Pichani ni mojawapo ya bendi kongwe kabisa nchini Tanzania,The Kilimanjaro Band “Wana Njenje”. Bendi hii ilianzishwa mwaka 1973 mkoani Tanga enzi hizo ikiitwa The Revolutions kabla ya kuhamia jijini Dar-es-salaam mwaka 1979.Jina The Kilimanjaro Band walianza kulitumia mwaka 1989 walipokuwa ziarani nchini Uingereza. Raha kamili ya “mduara” utaipata kwao.

Kwa muda mrefu walikuwa na makazi ya kudumu pale Ambassador Plaza(zamani Gogo Hoteli) mpaka miezi michache iliyopita walipohamia Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay ambapo kila ijumaa wanatoa burudani pale.Mafanikio ya bendi hii yamechangiwa na kujiendesha kama kampuni(The Kilimanjaro Band Company) huku kila mwanamuziki akiwa na hisa na pia kupokea mshahara mwisho wa mwezi kama kampuni za kawaida. Ni mojawapo kati ya bendi chache sana nchini Tanzania ambazo zimedumu kwa muda mrefu namna hiyo bila kusambaratika au kupotea kabisa.

Feedback / Comments

4 Responses to ““WANA NJENJE””

  1. Comment by mesa on October 17th, 2007 4:28 pm

    Jamani umenigusa penyewe yani nikukumbuka mduara we acha tu MAMACHANJA MAMACHANJA MIE NJAA YANIUMA, big up kumbe mna hisa safi sana, Mie namsubiri somo weut Dinah wa wambo flani, safi sana

  2. Comment by TanzanianDream on October 18th, 2007 12:17 am

    Wow atlast nasikia neno maendeleo limetajwa kwa maana isiyo wazi….Tatizo hizo hisa ni zao tu au kuna public ownership pipo cud get somthn’ from supportn them….

  3. Comment by Kimori on October 18th, 2007 1:42 am

    You look great NJENJE and you are douing a good job…keep it up!

  4. Comment by Mwaju on October 19th, 2007 11:01 am

    you did a good job but u r so quit for a very long time na mkumbuke umaarufu wenu kwa watanzania wengi ni kwenye mduara tu kutupigia aina nyingine za muziki ni kutukatili mashabiki na kujiporomoshea umaarufu

Leave a Reply