57!

Jumapili iliyopita Raisi Jakaya Mrisho Kikwete alisheherekea miaka 57 ya kuzaliwa.Alizaliwa tarehe 7 Oktoba 1950 katika katika kijiji cha Msoga kilichopo wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani katika iliyokuwa inaitwa Tanganyika. Alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Msoga kati ya mwaka 1958 na 1961.Baada ya hapo alihamia shule ya kati(middle school) Lugoba kati ya mwaka 1962 mpaka 1965. Baada ya hapo akajiunga na shule ya sekondari Kibaha kwa ajili ya O’level.Hiyo ilikuwa ni kati ya mwaka 1966 mpaka 1969. Baada ya hapo akaelekea shule ya sekondari Tanga kwa ajili ya A’Level. Mwaka 1972 mpaka 1975 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam akisomea Uchumi.

 

Pichani Raisi Jakaya Mrisho Kikwete, akikata keki kusheherekea hiyo siku yake ya kuzaliwa katika hafla iliyofanyikia kwenye makazi yake,Ikulu jijini Dar-es-salam. Kutoka Kushoto ni watoto wa raisi Ridhwan, Rashid Chodo,Mohamed (mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu ambaye ni yatima anayelelewa na raisi nyumbani kwake), Lulu na Khalfan Kikwete.

Picha kwa hisani ya Yahya Charahani.

Feedback / Comments

25 Responses to “57!”

  1. Comment by Kenny on October 12th, 2007 1:41 pm

    Duh vizuri Kikwete anaonekana yuko happy, by the way keki mbona inaonekana kama wamefanya watoto, au walitaka iwe too personal, and children walikuwa more involved katika kutengeneza keki? kwani watengeneza keki wengi Dar wangependa kupewa hiyo deal… ingekuwa powa.. Ooh na kama hiyo keki ilikuwa imetengezwa na proffesional inabidi wasimtumie tena huyo mtu, keki imekaa kama “pie”!!!

  2. Comment by mesa on October 12th, 2007 2:32 pm

    asante mr p sasa wife yoko wapi na salama je?

  3. Comment by Dinah on October 12th, 2007 3:01 pm

    Happy 57,
    Yaani Rais kazaliwa siku ya “Eid”? (joke) kumbe bado yanki! Watoto wake wananikumbusha wa Mwl Nyerere wanaonekana “humble” (kwa mujibu wa picha)hiyo njemba yenye Polo T-shirt wala huitaji DNA.

  4. Comment by TanzanianDream on October 13th, 2007 7:03 am

    Rais wetu bwana Bongo Fleva mno….Ebana Rais ni 57 yrs old n’ yet watu wanamuita kijana i doubt kama mi sio mtoto mchanga maana wabongo bwana mnapenda mno kusifia vitu ujinga…..

  5. Comment by NDAKI GOMBERA on October 13th, 2007 7:05 am

    Naomba kuuliza!

    Nasikia mheshimiwa ana bifu na my wife wake ndio maana hata kwenye BESIDAY hiyo kaamua kumpiga chini asitokee?

    Ila angemsamehe waweke mambo sawa.

  6. Comment by Dinah on October 13th, 2007 7:47 am

    TanzanianaDream, mimi nafikiri uzee ni muonekano sio namba. Alafu Bongo watu wanapenda sana kupunguza namba lakini sura zao zinaonyesha kuwa ni wazee sasa huenda Kikwete kaongeza :-)

  7. Comment by Moses Jakanyangoe on October 13th, 2007 11:39 am

    Sikumbuki naomba mnikumbushe, sijui mheshimiwa ana watoto wangapi vile?

  8. Comment by Ally on October 13th, 2007 2:10 pm

    Hongera prezoo!nimefurahishwa kusikia unalea mtoto yatima mungu akujaalie uwe na moyo huo!lkn isije kuwa anatoka Bagamoyo!!!!!

  9. Comment by Chiki on October 15th, 2007 1:15 am

    We Kenny wa kwanza hapo Juu acha ujinga, kwani keki ya nyumbani na ya watengeneza keki maarufu inatofauti gani? usimpangie mtu ale nini bwana, yeye mr.jk kaona hiyo ndo nzuri na simpo ya kumfaa, sasa wewe ulitaka itengenezwe ya shepu ya ngamia au ya ngazi 20? Mijitu mingine bwana inaboa sana!!Mbona keki yenyewe nzuri tu kuliko hizo unazosemea wewe? Nina uhakika keki ingekuwa ya dizaini fulani ungesema jk anatumia pesa kutengeneza keki, so alijua thats why aliifanya simple. Watanzania hatuna jema kwetu kila kitu lawama na kasoro!! Tubadilike jamani!!

  10. Comment by XX on October 15th, 2007 11:56 am

    Ridhwani lookz younger..i mean mashavu yameisha sasa ni copyright na baba yake.they look wonderful…kama ka reunion flani ila kwanini mai waifu wake hakuwepo jamani??alafu vipi vinywaji mbona keki peke yake??Anyways happy bday prezzo wetu u stil young n u look fresher than 57.

  11. Comment by Kenny on October 15th, 2007 2:19 pm

    Chiki, soma vizuri hiyo comment kabla hujasema nimeipondea keki.Nimesema imetengenezwa nyumbani, Sikusema itengenezwe gorofa, halafu keki gani ita costi too much tuseme ameibia serikali?? kama wizi upo tuu…

  12. Comment by TanzanianDream on October 16th, 2007 3:04 am

    Chiki inabidi uanze kubadilika wewe ambae unasoma comments za wenzako halafu huelewi ndo Tanzania kupitia watz walio kama wewe watabadilika kwa ujumla….

    Eti tubadilike?? au ubadilike?

  13. Comment by Colin on October 17th, 2007 2:26 am

    Nafikiria kuwa wife wake anaweza akawa upande mwingine,Coz ukicheki watoto ni kama walikuwa wanamuangalia mtu mwingine muhimu.Anyway cheers prez japokuwa tulifanya mistake kukupigia kura.

  14. Comment by keiko on October 17th, 2007 7:48 am

    this happens only in tanzania, kijana kuwa na miaka 57 :d

  15. Comment by Janet on October 17th, 2007 11:08 am

    Hi,
    Happe belated prezdoo!
    Nimesikitika kuona mtu ana comment kuwa keki ya nyumbani ni mbaya. Mimi mume wangu anapenda sana nimpikie keki mwenyewe ajali ionekana nzuri au vipi?Ananopenda kwanza kuwa keki imepikwa nyumbani na siyo ya mabox and pile ni mke wake kaapika. Si ninaamini Kikwete naye anapenda hiyo keki ipikwe na wanawe or mke wake na iwe ya nyumbani. We uliyecomment bado hujapata familia nini?

  16. Comment by LINDA BEZUIDENHOUT on October 17th, 2007 11:49 pm

    HAPPY BIRTHDAY MR PRESIDENT.

  17. Comment by speed on October 18th, 2007 3:47 am

    mi nafikiri swala la umri wanamuita kijana ukimcompare na marais wa nyuma,kidogo wao waliingia madarakani wakiwa na umri wa juu zaidi yake na kingine walichoona mr JK anaonekana yuko active sana, yaani kama mtu wa mazoezi fulani kiasi kwamba twamdhania ni kijana…

    mashavu ya rashid na khalfani yanafanana sana na huyo mtoto yatima…au twazibwa mdomo tusitie neno (joke)

    na swala la kupunguza umri kwa wabongo ni kitu cha kawaida ila naona mheshimiwa kaja tofauti inawezekana kweli kabisa unayosema Dinnah kwamba mzee karefusha umri…

  18. Comment by gina on November 13th, 2007 8:50 pm

    hongera, all the best kuongoza tanzania. Tusisahau tulikotoka kwani, hatujui ya mbele. amani idumu tanzania.

  19. Comment by gina on November 13th, 2007 8:53 pm

    Amani na utulivu, uendelee tanzania, kwa kila raia. Watanzania wote wana haki sawa popote pale.

  20. Comment by gina on November 13th, 2007 8:58 pm

    Tanzania is a peaceful country, tunaomba mwaka uishe salama, bila vurugu.

  21. Comment by kare on November 14th, 2007 12:09 am

    sherehe, kukumbukana ni vizuri, wakati wa shida na raha, kwani, hujui nani utamuhitaji wakati wowote, mungu ibariki tanzania.

  22. Comment by mbise on November 14th, 2007 2:46 pm

    hongera mzee jk, endelea kuliongoza taifa lako, salama kila la kheri, pia zingatia ushauri wa watu mbalimbali kwa manufaa ya taifa letu, hadi miaka ya mbeleni. Safari ya tanzania ni ndefu, ila kw ahaki na usawa, bila chuki na ubaguzi, tanzania itaendelea sana, na kudumisha upendo milele, all the best president.

  23. Comment by sibah on November 21st, 2007 9:24 pm

    wachoyo sana jamani, mnakula wenywewe makubwa basi.

  24. Comment by sinead on December 6th, 2007 5:27 pm

    hahah..that’s true yatima baby look like rashid and khalfan..mmh!!!?..OH UR 57 NOW happy birthday..cheers xx

  25. Comment by Fadhili Gwigilila Misigaro on February 25th, 2011 2:56 pm

    HONESTLY, Nimeipenda familia ya RAIS HASA HAO WATOTO, They are so happy of their DAD’S BIRTHDAY. Happy family

Leave a Reply