Ni ijumaa tena,ijumaa ya mwisho ya mwezi Novemba 2007.Mwaka unayoyoma,umri nao unazidi kupaa.Siku hazigandi kama alivyoimba Jide.Ni wakati mwingine wa burudani.Wiki inapoelekea ukingoni sharti uburudike kidogo.Maisha yenyewe mafupi haya.
Leo tunaye “Jabali la Muziki”,Marijani Rajabu na bendi aliyotamba nayo sana ya Orchestra Dar International.Wimbo unaitwa Zuwena. Hii ni mojawapo ya zile classic maarufu za Marijani na Dar International.Pata burudani.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Pichani ni “Jabali la Muziki” alipokuwa mdogo kabla hajaanza shughuli za muziki.Picha hii ni kwa hisani ya Issa Michuzi.
Wakati unaburudika na muziki,hebu soma kibwagizo kifuatacho ambacho msomaji wetu mmoja ametutumia.Endelea hapa ili ukisome kibwagizo chenyewe.Samahani kwa wale wasiotumia kiingereza.Ijumaa Njema.
A PhD graduate and an ordinary man went on a camping trip, set up their
tent and fell asleep. Some hours later, the ordinary man woke up his PhD
friend: ‘Look up at the sky and tell me what you see?’
The PhD man replies: ‘I see millions of stars.’ The ordinary man
asks: ‘What does that tell you?’
The PhD guy ponders for a minute: ‘Astronomically speaking, it tells me
that there are millions of galaxies and potentially billions of planets.
Astrologically, it tells me that Satan is in Leo. Time wise, it appears to
be approximately a quarter past three. Theologically, it’s evident the
Lord is all-powerful and we are small and insignificant. Meteorologically,
it seems we will have a beautiful day tomorrow. What does it tell you?’
The ordinary man is silent for a moment, and then speaks:
‘Practically. ……. Dr.; it tells me that someone has stolen our tent’.
MORAL OF THE STORY
Be educated in the right way and not go beyond the boundaries
Feedback / Comments
14 Responses to “ZUWENA-MARIJANI RAJABU NA DAR INTERNATIONAL”
Leave a Reply


sending...
nyie mnayuzingua tutafsirieni kwa kiswahili basi
Tafadhali, “Nalilia mtoto´´ na Dr. Remmy na Super Matimila!!!!!!!!!!!!!!1
aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah ..baaaaaab kubwa BC u imeianzisha vema kwa hicho KIBWAGIZO CHA pulu heveni dauni ****PhD***
Yaaaaaaaaaani Ijumaaaaaaaaaaa ipo palee paleee …
Hapo nakumbuka nasikiliza Radio Dume ilikuwa ikirindima miaka hiyo enzi za kina Domic Chilambo mwanza,Bahati Komba arusha n.k
Ukija kwenye wimbo jamani daima ukweli utabaki pale pale nyimbo za Marijani zilikuwa kali na bado zinatisha.
Achana na baadhi ya wasanii wa leo(SIO WOTE) amabo wao nikukurupuka tu na kuingia studio kisa kapata pesa ya kwenda studio.Wengine ni mashabiki basi tu wanafikiri nawao ni wasanii wanakuta watoa nyimbo ambazo zinakuja juu ka GESI ya soda soon inapotea inatulia ka TOGWA.
Cheki Zuwena hadi mr paul akaona bora arirudie,Jide akaona Siwema akaona alirudie.
Mola ipumzishe roho ya Jabari la muziki mahali pema peponi.Amina
Asante sana mzee maana imenikumbusha sana pale CBE kwa nyuma au usiku wa ijumaa live band Lions pale sinza….:)
We Nanal;
CBE kwa nyuma mlikuwa mkifanya nini? Mbona huelezei??
Stand by………..
Hee Miserere we acha tuu maana nikianza kuhadithia hapa ntamaliza mwakani it is a long story imebakia history mambo ya zilipendwa… si unajua ni vigumu kumsahau mpenzi wako wa zamani hasa pale…….. Usinikumbushe mie nikaaanza kulia..
Usilie Nanal usije ukaniliza na mimi.
BC endelea kukandamiza……. Mimi nauliza mzee kingunge kaenda wapi kwenye safu yeu hii??? samahani naona nimeenda nje ya maada…
Da! kaka hiyo ngoma haikufika mwisho lakini imenikumbusha mbali sana. Tuletee na Mzee Mwiluka pia next week kaka.
Link hii ina baadhi ya nyimbo zilipendwa
http://www.bongo5.com/content/blogcategory/118/203/lang,en/
upande wa kushoto wa page utaona menu uk-click “zilipendwa” unaweza kusikiliza nyimbo hizo
Haka kawimbo umekaiba wapi? Mbona hakajafika kunako kilele?
Ila kanagusa na kuchoma kumoyo……Dume zima lenye maringo na mikogo(sholilo/Bishoo) mikono kichwani huku analia…..nimecheka!
Lo! Kweli maisha ni safari. Hapa nilipo napambana na baridi mkoani Pennsylvania lakini sauti ya Bw. Rajabu limenikumbushia joto la Dar na utamu wa muziki wa KiTanzania. Sasa, ninafanya utafiti wa kumhusu Bw. Rajabu na hasa kuhusu wimbo wake wa “Masudi”. Je, kuna anayejua ni mwaka gani huu wimbo ulisikika kwa mara la kwanza mtaani?
a very fwantastic music.
SASA WEWE MCIHUZI NDANI YA BC MSIFANYE UZUSHI WA KUKATISHA MUSIC MKALI KAMA HUO AU NA NYINYI MSHA SAINI MIKATABA HEWA?
OK NEVER MIND TUWEKEE ULE MWIMBO WA MASUDI KAWA JAMBAZI MAANA HUO UJUMBE UTAMFIKIA KIJAN MMOJA PALE DAR MTAA WA KIZINGO YEYE HATAKI KAZI SHULE KAACHA YAANI TAFLANI TUU.NILIPOKUWA LIKIZO NYUMBANI TZA WAKATI NAJARIBU KUMUELEWESHA NINI MAANA YA ASIE SIKIA LA MKUU!AHMAD UKAWA UNAPIGWA HUO MWIMBO NIA NA MATUMAINI VIJANA TULEJEE KWENYE MAADILI TUNAYOAMBIWA
Na BC (Darwin Australia)