Habari za kusikitisha zilizotufikia ni kwamba gwiji la sanaa za maonyesho nchini Tanzania Mzee Godwin Zilaoneka Kaduma hatunaye tena duniani.Habari hizo zinazidi kupasha kwamba mauti imemfika Mzee Kaduma katika hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa ajili ya matibabu zaidi.Alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kupooza(stroke).

Msiba upo nyumbani kwake Bagamoyo jirani na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Heshima za mwisho kwa walio Dar-es-salaam zitatolewa kesho (Ijumaa) saa nne asubuhi habari zaidi zinasema heshima za mwisho kwa marehemu mzee Kaduma kwa walio Dar es salaam zitatolewa kesho saa nne asubuhi hospitali ya Muhimbili kabla mwili wake kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Bagamoyo na kisha baada ya kuagwa saa nane mchana utapelekwa kijijini kwake Itamba, Iringa, kwa mazishi.

Marehemu Kaduma enzi za uhai wake pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa la Lugha ambayo kwa sasa imebadilishwa na kuwa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ambapo baada ya kustaafu nafasi yake ilichukuwa na Dr. Daniel Ndagala.

Baada ya kustaafu serikalini marehemu Kaduma aliendelea na shughuli za sanaa akiwa kama kiongozi na mtendaji katika sanaa za maonesho zikiwemo ngoma na maigizo. Alikuwa mwanzilishi wa Kituo cha Sanaa za Maonyesho Tanzania (TzTC) na Taasisi ya Sanaa za Maonyesho Mashariki mwa Afrika (EATI) ambapo pia alikuwa Katibu Mtendaji wa kwanza wa asasi hizo.

Aliamua kupumzika kuzitumia asasi hizo mwaka 2003, ambapo aliendelea na shughuli zale za kawaida za kufundisha masuala ya sanaa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo akiwa kama mkufunzi mualikwa katika Idara ya Tamthiliya ambapo alikuwa akifundisha somo la uandishi wa michezo ya kuigiza kazi aliyokuwa anaendelea kuifanya mpaka mauti ilipomfika.

Kwa mara ya mwisho, marehemu Kaduma alifanya onyesho akiwa msanii wa kujitegemea mwezi Juni mwaka huu, wakati wa semina maalum ya kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, iliyoandaliwa na Mfuko wa Utamaduni Tanzania ambapo alitamba shairi lililoitwa Naililia Tanzania. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Picha kwa hisani ya Chemi Che Mponda ambaye mapema mwaka huu alipata fursa ya kuongea mengi na marehemu Mzee Kaduma.

Feedback / Comments

3 Responses to “MZEE GODWIN KADUMA HATUNAYE TENA.”

  1. Comment by Dinah on September 27th, 2007 12:49 pm

    Mungu awajaalie uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu.

    Mungu alitoa na ametwaa. Jina lake litukuze. Amina.

  2. Comment by Mija Sayi on September 28th, 2007 4:13 pm

    Bado siamini kama ametutoka. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amina.

  3. Comment by Johan Soderberg on November 24th, 2007 9:46 pm

    It was these sad news that made me find your website…

    It most certainly wasn´t “what I like to know” but thank you for posting it.
    And thank you for sharing the news with respect for Mzee Kaduma.

    Greeting from Sweden.

Leave a Reply