KABISA.

  TUNAZO RASILIMALI NA VITU VINGI VYA KUFANYA KILA MMOJA WETU NA KIWANGO CHAKE CHA ELIMU HATA KAMA NI CHEKECHEA AKAPAONA HAPA DUNIANI KUWA NA YEYE ALITAKIWA SIO KUISHI KAMA MGENI KISA MAISHA HUWEZI KUYAMUDU!

  HEBU KILA MTU ASIMAMIE VIZURI NAFASI YAKE NA AMUWAZIE MWENZAKE ZAIDI YA ANAVYOJIWAZIA YEYE!

 14. damassan, 29 March, 2008

  ivyo jamani hakuna hata vidio crip ya mbaraka mwishee,kwani alikwenda japan,ujerumani ivyo haziwezi kupatikana dvd au vcd kweli inawezekana jamaani, thenk’s mr michuzi kwa picha za king of lumba bong.

 15. watubwana, 19 October, 2008

  siri ya mtungi aijuaye ngata.MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.

 16. joseph abbas, 20 December, 2008

  nawapongeza san wadau kwa kujitokeza kupongeza nyimbo za mbaraka mwinshehe,kweli zinatisha.huyu jamaa alikuwa na kipaji cha aina yake.mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,amina.

 17. joseph abbas, 20 December, 2008

  wimbo wake wa “shida”ndo unanipa sana hisia za kuendelea kusikiliza sana nyimbo zake.mimi nawaomba wasanii wajaribu kuziimba tena nyimbo zake kama wanavyoziimba sana nyimbo za marijani rajabu.huu ni ukweli kabisa,,,,hakuna upinzani na nyimbo hizo kwa sasa.isipokuwa nyimbo za sasa hivi ni uhuni mtupu…….afanaleki…..!!!!!!!kifo hakina huruma…………

 18. Khalid Magram, 29 December, 2008

  Ahsante sana kwa kunikumbusha nilikotoka. Nakumbuka huu mziiki wakati napata mloo wa mchana hapo Gerezani mama ntilie.

 19. Nikolausi Mushi, 15 March, 2009

  Unapomzungumzia Mbaraka Mwinshehe, ni kama unavyomzungumzia Robert Nesta Marley au Bob Marley pale Jamaica. Mbaraka was an authentic and a gifted musician that our country has ever had in some decades, he was and still is, in my opion, a LYRICAL GENIUS. God gives and takes aways. RIP

 20. Loserian Stefano Mollel, 23 March, 2009

  Nimefurahi sana kupata kumbukumbu ya Mbaraka Mwinshehe Mwaruka. Hakika mpaka sasa sijapata mwanamuziki aliyechukua nafasi ya mbaraka moyoni mwangu. Nyimbo zake kama Expo70, Ester wangu sikiliza dhamani ya mapenzi, Jamani Morogoro,Hoyee hoyee yapendeza mji wetu mkuu Dar Es Salaam n.k. Hakika hazijatokea tena. Alikuwa ni mwimbaji anayetulia na kutunga muziki na sio kama sasa ambapo kijana anaingia studio na kuimba maneno anayojua mwenyewe na kustukia wimbo unapotea baada ya mwezi mmoja. Hao ndiyo wanamuziki tunawaita MOTO WA KUOTEA MBALI

 21. GEOFFREY KUMBURU(BLACK JEFF), 05 April, 2009

  KINACHONISIKITISHA MPAKA LEO NI MAZINGIRA YA KIFO CHAKE.ALIKUWA NI MMOJA KATI YA WATU WALIONIFANYA NIPENDE MUZIKI NA HATIMAYE KUWA MWANA MUZIKI.KILA MTU AMEZALIWA PEKE YAKE,NA AKIONDOKA HAKUNA WA KUZIBA PENGO LAKE.MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI MBARAKA MWISHEHE.MUNGU AWABARIKI MAMA AMNEY MBARAKA,RAFIKI YANGU TAJI MBARAKA NA FAMILIA NZIMA YA BINGWA HUYO,BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE,AMEN.

 22. Patrice A. Massawe, 27 August, 2009

  Kweli Mbaraka Mwinshehe kifo chake kilinihuzunisha sana. Nilikuwa ninamsubiri kwa hamu nijue kipya alichotoka nacho nchini Kenya. Badala yake nikajikuta tunapokea Mwili wa Mpendwa wetu, Msanii mahiri aliyekuwa anapendwa na kila kada kuanzia watoto hadi wazee. Cha kufanya ni kuenzi kila alichokifanya hapa dunia. Mungu ailaze roho yake Mahali pema Peponi.

 23. ched, 12 September, 2009

  mungu amlaze mahali pema peponi na penda sana nyimbo zake ,mashemeji wa ngapi,shida,tuliachana vipi,uzuri si hoja pia nampenda mwanae taji mbaraka
  asante

 24. wa morogoro, 06 October, 2009

  mungu amuweke mahali pema peponi,he is legend.

 25. GEOFREY, 07 October, 2009

  MIMI SI MTU WA UMRI ULE ALIOKUWA AKITESA MBARAKA LAKINI NIMEANZA KUFUATILIA NYIMBO ZA MBARAKA NIKIWA NA MIAKA 7 MWAKA 1989 KWA KWELI TANZANIA TUMEPOTEZA HAZINA YA MUZIKI.MUNGU AMPOKEE UKO ALIKO.

 26. stevembobo, 13 October, 2009

  R.I.P
  Mwaluka

 27. magogo, 17 February, 2010

  Kwanza ninakupongeza kwa kumkumbuka mtu muhimu katika fani hii ya muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla,kwa kweli nyimbo zake ukizisikiliza zina ujumbe ambao haushi maana nina maana kwamba maana zake hizo nyimbo zinanyakati tatu(3) wakati uliopita,wakati uliopo na wakati ujao(zilikuwa na maana zinamaana na zitakuwa na maana)mpk mwisho wa Dunia kwa kweli tumepoteza MSANII MUHIMU MNO,nashauri kwamba hawa WANAMUZIKI wetu wa sasa kabla ya kutoa nyimbo zao kwa HADHIRA wafikirie ujumbe uliopo ktk huo wimbo wake na utawagusa vp jamii,pia wasikilize kwanza nyimbo za nguli huyo ndipo watoe nyimbo zao MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA NA PAZURI PEPONI NA AMUEPUSHE NA ADHABU YA KABURI, AMINA.

 28. Koronya, 06 March, 2010

  Kuna kurasa ya Mbaraka Mwinshehe kwenye facebook na mafans Watanzania ni watatu tu.

 29. JOSEPH MASAJE, 10 January, 2011

  Ama kweli kifo we nimbaya kwa kumchukua kipenzi chetu MBARAKA MWINSHEHE bado tunakumbuka tungo zako nyinmg sana kama mtaa wa saba nanyingine nying sabna

 30. AUGUSTINE MRAMBA, 23 January, 2011

  Ama kwa hakika kifo hakina huruma.kiliweza kutupokonya kati ya magwiji wa mziki wa zilizopendwa.Tungo zake ziko na mashairi mazito ambayo yanahusu maisha tunayo ishi.Hata kule congo wanamfahamu kwa hilo.ama kwa kweli miziki ya zama ina utamu wake.anakumbuka kibao kama ntamtuma mshenga,shida,urafiki wa mwisho wa mwezi,ushamba umemtoka ,tina turudiane,sululu ya moro,pole dada,jogoo la shamba,baba mdogo nk nk,….aah Mungu ailaze roho yake mwinishehe mahali pema peponi.

 31. rumba historian, 18 September, 2012

  huyu ni bingwa kweli.nalianza kumsikiliza
  nikiwa na umri wa miaka mitatu,kibao chaka
  shida alikipenda sana babangu ambaye sasa
  marehemu. miziki yake huleta kumbukumbu bomba! ALIJARIBU SANA Charles lay kasembe
  kuindeleza bendi lo lakini masikini naye
  katuaga,kwetu kenya tunamuenzi mno.lala pema
  mzee. lakini vipi mwanawe mhutaji mbona hasikiki. ……..sululu oye.mahoka hoye!!!

 32. Eradius kahamba, 27 November, 2012

  Pongezi nyingi kwenu kwa kutuleta na kutukumbusha ya wenye hakiri na vipaji sio wengine bali ni Mbarack munshehe hakika makubwa kafanya hasa kuitangza nchi katka nyanja za sanaa bac tufuate nyayo zake kuisifia Tz, Mungu amlaze mahari pema Awesome Mbarack munshehe.

 33. Richard Mchina, 16 February, 2013

  Nawashauri vijana wa leo wasijifanye masupa staa wakati hata kupiga gitaa hawajuwi, mimi ninaamini kuwa mwanamziki ni razima ajue kupiga ala yeyote ya muziki.
  Lakini vija wa leo kila unayemuona anadai “MIMI MSANII” wanaiga muziki wa kigeni wangekuwa na uelewa mzuri wangeungana wangefuata nyayo za Mubaraka wapige muziki wa kitanzania halisi.

 34. Nani zaidi kati ya Mbaraka Mwishehe, Hemed Maneti na Marijani Rajabu?, 01 June, 2013

  […] kumtangaza Mkuu picha zao mbona zipo sana, fuata hiyo link na Video moja ya Marijani Rajabu. http://www.bongocelebrity.com/2007/0…uka-mwinshehe/ KAMANDA WA MATUKIO Raia Fulani likes this. Open your eyes, look within. Are you satisfied […]

 35. Dennis Frederick Galinoma, 12 November, 2015

  Kulingana wachangiaji waliopita, najifariji sana kwani mimi nilipata kumuona marehemu Mbaraka Mwinshehe kwani miaka yake ya mwisho nilikuwa shule ya sekondari hapa dar, mimi nilimshuhudia akiwa stejini, mnazi mmoja katika mashindano ya kutafuta bendi bora ili ikatuwakilishe huko Nigeria, kulikuwa na bendi nyingi sana lakini Mbaraka Mwinshehe na bendi yake alikuwa wa pili na Marehemu Patrick Balisidya na bendi yake ya Afro 70 akashinda na wakatuwakilisha huko Nigeria na bendi iliporudi kutoka Nigeria haikudumu sana na ikatoweka, Hii ilikuwa miaka ya sabini, lakini, nikiwa mdogo huko mwanza miaka ya 69, 70 hivi Mbaraka alitembelea na kupiga kambi Mwanza kwa muda mrefu sana na alikuwa akipiga dansi ktk ukumbi wa olofea karibu na makazi tuliokuwa tukiishi. ilikiuwa rahisi kutoroka na kwenda kuchungulia huyu bwana akipiga gitaa lake, miaka hiyo walioko nje walikuwa wengi kuliko walioko ukumbini, nakumbuka gari lao land rover lilikuwa na maandishi makubwa yaliyo ndio mtindo wa bendi hiyo “MAHOKA”
  Sidhani kama tutapata watu wa aina hii ki mziki, mbaraka mwinshehe, shem kalenga,patrick balisidya, david mussa, marijani rajabu,juma kilaza,muhidini ngurumo, bichuka rehani,juma mrisho, john kijiko,maneti,mwanjerwa, salum abdala, henry mkanyia na wengine wengi.

Copyright © Bongo Celebrity