Aina ya muziki ijulikanayo hivi leo kama Bongo Flava au muziki wa kizazi kipya umetoka mbali. Hii leo tunao vijana lukuki ambao kutokana na muziki huu, majina yao yanafahamika kila kona na hivyo tunawaita celebrities kutokana na kukubalika kwa kazi zao za muziki.
Lakini wangapi tunakumbuka walipotokea? Na je wao wenyewe wanakumbuka walipotokea? Bado wana muelekeo au mtazamo waliokuwa nao enzi hizo? Tizama video hizi tatu kutoka katika documentary iliyoitwa Hali Halisi-Rap As Alternative Medium in Tanzania miaka hiyo. Documentary ilitengenezwa na Madunia Foundation. Unaweza pia kusoma historia kidogo kuhusu muziki huu wa kizazi nchini Tanzania kwa kubonyeza hapa. Kwa mnaoijua zaidi historia muziki huu wa Bongo Flava tunakaribisha michango yenu.
Feedback / Comments
2 Responses to “ILIKOTOKA BONGO FLAVA!”
Leave a Reply


sending...
eee bwana eee..hizi video ni kali kupita mfano.watu wametoka mbali kumbe!
awali ma mc’s walikua wana rap kwa kutumia kikoloni,wapenzi(vijana) wengi wakawa hawapati ujumbe,hivyo wakaitaji sana radha ya kiswahili,na kuwaomba wana rap wawapigie radha ya tanzania(Bongo) hivyo ndo mwanzo wa kuibuka neno bongo flavor, sijaona ambapo imeelezwa hili.zaidi ya hili nimepanda kuona mc’s wa zamani, na harakati zao.