MCHUMI, PROF.IBRAHIM LIPUMBA

 

Ukiongelea wanasiasa wenye taaluma zinazoeleweka nchini Tanzania,sio ajabu mojawapo ya majina yako ya mwanzo mwanzo litakuwepo la Profesa Ibrahim H.Lipumba.(pichani). Lipumba ni Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama Cha Wananchi,CUF.

Alizaliwa tarehe 6 Juni mwaka 1952 katika kijiji cha Ilolangulu,wilaya ya Tabora Vijijini mkoani Tabora,Tanzania. Alianza elimu yake ya msingi (1959-1962) katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School huko Sikonge Tabora. Kuanzia mwaka 1962 mpaka 1966 alikuwa L.A Upper Primary School huko huko Sikonge,Tabora.

Baadaye aliendelea na masomo ya sekondari (1967-1970)-Tabora Boys Secondary School na baadaye (1971-1972) Pugu Secondary School. Mwaka 1973-1976 alikuwa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam ambapo alipata Shahada ya kwanza (BA Economics). Mwaka 1976-1978 alikuwa tena Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa ajili ya Shahada ya pili (MA Economics).Baadaye alielekea Stanford University nchini Marekani (1978-1983) alikosomea Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) kwenye masuala hay ohayo ya Uchumi.

Hii ndio inayomfanya Lipumba kuwa mmojawapo wa wachumi wanaoheshimika barani Afrika kama sio ulimwenguni. Kwa habari zaidi juu Profesa Ibrahim Lipumba na habari za uzoefu wake katika uongozi,nafasi za kazi alizowahi kushikilia,heshima za kitaaluma alizonazo, shughuli za kimataifa alizowahi kufanya nk bonyenza hapa. CV yake unaweza kuisoma kwa kubonyeza hapa.

Picha na Kassim Mbarouk.

Page 1 of 3 | Next page