
Swali lililopo kwenye kichwa cha habari hii ya leo linaweza kuwa na majibu chungu mbovu.Tunaweza kuendelea kujiuliza kama tunapenda.Pamoja na hayo,jambo moja lililo wazi ni kwamba mazingaombwe ni mojawapo ya sanaa kongwe sana ulimwenguni.Kama una tafsiri yako kuhusu mazingaombwe usisite kutuambia wenzako.Tupo hapa kujifunza na kuelimishana pia.
Vilevile kama unazikumbuka enzi zile ulipokuwa shule kisha matangazo ya kuhusu ujio wa mwana-mazingaombwe yakaanza kusambaa, jamaa akaja mstarini akawapeni sample kidogo ya mazingaombwe yake,utakuwa pia unakumbuka jinsi ambavyo ulikuwa unaenda mbio ikitokea kwamba mazingaombwe yanakuja shuleni kwenu na wewe huna kiingilio.Sema ukweli,ulikuwa unafanyaje ili usiyakose mazingaombwe?
Lakini si unakumbuka kwamba kulikuwa hakuna wana-mazingaombwe wanawake? Jadi hiyo siku hizi imevunjwa na Akanashe Joan(pichani juu).Huyu inasemekana ndio mwanamke wa kwanza mwanamazingaombwe Afrika Mashariki. Sanaa hii yeye amejifunzia au kuisomea nchini China. Hivi leo ni mwanamazingaombwe maarufu nchini Tanzania akitoa burudani popote walipokusanyika watu.
Feedback / Comments
13 Responses to “MAZINGAOMBWE NI NINI?”
Leave a Reply


sending...
Akanashe wewe endeleza fani, safi sana.
Nasikia hata Odemba ni mwanamzingaombwe au “karitaya”
Mwanamazingaombwe*
Huyu kama ndio demu wako ukimkorofisha anaweza kuhamisha hamu zako akapeleka ndiko kuliko siko nomaaa
ila Big Up Dadaa
but she needs some innovation to make her job reputable,sio vizuri kufanya maonesho kila kwenye kusanyiko la watu…let her find special venue for special audience..sio kila akiona watu anandunduliza au labda siajelewa
Akiingia Shinyanga wanamchoma moto fasta, wana usongo sana na wachawi au kile wanachodhania ni uchawi! Ashauriwe a-stay put kwenye sehemu zinazorecognize art and talent as just that, basi.
HUU SASA UCHAWI WA KINAIJERIA. HII ELIMU YA MAZINGAOMBWE HIVI INATOFAUTI GANI NA UCHAWI AMBAO WATU WANARUKA KWA UNGO? HIVI HUYU NI MZALIWA WA TANZANIA AU KATOKA NIGERIA? USIKUTE NI MPOPOZZZZ(NIGERIAN) NA WASI WASI NA URAIA WAKE.
aiseee hii dili kweli, maana kama unaweza badilisha karatasi zikawa pesa, shida ya didi watu kubomoa mabenki, si wakusanye karatasi wakamuone awabadilishie jamani, nikija bongo nitamtafuta.
NO COMENT! ney nakusupport- she is totally witch
mmhhhhhhhhhhhh
Jamani Huyu Dada Sio mchawi kaanza mbali hajaanza jana wala leo. Kwa kifupi yule anaetake kujua chochote muulizeni atawaambia……Si mpompo ni Mbongo mzawa kabisa!!!
Na kuhusu uchawi, uo sio uchawi its called illusions…..a misinterpretation of an experience of sensory perception, especially a visual one, where the stimuli are objectively present and the mistaken perception is due to physical rather than psychological causes……..Siwezi kuexpalin kwa kiswahili
Kazi kwenu kama hamtaelewa……..Jua Facts kwanza kabla hujameka Comment.
Akanashe endelea na Art yako……….Represent.
Mwanao!!…”
Duh!
bado Tupo nyuma watanzania kisanaa huh!,
sijawahi kuview hii page.watu wanachonga.I wish ningekuwa na muda wa kuwaeleza waliocoments wasiyoyajua ili kufumbua uelewa wao kuhusu mimi,nimeanzaje,nimefaidikaje na sasa nipo wapi na sanaa hii ya mazingaumbwe….ULILOLIJUA……….!!!!!!!!!!!!!!
Ni uchawi.
hivi uchawi unavuka bahari?