MISS TANZANIA 2007 NI RICHA ADHIA

Richa Adhia (pichani) binti wa miaka 19 tu anayeishi Kariakoo jijini Dar-es-salaam ndiye MISS TANZANIA 2007. Ameibuka mshindi katika mashindano ya Miss Tanzania yaliyofanyikia usiku wa jana katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar-es-salaam. Aliyeibuka mshindi wa pili ni Lilian Abel kutokea Kinondoni na wa tatu ni Queen David kutokea Temeke. Mmojawapo wa majaji wa mwaka huu alikuwa ni mnigeria Agbani Darego, mrembo wa dunia wa mwaka 2001.

Tulipomhoji mwezi mmoja uliopita mara tu aliposhinda taji la Miss Kinondoni, Richa Adhia alitueleza mengi ikiwemo ndoto yake ya kushinda taji la Miss Tanzania na nini anatarajia kulifanyia taifa la Tanzania endapo atashinda. Sio vibaya kama tutajikumbusha tena mahojiano hayo. Mahojiano kamili unaweza kuyasoma tena kwa kubonyeza hapa.

Mashindano ya Miss World mwaka huu yanatarajiwa kufanyikia huko Sanya nchini China ndani ya ukumbi maarufu wa Crown Beauty Theater tarehe mosi(1)Decemba. Washiriki wanatarajiwa kuwa wameshawasili nchini China ifikapo tarehe 2 Novemba.Picha zaidi na matokeo…

TOP THREE: Kutoka kushoto ni Queen David (Temeke), Richa Adhia (Kinondoni) na Lilian Abel (Kinondoni)

TOP FIVE: Kutoka kulia ni Richa Adhia, Victoria Martin, Lilian Abel, Hadija Sulla, Queen David.

TOP TEN: Bila mpangilio maalumuLilian Abel, Gladness Katega, Richa Adhia, Cecilia Charles, Latifa Warioba, Queen David, Neema Khatibu, Victoria Martin na Hadija Sulla.

Picha zote kwa niaba ya Michuzi.

 1. A.E. i o u, 06 November, 2007

  Adhia is my fellow Tanzanian like any other who is a Tanzanian. She is our flag carrier and let us encourage her to represent us all well. She was born in Tanzania from Tanzanian parents.Mom from the Isles while Dad is from Morogoro. What else do you want from her? For your info, there are more than 120 ethnic groups in Tanzania. We are a heterogeneous population, living peacefully without racial superiority or inferiority. SISI NI NDUGU TUNAONUIA MAMOJA.Ewe Mtanzania; Acha kabisa sumu ya ubaguzi, weeeeeeeee eeeeeeeee!!!!!!!! TAKE CARE MADAM ADHIA AND RAISE HIGH TANZANIAN FLAG.

 2. ramsees3, 18 February, 2008

  mimi ni mwarabu wa omani lakini moyo wangu na roho yangu ni Tanzania . Tanzania ndio ilio nizaa, rangi yangu ni nyeupe lakini hamna siku moja nilisahau kuwa mimi ni mtazania .Na kumbuka baba na mwalimu wetu marahemu mzee nyerere alipo nichukua kono mikono yake mwaka 74 alipokuja ziara Mpanda akisema mwanangu nilikuwa na miaka 10. nenda mbele dada richa watanzania wote kwako na mimi kwako.

 3. mbaguzi, 20 March, 2008

  hzehehehehe hawa wadosi au waarabu mhhh si wabongo tu hawa hiki ni kizazi ambocho kimezaliwa hapa kwahio ni wabongo sio swala la kuongea au kudiskasi bagua linalo baguliwa sio hili jamaaa mie najua kubagua siol hili eeeh oa mdosi zaa watoto wawe miss tz nao ileile tu mbona washamba nyie hamjaona timu ya socer ya ufaransa utasema ghana ile toeni ugoko wenu kichwani

 4. Egide, 16 March, 2009

  hello everyone;
  that issue really costs a shame to all east africans; but then i would like to know what followed last( 2007-2009)? how did you stop that problem? is Richa still participating in modeling these days? and can some one tell me how she managed to stand in that situation?
  hope she made it!
  (from Rwanda.)

 5. Juma, 04 August, 2010

  Sasa Raisi wa Marekani si mweusi??

Copyright © Bongo Celebrity