
Miongoni mwa nyimbo zenye mahadhi ya mwambao zilizotokea kupendwa sana ni ule uliojulikana kama “Njiwa” uliokuwa na mashairi yenye maneno kama “ewe njiwa,ewe njiwa,peleka salamu”. Mwimbaji wa wimbo huo alikuwa ni Patricia Hillary, malikia wa taarabu enzi hizo. Pichani ni Patricia Hillary akifanya vitu vyake. Patricia bado anajishughulisha na muziki na kuna habari kwamba amevirudia upya vibao vyake vilivyotamba enzi hizi ambavyo bado vinapendwa na wengi.
Page 1 of 3 | Next page