SHEIKH YAHYA HUSSEIN.

 

 

 

 

Iwe ni uchaguzi, mechi kubwa ya mpira au chochote kile chenye mvuto au gumzo la kitaifa, Sheikh Yahya Hussein (pichani) atakifanyia utabiri bila kusita. Kitu chochote kikitokea pia iwe ni ajali mbaya, mafuriko nk, Sheikh Yahya atakitolea maelezo pia akiweka sababu za kutokea kwa kitu au tukio hilo. Hivi leo anabakia kuwa mnajimu au mtabiri maarufu kupita wote nchini Tanzania. Amekuwa akifanya hivyo kwa miaka chungu mbovu mpaka hivi sasa.

Alizaliwa mwaka 1932 huko Bagamoyo kwa wazazi wakimanyema. Alipata elimu yake ya awali katika shule ya Al-Hassanain Muslim School jijini Dar-es-salaam. Baada ya hapo alikwenda visiwani Zanzibar alipojiunga na chuo kilichojulikana kama Muslim Academy kilichokuwa chini ya Sheikh Abdallah Swaleh Al-Farsy aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar wakati huo. Baada ya kuhitimu alielekea nchini Misri alipoendelea kusomea masuala ya dini katika chuo kikuu cha Al-Azhar kilichopo Cairo.

Alirejea nchini mnamo miaka ya mwanzoni ya 60 ambapo alianza kazi yake ya utabiri . Sheikh Yahya Hussein ndiye mtabiri wa mwanzo kueneza utabiri wa kila siku katika magazeti mbalimbali ya Afrika Mashariki enzi hizo. Jina lake lilivuma zaidi alipokuwa akitoa utabiri kupitia radio kuhusu mashindano ya mpira kati ya nchi tatu za Africa Mashariki yaliyojulikana kwa jina la Challenge Cup au Gossage Cup.

 1. kyng, 03 June, 2011

  leave him alone 2 rest where he is supposed 2. The first ppl 2 c Jesus were astrologers and if its a matter of spirits christians also swear in the name of the father the son and the holy spirit. nw what is a spirit? ghost of dead man so ur also wrong

 2. Abdi, 03 September, 2011

  Usifikie mahali ukaongea sana ukamkufuru mwenyezimungu,sikuzote imani hutoka moyoni mwa mtu,hulazimishwi kuamini amini unacho kiona kinafaa kuaminiwa na mwisho wa siku uta jua ulichokuwa unakifanya wala hautalaumiwa na mtu
  hivi kumwita huyo mzee mchawi huoni kama unakosa adabu?,…haaa!wewe!je kama ange kuwa ni baba yako hapo ungethubutu kusema?kwani lazima usikilize anacho kisema?
  Mimi huwa siamini vitu kama hivyo ila naamini mungu mmoja tu aliye hai basi!na kama hauna dini basi jiamini mwenyewe tu..

 3. Namatovu Halimah- UGANDA, 05 September, 2011

  Sheikh we want to see you in Uganda also

 4. Hashim Said, 06 September, 2011

  Hello Halimah! Sheikh Yahya is not with us again in this world!

 5. zahyr, 09 December, 2011

  plz leave my papa 2 rest where he deserves! ur not God nor Angels so msimuhukumu mtu while ww ur worse thn him na 4 ur info sheikh yahya hakuwa mchawi alikuwa mnajimu kipaji adimu duniani nakusema kutabiri ni guess work thats crazy just try 2 do that n we will c may Allh bless him wherever he is Amen

 6. Karenga, 28 December, 2011

  YOU ZAHRY ,YOU ARE RIGHT THESE CHAPS SHOULD LEAVE MY GRAND PA ALONE LET HIM REST IN PEACE,AND THE REST IS NON OF YOUR GODAMNED BUSSINESS,SO ALL BACK OFF AND TRY TO MOVE ON WITH YA DAILY LIVING.KARENGA SEOUL.

 7. hassan, 02 March, 2012

  yaan huyu shekhe kwanza sio shekhe kwani ni muongo kabisa akuna mtu ambaye anaye weza kutafsiri kuhusu siku ya kesho itakuaje kwan itakua ni moja ya kumshirikisha ALLAH ushauri wangu kwa waislamu wenzangu tuache kuamini hivi vitu jamani kwan ni dhambi kubwa sana na mungu ata waingiza motoni9 watu wa aina hiyo
  wab lahi toufiq

 8. ipty, 21 April, 2012

  tumuamini mungu tu tusiamini sheikh yahya

 9. salum, 30 June, 2012

  Ukweli unauma babu yenu yahaya husein jirani yake sasa no firauni hukooooooooooooooooooooo motoni. ushahidi 5/90 quran. au na nyie hamuamini kama babu yenu?

 10. salum, 30 June, 2012

  Hata michuzi anajua huyu mzee hakua sheikh ndio maana kamuweka kwenye bongo celebrity pamoja na remmy ongala na wote hapo juu. hahaa uislam hauna celebrity kama mzee yahaya husein.

 11. samuel, 07 March, 2013

  hello,kindly i need the contacts for Dr.Suleiman Mazinge ambaye anajua mengi kuhusu Illuminati and Free Masons,we are planning to save both the Muslim and Christians from the devil and we need special platforms to be aired on the TV in both talk shows and programs,this will take place in different TV media agencies under both religious sponsorships.kindly send me his contacts,Inshallar.

 12. samuel, 07 March, 2013

  from my previous request, my contacts are 0704 761 598,thank you.

 13. bongocelebrity, 07 March, 2013

  Unfortunately, we don’t have his contacts.

Copyright © Bongo Celebrity