
Hivi karibuni blog maarufu ya Michuzi ilifikisha watembeleaji milioni 2.Wakati watembeleaji hao wakielekea kufikia idadi hiyo, kulikuwa na shindano la mtu atakayekuwa wa milioni mbili kamili,bila pungufu wala nyongeza.
Baada ya mchakato mzima aliyefanikiwa kuibuka mshindi ni Brian Mariki,mtanzania aishiye Houston,Texas. Brian alijinyakulia zawadi ya $ 500 taslimu kama ilivyokuwa imeahidiwa.
Pichani Issa Michuzi (kulia), akitimiza ahadi hiyo kwa kumkabidhi mama mzazi wa Brian, mke wa Balozi Richard Maliki zawadi hiyo ambayo kupitia kwake itafikishwa kwa Brian ambaye ndiye ameelekeza kwamba zawadi hiyo ipitie kwa mama yake mzazi. Hongera Michuzi kwa kutimiza ahadi na Brian kwa kuibuka mshindi.
Feedback / Comments
One Response to “ZAWADI”
Leave a Reply


Why thank you!