TULIPOONGEA NA RITA PAULSEN.

 

 

Ukizungumzia wanawake wajasiriamali(entrepreneurs) nchini Tanzania,huwezi kukosa kumtaja Rita Paulsen (pichani),Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni maarufu ya Benchmark Productions yenye makao yake makuu jijini Dar-es-salaam.

Rita ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 12 kwenye masuala ya utengenezaji matangazo na masoko,sio tu ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo yenye mafanikio nchini Tanzania na kimataifa, bali pia ni mmojawapo wa majaji katika show maarufu ijulikanayo kama Bongo Star Search. Show hiyo ambayo hivi karibuni imezidi kujipatia umaarufu mkubwa nchini Tanzania,ni ubunifu mwingine mahiri wa Rita na kampuni yake ya Benchmark Productions.

Show hiyo ambayo hurushwa kila jumapili mara tu baada ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia kituo cha televisheni cha ITV,inasemekana ndio show ambayo ni “very interactive” nchini Tanzania kwa maana ya kwamba inampa mtazamaji nafasi ya kutoa maoni yake au dukuduku lake wakati huo huo inapoonyeshwa. Hilo linawezekana kwa kutumia tekinolojia za kisasa za simu,sms nk.

Hivi majuzi BC ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na show hiyo. Katika mahojiano haya Rita anaweka wazi mustakabali mzima wa show hiyo na pia kutoa ushauri makini kwa vijana wa muziki wa kizazi kipya kuhusiana na kazi zao za kisanii na maisha kwa ujumla.Pia anajibu swali ambalo limekuwa likiulizwa na wengi;kwanini wakati mwingine majaji wa Bongo Star Search huwa “wakali” namna hiyo??!Fuatana nasi katika mahojiano hayo.

BC: Rita Paulsen, karibu sana ndani ya BongoCelebrity.

RP: Asante sana.

BC: Kama kawaida,kwanza kabisa tungependa kujua historia ya maisha yako kwa ufupi.Ulizaliwa wapi,lini,ukasomea wapi nk

RP: Mimi nimezaliwa Tanzania mkoa wa Kagera wilaya ya Karagwe. Nimesomea Uganda na Harare-Zimbabwe.

BC: Wengi tunafahamu kwamba hivi sasa wewe ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark. Ilikuwaje kuwaje ukaanzisha Benchmark Productions? Je kuna uhusiano wowote kati ya Benchmark yako na Benchmark Productions ya huko Muskegon, Michigan nchini Marekani?

RP: Hakuna uhusiano Benchmark ni kampuni inayojitegemea. Nilianzisha Benchmark kwa sababu kwanza nilikuwa napenda sana kujiajiri na pili wakati nimeanza kulikuwa hakuna production house za quality(viwango) vizuri.Niliamini nitaweza kubadilisha hilo yaani to make a difference because of my creativity and the love I have for the work I do.

BC: Unakumbuka ulivyokuwa mtoto ulitaka kuwa nani?Na kama kuna mahali uliachana na ndoto hiyo unadhani nini kilitokea?

RP: What I am today is what I wanted to be. Thank God.

BC: Sasa tuje kwenye kiini hasa cha sisi kutaka kufanya nawe mahojiano haya.Ni kuhusu Bongo Star Search.Kwanza kwa mtu ambaye hailewi nini maana ya Bongo Star Search unamuambiaje na ilikuwaje mkaamua kuanzisha kitu kama hiki?

RP: Kwa kifupi ni shindano la kumtafuta msanii chipukizi nchini Tanzania mwenye kipaji na ambaye hajawahi kurekodi pamoja na kipaji cha hali ya juu alichonacho. Tuliamua kuwasaidia watu kutimiza ndoto zao kwani ni wazi kwamba kuna watu wengi wenye vipaji ambavyo havijavumbuliwa.Tanzania ni nchi ambayo imebarikiwa na vipaji mbali mbali na ndio maana tuliyaanzisha mashindano haya.

BC: Mpaka hivi sasa unalielezeje shindano zima linavyokwenda?Nini kinaendelea hivi sasa?Nini siri ya mafanikio ya show hii ambayo inaendelea kujizolea umaarufu siku baada ya siku?

RP: Kwa sasa shindano limebakiza washiriki 20 ambao wanasubiri kupigiwa kura na watanzania. Vipindi takriban 10 vimesharushwa kupitia runinga ya ITV.

Mafanikio ya show hii inatokana na uhalisia wake kwani inamgusa kila mwana jamii nchini (Reality). Pia matumizi ya lugha yetu ya Kiswahili inafanya shoo hii kupendwa na wengi. Majaji na washiriki wanawiana kwa kila kitu kwa ujumla ni burudani ya kipekee.

 

Rita Paulsen.

BC: Majaribio(audtions) ya mwanzo ya Bongo Star Search yanafanyika katika mikoa kama sita tu hivi(Dar-es-salaam,Mbeya,Dodoma,Mwanza,Arusha na Zanzibar).Ni kwanini mliamua kuchukua mikoa hiyo tu?Je hamdhani kwamba hiyo inawezekana kuwa imewanyima nafasi vijana wa mikoa mingine hasa tukizingatia hali halisi za uchumi za vijana wetu?

RP: Mwaka jana tulifanya auditions Dar-es-salaam pekee kwa sababu uwezo wetu kifedha ulikuwa hauturuhusu.Mwaka huu tumejitahidi kwenda kwenye mikoa michache zaidi kama ulivyoitaja.Mwakani Mungu akipenda tutafika kila mkoa.Mwanzo mgumu lakini tutafika.

BC: Na pia kabla hatujaenda mbali sana,mshindi anapata zawadi zipi hasa? Na pia watu wengi wangependa kujua mshindi wa mwaka jana yuko wapi na nyie mnahakikisha vipi kwamba anaendelea kusimama imara katika fani?

RP: Kama ilivyoada zawadi zitatangazwa siku 14 kabla ya fainali na mwaka huu zawadi zitaboreshwa zaidi.

Mshindi wa mwaka jana Jumanne Iddi amefanikiwa kurekodi albamu mbili ambazo zinafanya vizuri kwenye kumbi mbali mbali na pamoja na wapenzi kununua kanda zake.

Amepata mafunzo ya kutosha kuhusu haki miliki na jinsi ya kujiendeleza kimaisha. Kwa ufupi maisha yake yamebadilika kupitia Bongo Star Search.

 

Mshindi wa shindano lililopita la Bongo Star Search,Jumanne Iddi,akiwa ameshikwa na butwaa siku alipotangazwa mshindi wa BSS.

BC: Kwa ujumla vijana wengi sana walijitokeza kujaribu bahati yao ya kuwa washindi wa Bongo Star Search.Ukiwa mmojawapo wa majaji,unaweza kutuambia mlikuwa au mnaangalia vitu gani hasa katika kujaribu kumpata mshindi?

RP: Tunachoangalia sana ni jinsi mshiriki anavyotumia sauti yake na jinsi anavyomiliki jukwaa. Pia tunaangalia star quality za mshiriki kwa ujumla.

 

Rita Paulsen(katikati) akiwa na majaji wenzake wa Bongo Star Search,Salama Jabir(kulia) na Master J(kushoto).

BC: Kumekuwepo na malalamiko kadha wa kadha kuhusiana na jinsi ambavyo majaji(mengi yameelekezwa kwa Salama Jabir) kuhusu jinsi ambavyo amekuwa akiwaumbua au kuwakatisha tamaa kabisa baadhi ya washiriki.Watu wengine wanasema kuna hata baadhi ya vijana waliotaka kushiriki wamekacha kutokana na kuogopa kuumbuliwa.Unaliongeleje suala hili na una ujumbe gani kwa vijana wanaotaka kushiriki siku za mbeleni?

RP: Kwa kweli watu wengi hawapendi kuambiwa ukweli na ndio maana malalamiko yanakuwepo. Ukweli wanaotoa majaji ni kuwasaidia vijana na sio kuwapotosha . Ni bora kumwambia mtu ukweli kuliko kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Hata hivyo hii inajenga kujiamini unapoambiwa ukweli na majaji kwa hiyo washiriki hawana haja ya kukacha ushiriki.

BC: Mwisho tungependa kukuuliza swali hili kwani kutokana na kazi zako za kila siku unakuwa karibu,kwa namna moja au nyingine, na wasanii wa muziki wa kizazi kipya au bongo flava.Nini mtazamo wako kuhusiana na muziki huu?Na unatoa ushauri gani kwa wanamuziki hao hususani katika suala la kutengeneza video za miziki yao?

RP: Inabidi wasanii wa Bongo flava wawe wabunifu zaidi katika tungo zao na kwa upande wa video wajitume sana kutengeza video zenye ubora.Wawe na mikakati ya kuboresha kazi zao ili waweze kumudu maisha na kuweza kufuatilia haki zao kama wasanii.

Pia nawashauri wapate mameneja ambao ni wa dhati.Ambao wanatoa kipaumbele katika kuendeleza vipaji vyao na si wa kuwatumia kwa muda na kisha kuwatosa. Meneja wa kweli ni yule anayefanikisha ubora wa kazi ya msanii wake.Wasanii wahakikishe wanatengeza hela sio usupa-staa wa jina tu!

BC:Kila la kheri Rita katika kazi zako.Asante kwa muda wako.

RP: Shukrani.Kazi njema pia.

*Kwa habari zaidi kuhusiana na show ya Bongo Star Search,majaji wa show hiyo (akiwemo Rita mwenyewe) tembelea tovuti ya Bongo Star Search kwa kubonyeza hapa.

*Kwa habari za mshindi na washiriki wa Bongo Star Search mwaka jana na zawadi walizojipatia bonyeza hapa.

Picha kwa hisani ya Rita Paulsen na Mrocky.

 1. mohamedi selemani, 14 May, 2008

  hongeleni sana bechi la,bss lakini salama acha kukatisha tamaa watu kwani hakuna alio zaliwa anajua.hata wewe hukuzaliwa unajua.

 2. Fortunate, 13 August, 2008

  Hi. i don’t want to Describe my self l, But the truth is, This Lady Could be An Angel, First if i was in the same Agement i’d prefer Her as My Woman, She Is kind, cherishing,has an innocent look i do Believe that she’s Even obidient at work, Does her Work properly. and second if i was to chose an advicer or if i am to be a Big Business man with a Firm, i’d rather have her among the Consultants in my members of Board.
  God gave her, Talent, looks and Morals, She is an ‘A’ lady, and let me grant Her if she wasto be a Today’s University Student, She could be An A or B Student, including her Outlooks in class and wherever!#
  sorry Scripture was so long but She Deserves all this Praises, The pleasure is her’s!

 3. Mary Mkwaya Malamo, 19 September, 2008

  Mzuka kwa sana Madam, Keep it up mom.

 4. john, 03 April, 2009

  Jamani Rita ni one of the Iron ladies hapa Africa.
  Naombeni mawasiliano yake yoyote jamani/////
  plzzzzz

 5. Mjololo Ng,ughuya, 02 May, 2009

  Hongera Rita wewe ni mwanamke shujaa.endelea na moyo wako wa kuwainua vijana.
  kwa mavazi uko vizuri sana,hongera,leo na mimi ni jaji wako.
  Nitwa Mjololo Ng,ughuya
  Arusha

 6. rita, 27 May, 2009

  i like u rita if possible i wil find u

 7. JimmieM;, 30 June, 2009

  …ahhhh mimi nimefurahi kwanza kwa BC na usahili kwa dada RP, pili mawazo ya wajumbe wenzangu hakika nayakubali kama yalivyo, tatu mjumbe mmoja upec upec amenichekesha, eti anataka mawasiliano ya dada Rita tena yoyote yale, Duh, enhe tena anacctiza plizzzzz, haaa watu bwana, mhhhh!
  BC mpe huyo bwana hata barua pp ya dada,
  na mwisho kwa kweli dada RP anafanya vema ila asiwe kama hao akina ”majani”, mi naamini watanzania wengi hawapendi kuambiwa ukweli moja kwa moja tena kwa ukali, mh wanapenda lugha ya upole kama ya dada Rita,
  ndio maana wanampenda…
  watanzania ni wapole,
  twende nao ivo ivo, mambo ya kenya tuyaache huko huko, nk.
  asante asanteni.
  JimmiM;

 8. Pam, 14 July, 2009

  jamani Madam nmi naomba nitoe japo kaushauri tho kwakuw nimechelewa kukatuma sijui kama katafikiriwa…na yoyote atakayeweza kuusoma naomba ampe any muusika .that kwenye upigaji kura wa kuwatoa washiriki wa bongo star search wawe wanasema watanzania tumpigie mtu ambaye atoke…na si ambaye abaki…kwani kama mtu hajui ni rahiisi wote kumnote but kwa hii ya kumpigia anayebaki ni mbaya kwani mwingine anjua kuimba sema hana ndugu na jamaa wengi maana tutake tusitake hili pia lina changia …..

 9. Msungu, A, 29 July, 2009

  Good work Rita Keep it up, U deserve cong..
  Love ya

 10. Josephina wa Arusha, 17 August, 2009

  Madam Ritha napenda unavyovaa,unavyo wa jaji wasani wetu upo juu, endelea na moyo wako huo huo.

 11. Edda Mwambusi, 02 September, 2009

  Mimi napenda kujua historia ya Rita mbona hekima na busara aliyopewa na Mungu sio za kawaida?

 12. lin, 07 September, 2009

  i realy admire u sana yani sana u r a woman of ambition and status n ur achiements are excellent.
  besides u r beautiful, u hav kind heart u hv helpd a lot of people is like u gv and get.

  all the best for ur future success

 13. frank, 25 September, 2009

  NICE WORK MADAM RITHA……………..! You are incredible and realy I appreciate everything in your presence….. thanx for being whom you are and GOD will bless you….!

 14. yasmine, 30 September, 2009

  madam uko juu sn salama acha kuvunja watu moyo wape hope pf upo juu i realy like u mastey j ur the same like salma

 15. CHRISTINA, 30 September, 2009

  hi,
  madam rita mimi nakufagulia sana, your a good woman i love you so much.

  its me tina wa tanga (tanga city council)

 16. WITNES MAMUYA, 30 September, 2009

  hello!!!
  kila mtu ana jinsi anavyoishi na watu ma maongezi yake,so mnavyo mlaumu salama si kuwa atapretend kuwa vingine while sivyo,jaribuni kuangalia mnavyosema na hali halisi,

  then madam ritha anafanana na mama wa kiafrica sababu ana sifa zote ambazo mama anatakiwa awe nazo,

  nampenda sana na anaweza kuishi na mtu yeyote

  take care n may god bless you mam!!!!!!!!!

 17. ANDREW KISANGA, 30 September, 2009

  yap maadam rita keep it up but remember to change your idea about judges like salama michosho wanatakiwa wawape moyo washiriki na sio kuvunja mtakosa washiki mwakani……..congratulation.

 18. kukuku, 01 October, 2009

  madam ritha pamoja majudge wenzako hamfai kuwa majudge! hamtakiwi kupiga makofi au kushangilia wakati mwimbaji anaperform mnachotakiwa ni kufanya jugement! im real bored na tabia zenu

 19. godwin, 01 October, 2009

  salama nenda shule acha kuuza sura shule yenyewe unaungaunga!

 20. maochieng, 02 October, 2009

  salama big up wabongo hupenda kusifiwa hata kwa kitu hawakiwezi. endelea kuwaambia ukweli wajifunze.

 21. maochieng, 02 October, 2009

  Madam rita asante sana kwa kumwibua Kasian wa Mwanza mwaka huu. hakika yule kijana ana sauti ya kuimba ya kiume. i wish angekuwa anaweza imba kizungu aimbe nyimbo za Barry White. ananikumbusha project fame ya South Africa mwaka 2003. alikuwepo kijana wa Nigeria anaitwa Daree alikuwa anaimba Bess utaipenda kama yeye. Pse mwambie Kasian aimbe nyimbo ya Don Williams ya “You are my best Friend.” kwa sauti yake atatukoga nyoyo mashabiki wa BSS.

 22. GEOFREY, 07 October, 2009

  Keep it up madam We see your efforts

 23. GEOFREY, 07 October, 2009

  Hi to all judges, nawashangaa sana watanzania wanaowaponda majaji hususani Salama hivi mnataka majaji wanaowabeba wasanii hata kama wanaimba vibaya? Tunahitaji vipaji sahihi na sio blabla.muziki ni fasihi na kazi ya fasihi ni kukosoa panapokuwa na dosari .Na sasa mnataka hata kama wanaimba vibaya wasifiwe, hapana majaji naomba muongeze ukali katika maamuzi ili mtupatie mshindi sahihi. angalieni mtu kama Kassian bila ukali wa majaji kumtaka abadili style ya uimbaji angetisha kama anavyotisha hivyo? bila kumsahau jackson.

 24. Basil, 08 October, 2009

  “HONGERA SANA MADAMEE”
  Hakuna anayepingwa kwamba r byuti n intellegent woman, na dada zetu wakipata nafasi inabidi wajifunze toka kwako na hata sisi vidume twabidi kujifunza mengi sana toka kwa madamee… nakuita madamee coz u got the same name as ma gal nem na wadogo zangu used to col her with dat nem..
  “NDELEA NA MOYO HUO” wa kuinua vipaji na kuwawezesha vijana wa kitanzania kusimama kwa miguu yao..
  2009 BSS ni ya ukweli na washiriki wako poa, mimi nipo kwenye boti ya PETER MSECHU but hata PASCAL(baba ritha jr)akiwa mshindi sito shangaa.. kaza buti madamee natamani BSS iendelee hadi nitakapo zeeka na sasa i’m only in 20s…
  contact: wajimilajr@yahoo.com

 25. Basil, 08 October, 2009

  Wanaomponda SALAMA kwamba anua sana basi nafikiri hawafuatilii TUSKER PROJECT FAME na kumuona jaji IAN, nadhani wakimuona IAN watamuacha SALAMA afanye kazi yake…
  KAZA BUTI SALAMA “DO YOUR JOB”

 26. elizabeth swai, 09 October, 2009

  nawapa hongera majaji wote

 27. domin lema, 09 October, 2009

  you guys ur work is great! mungu akubariki sana madame! salama ni judge mzuri sana! kaza uzi mamy!
  chaaa!oooo

 28. Beatus N, 15 October, 2009

  Well done Rita!!!!!! Keep it up!!!Thanks for makin people stars!My request try to train them how to gave thanks to their fun…or let me say to talk to the media to do as star.May GOD bless u…

 29. Cresencia, 01 November, 2009

  I like this argument from you Madam Rita: “What I am today is what I wanted to be”. In life; very few people achive this! I am happy for you Rita

 30. wakuvwanga, 02 November, 2009

  welldone madam bt it seems huwa na mahaba na baadhi ya contestants kama kevin mhhhhhhhh am not sure but next tym msitangaze mapema matokeo coz unawavunja moyo washiriki mpaka wanashindwa ku perfom well nihayo tu

 31. millen, 12 November, 2009

  nakupa big up kwakuinua vijana ww nimsaada kumbwa kama mama maria wa yesu ubarikiwe na bwana

 32. chichi, 24 November, 2009

  mamy i lav u,napend sana kaz yako god bless you………

 33. Phil M, 03 December, 2009

  Whatever you are doing girl… just keep on doing it for you know you are doing the right thing.

 34. jacqline, 19 February, 2010

  naomba niwe mchangiaji mchelewaji
  inshort Salama anasema ukweli ingawa andiscourage,msimponde cause hakuna mkamirifu.

 35. Hucna, 14 April, 2010

  Wooooow,sooooo gud,keep it up madam!!I real appriciate ur goodness,the show z so 9c!!I wsh all females 2b lyk wat u do at their respective areas.Be blessed

 36. vennis, 01 June, 2010

  da kweli ant wewe ni mzuri na usiyependa makuu. unayependa kusaidia endelea hivyo hivyo Mungu yu nawe.

 37. nteeh Mbwambo, 30 June, 2010

  Big up Ritah

 38. MUSAMWAKIPOSA, 07 August, 2010

  MI NAONA WOTE MKO POA TU MAJAJI WETU ONGEZENI BIDII HILI KUPATA WASANII BORA HAPA KWETU TANZANIA.PIA SALAMA YUKO POA TU.

 39. eliza, 01 September, 2010

  sema tu bado nasoma na nipo boding ila ninge jiunga na bss na madam ungenikubali ilove ya work

 40. ritha, 28 September, 2010

  upo juu mamaa ritha nakufagilia ile mbaya…………….. strength of woman

 41. Mwilla Z, 20 October, 2010

  Bongo star search season hii ime advance zaidi. Lakini sisi wadau tunaona kama muda mwingi mnaonyesha maisha ya washiriki kwenye jumba lenu. Nafikiri hii siyo Big Brother wala Maisha Plus.

  We need to see participants performing. Tunaomba hizo story zipungue na watu wapate wanachokisubiri – MUZIKI

 42. Benson Lucas Munuo, 07 December, 2010

  Big up Madam Ritah ,upo juu ile mbaya,endelea na moyo huo huo wa kuinua vipaji vya wasanii washanga.

 43. Rita, 14 December, 2010

  Hi Rita .. ‘my name sake aint our name ”beautiful?” Oh I know and believe so. To say the truth Rita, what you are doing for the youth in the music industry is really great. I congratulate you on this and many more. In Life, if you could touch people heart in a special way or give way forward for their lives in a unique way…You are a wonderful humanbeing despite of all shortfalls that ”each one of us have…No one is ever a perfectionist no matter how much we want to be. We all differ somewhere along the life channel and thats why we are ALL different, we think differently, we feel differently, we differ…only that we all smile or laugh in the same language but still each laugh and smile…can mean so many things on each individual. Bong Star search is Good, I really love it and enjoy watching it. I have been watching it from the very 1st Bongo star search…its a worthy talent show that searches and seeks even the hidden talent, it encourages in the music industry and people who think are connected well to music…should for sure try Bongo Star search…Tanzania has major talented people who don not get chances…they lack opportunity but they are sooo able. This is one great example Rita that you have showed…Let it be bait for other shows of the same or different talents. I know you, You most likely know me…I just wanted to use ONLY my first name…but CONGRATULATIONS from my heart. R

 44. upendo mwamatandala, 04 January, 2011

  na nyie mliopata fursa hii ya kutoa maoni yenu tumieni lugha nzuri maana naona bado nanyi mna lugha sio za kuelimisha ila kuponda na chuki iliyojaa jueni kama ulivyokasirika wewe na kutoa lugha kali basi hata salama jabir ndio hivyo hivyo kwa hiyo jaribuni kutoa maoni kwa umakini

 45. upendo mwamatandala, 04 January, 2011

  mmi namuunga mkono Salama kwa sana tu ,kwa sababu lazima tupate vipaji vya ukweli kwa hiyo kipaji alichopewa Salama kusema ukweli kutoka moyoni mwake ingawa anatumia lugha za kukatisha tamaa kwa mshiriki kinasaidia katika kusukuma gurudumu la kusaka the winner of BSS, hivyo Salama kazia hapo hapo na ninavyokufahamu hutobadili mtazamo wako,ila mjitahidi kutoa washindi waliochaguliwa na wananchi sio kuchakachua matokeo kama ya 2009

 46. Kepha wa Ukweli…………..KIMARA, 15 February, 2011

  Hongera kwa kazi yako nzuri ya kulisaidia Taifa kwa kuwakomboa vijana ktk wimbi la umaskini endelea na moyo huo huo ila HAKIKA uu mzuri mama ila punguza naniliiiiiii.

Copyright © Bongo Celebrity