Ni ijumaa tena.Wakati mwingine wa kupata midundo.Leo tunatoka ndani ya jiji mpaka mji kasoro bahari.Pale tunamkuta marehemu Mbaraka Mwinshehe(pichani) akiuambia umma kwamba sasa amehamia Mtaa wa Saba,kutoka kule alikokuwa akiishi ambapo mapaka yalikuwa hayaishi kulia lia.Anasema ile nyumba aliyokuwa anaishi sio nyumba,ilikuwa na mikosi…Wimbo huu ni kutoka katika mkusanyiko wa nyimbo zake ulioitwa Ukumbusho Vol.2.
Hivi ni kweli kwamba mahali unapoishi panachangia sana kufeli kwako au kufanikiwa kwako?Wewe unasemaje?Sikiliza ujumbe,pata mdundo,sikiliza nyuzi bin nyuzi ya gitaa la Mbaraka.Ijumaa Njema!
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page