Mashindano ya kumtafuta mrembo wa Tanzania maarufu kama Miss Tanzania kwa mwaka huu wa 2007 yanatarajiwa kufanyika jijini Dar-es-salaam tarehe Mosi mwezi wa Septemba katika viwanja vya Leaders Club-Kinondoni. Kwa maana hiyo tofauti na miaka ya nyuma au ilivyozoeleka, mwaka huu hayatafanyikia katika ukumbi wa Diamond Jubileee.

Pichani washiriki wa shindano la mwaka huu,wakiwa wamepozi na gari ambalo mshindi wa mwaka huu atazawadiwa pamoja na zawadi zinginezo.Mdhamini mkuu wa mashindano ya mwaka huu ni kampuni ya simu za viganjani Vodacom.

Mmoja ya washiriki wa mashindano ya mwaka huu ni Richa Adhia kutoka Kinondoni jijini Dar-es-salaam. Kutokana na yeye kuwa ni mtanzania mwenye asili ya bara la Asia (nchini India), tulipofanya naye mahojiano takribani mwezi mzima uliopita ilionekana wazi kwamba watu wengi watakuwa wanasubiri matokeo ya mashindano haya mwaka huu sio tu kuona kama Richa Adhia anaweza kuibuka mshindi au mmojawapo wa washindi bali pia kutokana na msisimko wa mashindano ya mwaka huu tangia yalipoanza kwenye ngazi ya vitongoji. Je nani ataibuka mshindi kwa mwaka huu wa 2007? Jibu tutalipata Septemba Mosi.

Kama ulipitwa na mahojiano yetu na Miss Kinondoni na maoni ya waliochangia unaweza kuyapata kwa kubonyeza hapa.

Feedback / Comments

6 Responses to “MISS TANZANIA 2007”

  1. Comment by Neema on August 23rd, 2007 11:07 pm

    Good luck to all of you, atakaeshinda jaribu sana kuitangaza Tanzania, na ni vizuri zaidi mkifika kwenye jukwaa kuomba mkalimani wa lugha ya kiswahili ili tutangaze lugha yetu. Si mnaona wachina wenzetu wakifika pale wanaomba mkalimani, sio kwamba hawajui English, wanataka tu kuboresha lugha na utamaduni wao, tujaribuni basi na sisi.

  2. Comment by jeff on August 28th, 2007 6:06 am

    need to know about positive and negative impact of miss Tanzania from 1994 to now.

  3. Comment by TINA on August 30th, 2007 6:24 am

    Atakae shida ajaribu kutake care asiwe kama wema sepetu heshimu nchi yako nawatu wote.

  4. Comment by miss pauline joseph on September 5th, 2007 3:42 am

    jamani mjitahidi msiwe kama wema sepetu kwa mie sijui mtoto yule walimwokota wapi,si vyote ving’aavyo ni dhahabu jamani ndugu zangu

  5. Comment by stambuli on September 6th, 2007 1:45 am

    Mnashangaa nini bwa.Misosi kaimba nitoke vipi?kila mtu anatafuta namna ya Kutoka naye akasepetuke ulaiyani,mapredishee mate yanawatoka hapo wanataka kubadili spare mpya.

    By Stambuli(Jam Stam)

  6. Comment by mwajuma ramadhani on September 10th, 2007 5:26 am

    tunatakiwa kudumishalugha yetu pia nampongeza miss aliyechanguliwa asiwe wema sepetu pia nidhamu inatakiwa.

Leave a Reply