
Picha ya leo ni hiyo ya Mlima Kilimanjaro. Mlima huu ni mojawapo ya vitambulisho muhimu sana vya nchi yetu. Ukisikia The Land of Kilimanjaro unajua nini kinaongelewa. Matangazo ya televisheni ambayo yamekuwa yakionekana hivi karibuni katika vituo mbalimbali vya televisheni Ulaya na Marekani ya Kaskazini hususani CNN,huenda yakasaidia kuukumbusha ulimwengu na pia jirani zetu kwamba Mlima Kilimanjaro upo kaskazini mwa Tanzania na si vinginevyo. Mtu ambaye anapewa heshima ya kuwa mtu wa kwanza aliitwa Yohani Kinyala Lauwo (baadaye alijulikana zaidi kama Mzee Lauwo). Cha ajabu alipomsindikiza mzungu wa kwanza kuupanda Mlima mjerumani aliyeitwa Hans Meyer, vitabu vya historia (potofu) vikampa sifa zote Hans Meyer. Mzee Lauwo alizaliwa mwaka 1872 na akafariki mwaka 1996. Unaweza kusoma kuhusu historia hii zaidi kwa kubonyeza hapa.
Feedback / Comments
4 Responses to “PICHA YA WIKI # 6”
Leave a Reply


sending...
Picha nzuri sana hii.Asanteni pia kwa hiyo information ya Mzee Lauwo.Hapo ndio ninapowapendea BC,kila post ina information muhimu and sense.Endeleeni kuelimisha na kuburudisha.Patrick-Houston TX
Wow!
i like what your doing keep it up to preserve our culture.good job
Interesting piece. This is yet another sad testament to how Europeans and other foreigners are branded as authorities on Africa’s history and heritage.