Kunako miaka ya 80 na mwanzoni mwa miaka ya 90, majina ya Ma-DJ yalikuwa makubwa kama ilivyo kwa wanamuziki wa kizazi kipya na cha zamani hivi sasa. Mojawapo ya majina hayo ni DJ Seydou(pichani). Yeye na DJ mwenzake aliyekuwa anajulikana kama DJ Yaphet Kotto walitamba sana na disco lao la RSVP Discotheque pale Mbowe (siku hizi Club Billicanas). Enzi hizo vijana walikuwa waende wanakokwenda usiku unakuwa haujakamilika kama hawatofika Mbowe kupata ladha kutoka kwa DJ Seydou na mwenzake.Jina lake halisi ni Saidi Mkandara.
Tofauti na Ma-DJ wenzake wa enzi hizo, yeye alikuwa sio muongeaji sana. Badala yake yeye alisifika sana kwa uwezo wake wa kupangilia miziki. Akianza vitu vyake alikuwa hakai mtu kitini mwanzo hadi mwisho. Uwezo wake wa kusoma ukumbi na kujua aweke muziki gani ulikuwa unawastaajabisha wengi.
Isitoshe DJ Seydou alikuwa akisifika kwa kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote mwingine enzi hizo. Kila jumamosi alikuwa hakosi kuibua kibao ama vibao vipya kutoka kona mbalimbali za dunia.
Hivi sasa DJ Seydou ni mshauri wa muziki wa sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Club Ambience ya Sinza na Sanaa Pub. Hazina ya muziki wa zamani na wa sasa aliyonayo haina mfano. Uliwahi kuhudhuria disco la DJ Seydou? Tupe kumbukumbu zako kwenye sehemu ya comments.

Pichani DJ Seydou akiwapa vijana historia ya burudani nchini Tanzania tangu enzi hizo mpaka sasa. Hiyo ilikuwa hivi karibuni wakati wa matukio ya WAPI pale British Council jijini Dar-es-salaam.
Baadhi ya miziki ambayo Seydou alikuwa akiipiga enzi hizo ni kama huu hapa uitwao Get Down on It wa Kool and The Gang. Asante msomaji wetu Daniel kwa kutukumbusha tune ya wimbo huu. Pia unaweza sikiliza vibao Midas Touch kutoka kwa Midnight Stars, Don’t StopTill you Get Enough kutoka kwa Michael Jackson, A Night To Remember kutoka kwa Shalamar, Kleer- Intimate Connection…
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Picha zote kwa niaba ya Bob Sankofa. Kwa picha zaidi za matukio ya WAPI unaweza kutembelea blog ya Bob Sankofa http://mwenyemacho.wordpress.com
Page 1 of 3 | Next page