Jina la “Simba wa Vita” ndio jina ambalo watu wengi wamekuwa wakilitumia kumtambulisha mzee wetu Rashid Mfaume Kawawa (pichani). Huyu ni miongoni mwa viongozi wa mwanzo kabisa wa Tanzania ambao mpaka hivi leo bado,siku moja moja,huwa wanajumuika nasi katika matukio mbalimbali ya kitaifa.

Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza nchini Tanzania na baadaye kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.Alizaliwa mwaka 1926 katika kijiji cha Matepwende Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Tanzania. Alianza elimu ya Msingi huko Liwale -Lindi mnamo 19411942 na kuendelea na masomo ya sekondari katika shule ya Dar es Salaam Secondary School.

Simba huyu wa vita,katika kipindi chake cha uwajibikaji,alishika nafasi mbalimbali za ki-uongozi.Ukitaka kuzijua nafasi mbalimbali alizowahi kushika tafadhali bonyeza hapa kwa CV yake kamili.

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

Feedback / Comments

13 Responses to “FIRST PRIME MINISTER.”

  1. Comment by Edwin Ndaki on November 29th, 2007 3:03 am

    Labda mimi ndio ka historia ka chini ya mwembe kananipiga changa.

    Tarehe 9dec tunasherehea UHURU wa Tanganyika au Tanzania?Maana hakukuwa na Tanzania 1961.

    Leo hii hapa BC mmeandika waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania.Binafsi nakumbuka pia Mwl Nyerere(RIP) pia niliambiwa ndiye aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa nchi yetu.

    Hebu nitoeni TONGOTONGO maana wengine huku kwetu Tandaimba kupata habari sahihi ni kazi.

  2. Comment by Arktekt on November 29th, 2007 4:14 am

    Nilikuwa najua waziri mkuu wa kwanza Tanzania alikuwa Mwl Julius Nyerere kuanzia 1961 mpaka 1962 tulipopewa uhuru kamili?

  3. Comment by Dinah on November 29th, 2007 5:25 am

    Kwani muungano wa Tanganyika na Unguja bin Zanzibari ulikuwa lini?

    Kumbukumbu zangu za historia zinadai kuwa Waziri wa kwanza wa Tanganyika(kabla ya muungano) alikuwa Hayati Mwl JK Nyerere na Waziri wa kwanza wa Tanzania (baada ya muungano) alikuwa Rashidi Kawawa….au?

    Ninachokumbuka kuhusu Mzee Kawawa ni watu kutunga vichekesho tu kuhusu yeye……

    Mzee Rashidi Kawawa upo na utaendelea kuwepo kwenye historia ya Tz, kila la kheri ktk shughuli zako na maisha kwa ujumla.

  4. Comment by Kimori on November 29th, 2007 6:30 am

    Kweli miaka hiyo kulikuwa na mteremko…nimepitia hiyo CV haraka haraka…lo kama ingekuwa ndo sasa hivi hata ualimu wa shule za msingi asingepata!….mlikuwa na bahati sana!

  5. Comment by Ndoro on November 29th, 2007 7:22 am

    BC na Dinah wako right,Tanganyika na Tanzania vitu viwili tofauti,Kawawa ni first pm wa Tanzania,

  6. Comment by maya65 on November 30th, 2007 3:28 am

    Nini maana ya” SIMBA WA VITA”?
    nakumbuka akina generali Mayunga, Mti mkave na Kambare ndio waliokuwa makamanda wa vita vya kagera ,sasa kawawa ndio alikuwa mstari wa mbele katika kumtoa nduli Idd Amin? sasa nyerere ndio aliokuwa kinara wa vita ile na ndie alietangaza vita baada ya idd amin kutuvamia, nadhani ndie aliestaili kuitwa “SIMBA WA VITA” na sio Kawawa!!!!!!
    mnaonaje wadau? ni sawa na kumpa mtu cheo asichostaili!!!!

  7. Comment by maya65 on November 30th, 2007 3:29 am

    i mean Mti Mkavu

  8. Comment by changa on November 30th, 2007 9:41 am

    ETI ‘SIMBA WA VITA’! Vita gani? Operesheni vijiji(mwanzoni mwa miaka ya 70) ambako watu walikufa kwa kulazimishwa kuhama kwenye nyumba zao na kuhamia chini ya miti eti Kawawa kasema vijiji vya ujamaa? AU Vita ya kujilimbikizia mali hadi inchi kuishiwa hata dawa ya mswaki(miaka ya mwanzo ya 80)? Vita Tanzania/Uganda ilianza huyu mheshimiwa akiwa waziri wa ulinzi, kabla haijafika hata robo ya mapambano akatimuliwa kutoka wizara ya ulinzi!!!

  9. Comment by Arktekt on November 30th, 2007 12:55 pm

    Kawawa alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1962-1972 so anaqualify kama Waziri mkuu wa Tanganyika na Waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania.

  10. Comment by Arktekt on November 30th, 2007 12:57 pm

    Then akachaguliwa mwaka 1972-1977, kuanzia hapo Sokoine akachukua kiti.

  11. Comment by KABEWA on December 4th, 2007 3:52 am

    ka cv kangu ni mara 10 zaidi ya CV ya Kawawa lakini leo niko home tu sina dili

  12. Comment by Tahir on December 4th, 2007 12:26 pm

    Kuhusu “usimba wa vita” naona Kawawa anapakwa mafuta kwa nyuma ya chupa. Hana sifa hizo. Lakini nasikia ana udini kwasababu ama aliwahi kuwa na mke zaidi ya mmoja au mpaka sasa anao. au alikuwa na mtindo wa kuoa baadae anaacha? Hebu anaejua aweke hili wazi. Ni kweli Kawawa alikuwa mdini?

  13. Comment by rashid musalam ali on September 5th, 2008 1:15 pm

    in 1970s my uncle use to call me rashidi kawawa and i did’t knew what does it mean untill today i found that rashidi kawawa was a grate man and prime minister of tanzania

Leave a Reply