
Yapo mambo ya kitaifa ambayo sote hatuna budi kushirikiana katika kupambana nayo.Mojawapo ni ugonjwa wa ukimwi.Raisi wetu,Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete miezi michache iliyopita,kama wanavyoonekana pichani,walituongoza kwa mfano wa kivitendo katika vita hiyo.BC leo inapenda kukumbusha kuhusu kampeni hiyo yenye kauli mbiu Tanzania bila Ukimwi inawezakana.Bila kunyosheana vidole,kutengana,kutupiana lawama wala kumnyanyapaa mwingine kila mmoja wetu ana wajibu katika vita hii.
Feedback / Comments
18 Responses to “TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA-JK”
Leave a Reply


haya bwana we endelea kudanganya umma na majibu
huyo baba mbona kaathirika siku nyingi?
J na Mama Salma Kikwete ni wanandoa….nini sababu ya kupima? Inamaana mmoja wao sio mwaminifu au?
Kama nyote ni waaminifu ndani ya ndoa/uhusiano wenu kwanini mkapimane?
Tupime ngoma ikiwa hatuna uhakika na afya zetu hasa baada ya wapenzi wetu kutokuwa waaminifu au sisi wenyewe kutokuwa waaminifu……vinginevyo ni kusanifu waathirika
Watanzania waanza kujifunza na kuamini matumizi ya Condom, wajifunze kuridhika na mpenzi mmoja. Kama unataka mpenzi ajuaye mambo basi ni wajibu wako kumfunza huyo ulienae ili mfurahi wote na sio kwenda kusaka mwingine nje ya ndoa/uhusino ukidhani utapata bora zaidi.
Wakati umefika WaTz tubadilike……mnaudhi sana.
mfano wameonyesha kwa watanzania, hongera zenu, kwani jamii inafurahishwa na mambo mnayofanya, tunawatakia mmalize mwaka salama, kwa kusameheana na kuzungumza, ili kufikia muafaka na kutatua matatizo.
lazima wapime, kwani wanandoa hawapimi, wanaonyesha mfano kw ajamii jamani.
Ivi wanapimaga nini? vihamba au?
Unfortunately, HIV/AIDS is going to touch every single family in our country if obstinacy from unprotected sex is not maintained. The estimated figures of the infected population are so alarming, especially when you are out of the country than when you are in!
Going for the test is not the most effective way in a corrupt country like ours, or rather people should change the mindset! It was earlier thought that HIV/AIDS is notorious among the poor population, but this has not been the case so far!
Kimori hapo umesema kitu cha msingi sana kuhusiana na swala la upimwaji wa virusi vya UKIMWI ktk nchi iliyokubuhu ktk rushwa (kutokana hali ngumu ya maisha kila mtu anajiangalia yeye a.k.a ubinafsi)
Kuna watu (wale wanaopima ili kufunga ndoa au kuanzisha uhusiano mpya wa kimapenzi) wanalipa Docs ili waandikiwe HIV- wakati ni HIV+, vilevile kuna swala la kuogopana…..Doc unapigwa mkwara sasa kwa vile unahofia kupoteza kazi….mwenyewe unaweka majibu chanya wakati ktk hali halisi ni hasi.
Vita ni yetu sote sio kwa kupima nakujitangaza bali kubadilisha tabia na kuwa na mpenzi mmoja unaeshiriki nae Ngono, Pia tumia kinga (condom) kwa kila tendo unless mnataka kummimba/kumimbwa(kuzaa).
Utamu wa ngono unadumu kwa muda usiozidi nusu saa na ni bure kabisa lakini HIV ni mpaka kufa na ni gharama pia kuishi na virus vyake kwani utahitaji lishe bora, madawa ya mara kwa mara ambayo mpaka mwaka jana yalikuwa yakigharimu $180.
Tubadili tabia jamani…..thamini mpenzi wako….thamini utu wako. Mnaudhi!
Tunaudhi kina nani?unataka tuweke mambo yako hadharani hapa kama unamdanganya jamaa?we dinah tulia bana!!kisha tunatakiwa tufate dini zetu hakuna kuwa na mpenzi 1 unaeshiriki nae ngono unachotakiwa kuwa na mke unaefanya nae mapenzi nafikiri hiyo ndio dawa pekee kuacha uasharati basi,sio condom sio kuwa na mpemzi mmoja uongo mtupu.
Wote wenye tabia chafu ya kungonoana ovyo tena bila kinga hasa nje ya mahusino yenu iwe ndoa au vinginevyo.
Wabongo bana eti mnaudhi! wewe sio mbongo dinnah? eti anajitenga kwa sababu yeye haudhi na hana ukimwi! Tukapime na kisha tujihadhali na vyanzo vyote vya ugonjwa huo.
dinah sio mbongo, huna habari, yeye ni muitaliano.
kupima naona, na ya lowassa na mywife. Au wamebania, maana bibie yule nae, ana uchu.
Yaani jamaa kutoka maisha bora kwa kila mbongo hadi Tanzania isiyo na UKIMWI inawezekana.
Issue si kupima, u-salama?Na km umeathirika au hujaathirika u-tayari kubadili tabia?Nani wa kwanza kuonyesha njia?Viongozi wana nafasi yao…. wakuu wa dini…. mkuu wa familia….. kiongozi gani ameshaonyesha njia hata kwa kujitangaza tu kwa umma? Ili watu wa-feel kweli that UKIMWI hauna mtoto, mkubwa, kiongozi, Kasisi etc.
Huku Netherlands na ulaya magharibi (Western Europe) nzima UKIMWI si tatizo but incase hata mwalimu wa shule ameupata anajitangaza shuleni. Ni mwalimu gani Tanzania anaweza fanya hivyo? Kama viongozi tu wanaficha?
Kama Mkapa ali-declare ni janga la Taifa,lazima tu-deal nalo kitaifa. Actors wa UKIMWI ni kila mtu, play your part,ila waonyesha njia hamjaweza PLAY YOUR PART.Kwanini part yenu iishie kupima na ku-advocate matumizi ya condom tu? Basi hata mtupe majibu ya kweli.
Tanzania ni “secular state”. Ila watu wake are releigious.Ikiwemo nyie viongozi wetu. Sasa km mnadanganya umma,ni mnamdanganya Mungu wenu pia.
Tubadilike na kila mtu acheze nafasi yake.
Mr. President said he was nervous after atking the HIV test, I think he should explain WHY? He has been maried forever, there’s no need to be worried.
HE! Mr prezii was nervous??Huyu JK nae bwana drama tupu. Sasa alikuwa anaogopa nini????Kumbe anajua kuwa ayafanyayo ndio sio eeeee!!!
nyie wote washamba kupima muhimu nyie mnataka rais asiye wa mfano kuwa nervous is part of being a human dont say nyote mko fit!!!!!!!!!!!!1