
Ukiwa jijini Dar-es-salaam na kwingineko popote inaposikika Clouds FM (88.4) nchini Tanzania na ukafungulia redio yako kuanzia saa 12 mpaka saa 3 asubuhi, watangazaji Ali Masoud maarufu kama Masoud Kipanya (pichani aliyesimama) na Fina Mango (aliyeketi) watakusaidia kuianza siku yako vyema kwa habari mbalimbali zinazoambatana na burudani. Kipindi chao kinaitwa Power Breakfast.
Masoud Kipanya pia ni mbunifu wa mitindo (fashion designer) na mchora katuni matata sana. Katuni yake ya Kipanya inapatikana ndani ya gazeti la Mwananchi na pia kwenye tovuti yake. Masoud alikuwa ni mmojawapo wa watu maarufu nchini Tanzania (bongo celebrities) tuliofanya nao mahojiano mwanzo mwanzo blog hii ilipoanzishwa. Mahojiano hayo bado yanapatikana hapa mtandaoni. Unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.
Feedback / Comments
23 Responses to “KIPANYA NA FINA MANGO”
Leave a Reply


sending...
Kwa kifupi hawa jamaa huwa wananifanya niamke mapema kila siku lakini nachelewa kazini kila siku, nikifika kazini sishuki kwenye gari hadi baada ya nusu saa hivi. Huwa sikikosi kipindi chao aisee. Jamaa ni zaidi ya watangazaji, they are very funny (Nimetia kizungu hapo
Kipindi chao ni cha kisayansi sana. Unajua muda wa kile kipindi ni makini sana maana huwa ndio tunakwenda makazini na foleni huwa ni bab’kubwa lakini hawa jamaa huwa wanatusaidia tusiione kabisa ile foleni. Huwa naangalia madereva wa magari mengine asubuhi zile, kila mtu huwa anatabasamu. Jamaa matata sana hawa.
BC mmesahau kusema kuwa Kipanya pia ni mbunifu wa mitindo, ana lebo yake inaitwa KP. Matata sana ile lebo nayo.
Fina (Chief Justice), endeleza libenenge mama. Kipanya you are just off the hook my brother. Kuna yule mshikaji wenu mwingine mnatangaza naye, jamaa naye funiko la kufa mtu namfananisha na Richard Quest wa CNN hasa akiwa anafatilia habari za nje ya studio live.
PAMOJA!
mhhh hiyo poz yao mbona ina utata?
ni mapatner kikazi au boy friend na girl friend?
haahaahaaa!!!!!
Yaani hawa jamaa ni funika bovu hakuna wakuwakamata hawa watu ni balaa si kitoto wanaaaaaaaaaaaaa!
BC kazi bomba kinomaaaaaaaaaaa
baba malcon vipi mama malcon hajambo? A.K.A Matha
Hongera sana timu zima ya “Kifungua kinywa cha nguvu” sijui kama nitakuwa nimeleta vema kwenye lugha ya kibantu kutoka kwenye lugha ya malkia.
Ama hakika kati ya kitu ambacho huku ughaibuni ukiniuliza na nakikumbuka na kukikosa bongo basi ni kipindi chao hawa waheshimiwa.
Ingawa naona hapo kakosekana rafiki yangu Gerald Hando,natumaini bado yupo Mawingu FM.
Ila BC,naona labda mimi ndio nimechemka au nyie,maana nilitegemea kupata mahojiano ya Fina pia ila naona ya Masoud Kipanya tu.
Naamini hatujachelewa utatuletea mahojiano ya huo ndugu yangu wa KUNYUMBA(songea).
Na kati ya swali ambalo naomba umuulize vipi anaendeleaje na sanaa ya muziki.Maana nakumbuka alikarabati wimbo wa “SHOGA2 pia alitoa kitu kingine “twende kunyumba”(sina uhakika na jina la wimbo)
Na kama bado anaendelea na album yake na nyimbo zake tutasikiliza wapi?Au BC mtusaidie mtuwekee japo wimbo wake mmoja usindikize mahojiano yake.
Kila la kheri mnafanya kazi nzuri BC.Pia na kila la kheri Kipanya,Fina MAEMBE(nafikiri rafiki yangu Fina huwezi jali maana najitahidi kuepuka kutumia lugha ya malkia)
Wasalaaam
NDAKI
Baab kubwa lkn mbona huyu fina kama amebadilika au mi cmjui?!maana mi siku zote nikisikia jina lako huwa najua mtoto 1 mkali sana lkn mbona anachekesha?hahaha just jokin kazi yenu naikubali sana.
BC hivi clouds fm 88.4 inapatikana kwenye Internet? Tulio mbali tunakosa huo huondo…kama kuna anayejuwa naomba anijulishe! Picha imewapendeza sana.
Big up saana, sio siri mnadatisha na kuibua hisia zilizolala….i luv u guys!!!
Hongereni sana KP na Fina, bila kumsahau Gerald.
Mnachonifurahisha, kati yenu hakuna hata mmoja mwenye cheti cha ngazi ya chini kabisa cha Uhandishi wa Habari. Lakini mnafanya mambo makubwa kuliko Waandishi Habari “Waandamizi” (with Masters !). Kwa mfano, Masoud na Fina ndiyo Waandishi wa kwanza kabisa kupewa guided tour ndani ya Bunge wakiongozwa na Mh. Spika Sitta- na ilirushwa live.
Hii inathibitisha kuwa Elimu siyo Vyeti bali……..
Nina wasiwasi kama radio nyingine huwa zinapata wasikilizaji mida wanapokuwa hewani….
Kazeni buti zaidi, na Papa Joe (Joseph Kusaga), please wacheki take home yao iwe zaidi ya kima kilichotangazwa majuzi.
Iddi Njema.
hivi hii radio ya clouds fm inapatikana katika internate? naungana na mdau hapo juu…kama kweli hao jamaa wanafanya mavituzi basi angalau tuwasikie live katika internate …mimi niko huku japan…..
BC hujanipa jibu, bado nahulizia hao clouds 88.4 fm wanapatikana kwenye tovuti kama redio zingine? naomba tovuti yao ili nasi tusikie hiyo power breakfast sisi tulio mbali!!! jamani ujanja wote huo tunazidiwa na kameme fm redio ya wakikuyu ipo kwenye tovuti!!!
Sinzia,
Tunavyojua sisi ni kwamba Clouds FM haisikiki mtandaoni bado.Mpaka hivi sasa radio pekee inayorusha matangazo yake kutokea nchini Tanzania na kupatikana mtandaoni ni Radio Maria(ya kanisa katoliki).Wao wanapatikana kupitia http://www.radiomariatanzania.co.tz.
kazi nzuri kipanya keep it up and dada fina
KIPANYA NAKUFAGILIA……………FINA HILO DOMO KULIFANYA HIVYO MANAKE NINI!!!!!!!!!!
Fina na Masoud mkoo juu sana i love uuuuuuuuuu.
Aah kwakweli you guys rock! Yani imenibidi ninunue simu yenye radio ili niweze kuwasikiliza hadi niwapo kazini. Hongereni, kwakweli mna vipaji sio siri. Nawapenda!
asanteni sana kwa kuzungumza yale ambayo mmeona yana ukweli,watanzania wengi wanakuwaga wagumu sana kusifia pale kwenye ukweli,maoni mengi yametupa morale ya kufanya vizuri zaidi..2008 tutafanya bidii na kuboresha zaidi asanteni sana
KP na Fina Mango ni funika mbaya, kwa watazamaji wa CNN nawafananisha na T.J na Betty Nguen . keep it up Masoud and Fina
Nathan
jamani fina yani tangu uniteme kipindi kile twasoma wote shule ya sec SHAABAN ROBERT ndio hata kunitumia msg za kuni julia hali hutaki sawa bwana ! jus jokin ya never mind , i like u gayz best of lucky
He Fina na Masoud mko wapi,i missed alot, naamin mko poa angalau masoud namuona maisha plus jaman Fina nakupenda sana kwangu u mrembo
wangu Fina upo wapi,yaani nimekumisi ile mbaya ,wewe kwangu ni zaidi ya wote ,upo juu sana,mapozi,sex body,macho , big up
naitaji kujua kuhusu masudi na fina wapo wapi kwa sasa na kama wapo kwenye stisheni ipi bira kumsahau kaka bonda basi maguludum>dr seba mzee ya njia panda? hogeleni sana kutimiza miaka kumi tunasubili tv mwanza.umbi kwa mb kusaga unafamilia imala sana katika radio
naitaji kujua kuhusu masudi na fina wapo wapi kwa sasa na kama wapo kwenye stisheni ipi bira kumsahau kaka bonda basi maguludum>dr seba mzee ya njia panda? hogeleni sana kutimiza miaka kumi tunasubili tv mwanza.umbi kwa mb kusaga unafamilia imala sana katika radio naitaji kuoa katika familii hiyu.vp mlimtoa jackakilini kombe maana sauti yake kama marehem amina chifupa