Picha ya wiki hii ni hiyo ya Hugh Ramopolo Masekela,mwanamuziki mahiri na mashuhuri kutoka Afrika Kusini.Masekela ameshafanya maonyesho mengi nchini Tanzania.Hivi leo huwezi kutaja majina makubwa ya wanamuziki kutoka barani Afrika bila kulitaja jina la Hugh Masekela.Wanaojua historia ya muziki watakushangaa ukifanya hivyo.Hugh Masekela alizaliwa tarehe 4 Aprili mwaka 1939 huko Witbank,Afrika Kusini.

Aliwahi kuwa mume wa Miriam Makeba(jina lingine kubwa la muziki barani Afrika) kabla ya kutalakiana mwaka 1966.Kwa habari zaidi za mwanamuziki huyu bonyeza hapa.Ukitaka kutizama mojawapo ya video zake,bonyeza hapa.Hii ndiyo picha yetu ya wiki.Imepigwa na MichuziJR

Feedback / Comments

Leave a Reply