MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Nature ambaye kama mtakumbuka BongoCelebrity iliandika juu ya kuchaguliwa kwake kuwania tuzo za kituo cha televisheni cha Channel O zijulikanazo kama Channel O Spirit of Africa Music Video Awards, ameshinda!

Juma Nature ambaye alihudhuria utoaji wa tuzo hizo zilizofanyikia katika ukumbi wa jiji la Johanesburg (Johanesburg City Hall) nchini Afrika Kusini hivi karibuni , ameshinda kwa upande wa video bora kutoka Afrika Mashariki kutokana na wimbo wake Mugambo.Matokeo kamili unaweza kuyasoma katika tovuti ya Channel O.

Katika mazungumzo mafupi tuliyofanya naye baada ya kurejea toka Afrika Kusini na ushindi, Nature amewashukuru watanzania wote waliompigia kura ili ashinde.Amewataka wote kuendelea na moyo huo huo kwani sio tu kwamba wanasaidia kukua kwa muziki wa kizazi kipya bali pia kuzidi kuitangaza Tanzania katika medani za kimataifa.

Wimbo Mugambo ulirekodiwa katika studio za Bongo Records na video ikatengenezwa na Visual Lab iliyo chini ya uongozi wa Adam Juma. BongoCelebrity inampongeza Juma Nature na wote walioshirikiana naye kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha ushindi huu. Siku za nyuma tuliwahi kufanya mahojiano na Juma Nature ambayo unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

14 Responses to “NATURE ASHINDA TUZO ZA CHANNEL O!”

  1. Comment by Dinah on October 13th, 2007 1:29 pm

    Mimi napenda mpangilio wa meno yake :-)

    Hongera JN kwa ushindi huo.

  2. Comment by jull on October 13th, 2007 2:53 pm

    SHEIKH YAHAYA ALITABIRI USHINDI WAKE

  3. Comment by kibunango on October 13th, 2007 7:11 pm

    Hongera sana

  4. Comment by Kasyome on October 14th, 2007 6:38 am

    Hongera sana Necha!
    Yaani huyu jamaa alipotangazwa tu kwa mara ya kwanza kwamba anawania hii tuzo niliamini angeshinda tu!Kwa nini?Msikilize!!!!!!

  5. Comment by TanzanianDream on October 14th, 2007 1:17 pm

    Duuh Wabongo bwana wanafki mno eti nilijua atashinda mbona hukujua atashinda MTV Europe?au ulijua halafu akashindwa?

    Nway huyu jamaa ndo msanii mwenye mganga hodari kwa wasanii wa Fleva labda anashindana na bwana Mheshimiwa kwa kuwa na mganga hodari…

  6. Comment by Big Willy on October 15th, 2007 3:14 am

    Big up sana mtoto wa kiumeni mwendo huohuo kaka kaza buti aminiaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mlume

  7. Comment by kinono on October 15th, 2007 10:26 am

    Lakini wanamuziki wa kibongo kwa nini wengi wanakuwa wachafu?

  8. Comment by mohamed on October 16th, 2007 10:05 am

    Hongea mgoshi!

  9. Comment by emanuely lwilla a.k.a CHOMA P on October 16th, 2007 1:52 pm

    BIG UP KAKA KAZA MWENDO ILAINAKUBIDI UBADILIKE KAKA SI UNAJUA MWANZO MGUMU SIKU ZOTE M2WANGU SAIZI KILICHO BAKI CHEKI LIFE LAKO KAKA SIUNAJUHA MAJUKUMU.SINA MENGI KAKA

  10. Comment by speed on October 18th, 2007 3:23 am

    T/dream nmeshindwa kukuvumilia kwakweli,ninachofanya ni kukukanya ndugu la sivyo utaishia kubaya,watu wakiamua kukasaka uwape ushahidi watakupata tu hata ujifiche vipi…ohooo!!!!!11

    anyway,msitu wa vina…ohi ohi oi oi..sana tu mtu wangu…endelea ziba ziba vilimi limi vya watu mpk waje wakupigie magoti mtu mzima.

    kikubwa nimemiss michano yako style za “hili game”,otherwise kwa bongo uko juu.

    Hongera sana mtu mzima….

  11. Comment by Simon Kitururu on October 18th, 2007 4:09 am

    Hongera Mkuu!

  12. Comment by beutness on October 19th, 2007 5:12 am

    mi simfagilii hata kidogo, aache unafiki umbeya na majungu.

  13. Comment by MIJIHELAAAAA! « MWENYEMACHO DOT COM on November 12th, 2007 2:27 pm

    [...] kusema blogu zina nguvu kubwa sana katika kubadili upepo wa matokeo ya kitu fulani. Kwanza ilikuwa Juma Nature juzijuzi pale kwenye tuzo za muziki za Channel O, akanyakua ile kitu. Halafu leo usiku, baada ya [...]

  14. Comment by MIJIHELAAAAA! « MWENYEMACHO DOT COM on November 12th, 2007 2:31 pm

    [...] kusema blogu zina nguvu kubwa sana katika kubadili upepo wa matokeo ya kitu fulani. Kwanza ilikuwa Juma Nature juzijuzi pale kwenye tuzo za muziki za Channel O, akanyakua ile kitu kwa nguvu ya kura ya wadau. [...]

Leave a Reply