Kwa miaka kadhaa kumekuwepo na majadiliano kuhusu mila,utamaduni na desturi za mwafrika au mtanzania kwa ujumla.Mpaka hivi leo mjadala bado unaendelea na wala hakuna dalili za kufikia makubaliano.Tafsiri au maana hasa ya mila,tamaduni na desturi za mwafrika inazidi kuwa uwanja mpana usioonekana kuwa na mwisho.Kila mmoja ana tafsiri yake hivi leo.Wote wapo sawa.Kila mtu kivyake,kwa raha zake wengine wanasema.Hata wewe msomaji una tafsiri yako binafsi juu ya suala hili.Usibishe.

 

Pamoja na uhuru huo wa kuchagua,kuwa na mtizamo tofauti,kuelewa unavyoelewa,kuamini unavyotaka kuamini nk lipo swali moja gumu au linaloekea kuwa gumu kupita yote ambalo bado linaulizwa mara kwa mara; Hivi mila,tamaduni na desturi za mtanzania ni zipi haswa?

Kama tulivyodokezea tu hapo juu, ukifuatilia popote pale,iwe ni mtandaoni,magazetini,vibarazani,vijiweni au hata kwenye nyumba za ibada,utakutana na jambo moja dhahiri,maswali ni mengi kuliko majibu.Wakati mwingine ngoma huwa droo.

Yote tisa,kumi ni kwamba watu wengi duniani wanakubaliana kwamba Afrika ndio kiini cha midundo mingi ya muziki (na pia mambo mengine mengi tu) ingawa wenzetu wa magharibi siku zote wamekuwa mabingwa wa kuiga na kisha kuingia chini ya uvungu wa kitanda kama vile wanacheza mchezo wa “tiyari bado” na kisha wakaibuka na kusema kwa sauti kubwa “Sisi Ndio Tumevumbua Hiki na Kile”.Wanaosema hivi huwa wako bize wakipindisha ukweli siku zote.Wanaingia na kutoka vichwani mwa watu kama vile wafanyavyo siafu wakimlinda malikia wao.

Kundi la AFRIKALI (pichani) lenye makao yake makuu jijini Dar-es-salaam lenyewe linajaribu kuthibitisha dhana hiyo ya “muziki asili yake wapi” kwa kupiga na kucheza muziki wenye asili ya kiafrika au kitanzania.Wanapenda pia kutumia vyombo vya muziki asilia kila inapowezekana.Muziki asilia ni upi huo?Swali zuri ambalo kama mengine kuhusu mila na desturi, majibu yapo lukuki. Ukipata nafasi ya kuwaona AFRIKALI(huwa wanafanya maonyesho yao sehemu mbalimbali nchini Tanzania na pia nje ya nchi),unaweza pia anza kupata baadhi ya majibu kuhusu uasilia wa muziki wa kitanzania.BC inawapongeza vijana hawa kwa ubunifu na umahiri katika kujaribu kutunza mila,tamaduni na desturi kupitia muziki.

Picha kwa hisani ya MichuziJR.

Feedback / Comments

7 Responses to “AFRIKALI”

  1. Comment by Pope on December 5th, 2007 2:16 am

    Unapoongelea utamaduni kwa upeo wangu mdogo ni:-
    Chakula, Mavazi, Lugha,Simulizi, Nyimbo, Ngoma, Muziki (sijui zinatofautiana), na vinginevyo.

    Kwangu mimi utamaduni wetu una adui wakubwa wawili.
    1. Utandawazi (Globalisation)

    2. International Media

    Utandawazi ndio unaua kila kitu ukiongeza na International Media ndio kabisa.

  2. Comment by Dinah on December 5th, 2007 5:39 am

    Mngepiga vibwaya ndio mngependeza zaidi….Big Up Afrikali.

  3. Comment by Mchunguzi on December 5th, 2007 7:39 am

    Khaa!
    Sasa huyo wanaem manua hivyo si watampasua Msamba jamani!?!
    Mweeh!

  4. Comment by philbert on December 6th, 2007 4:42 am

    unapoongelea utamaduni hili ni suala pana.hila kwa ufupi kwa mtazamo wangu mimi Utamaduni ni uhasilia. (asili )kwa nini nasema hivyo ni kwamba utamaduni hauwezi kufanana na daima hautafanana kwa sabababu kila watu wana asili zao za kikabila na kijiografia.kwa mfano ukisema ndani ya tanzania kila kabila lina utamaduni wake ambao unajifanana.utamaduni wa wahaya haufananni na wasukuma wala wazaramo na wachaga.wengine wanasema utamaduni wa pwani lakini wadigo, wamakonde na wandengereko hawafananishi utamaduni.ok ukienda east africa wakenya na waganda na watanzania hawafanani kiutamaduni.ukisema africa kwa ujumla kila nchi ina utamaduni ambao ndani yake bado kuna tamaduni tofauti.hata ulaya vile vile.sana sana ukitaka ku generalise utamaduni ni kuangalia vitu ambavyo kwa kiasi vinafanana miongoni mwa hayo makundi. lakini ni kila kundi lina utamaduni wake.

  5. Comment by bino on May 31st, 2008 11:40 pm

    ninavyjua kila mtu ana tafsiri yake ya utamaduni na huwezi mjudge mtu, wengine ngoma za asli, kuendeleza mila na lugha ya kiswahili hata ughaibuni.

  6. Comment by Gebo Arajiga on June 2nd, 2008 7:09 am

    Kwa kweli hili kundi hata mimi nalipenda sana kutokana na shoo zao kuwa nzuri huku kweli wakiwakilisha utamaduni halisi wa mtanzania halafu lingine ina wasichana warembo kwelikweli.

  7. Comment by FIDELIS FESTUS on July 30th, 2009 5:44 am

    Vijana wa leo mnajitahidi kudumisha mila ile wa2 walikwisha sahau hongereni sana.

Leave a Reply