Umaarufu au u-celebrity huja kwa njia nyingi.Sio lazima uwe mwanasiasa au mwanamuziki au mtangazaji au… ili kuukwaa u-celebrity. Ndio maana miaka ya nyuma lilipotokea shindano la kumtafuta mtu mwenye sura mbaya kuliko wote nchini Tanzania,watu walijitokeza kwa moyo mmoja.

Pichani aliyepo katikati ni jamaa anayeitwa Masudi ambaye ndio alishinda shindano la mtu mbaya kupita wote nchini Tanzania miaka hiyoooo. Hapo alikuwa amepozi na mashabiki wake ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja. Watu maarufu wengine walioshiriki shindano hilo walikuwa ni Dr.Remmy Ongala wa Matimila Orchestra Band na Mzee Jangala (yule muigizaji maarufu wa vipindi vya redioni enzi hizo).

Baada ya Masudi kuibuka mshindi Dr.Remmy Ongala alikata rufaa akidai jamaa kapendelewa kwani sio mbaya kumshinda yeye! Hatujui kama rekodi ya Masudi (ya kuwa mbaya kushinda wote) bado haijavunjwa au la kwani mashindano hayo hayakuwahi kurudiwa tena. Cha kufurahisha ni kwamba baada ya kupata ushindi wanawake kibao walianza kumzengea bwana Masudi wakitaka kuwa naye maishani.Hapo ndipo swali linapobakia; Kuna Binadamu Mbaya?

Picha hii ni kutoka katika picha za kumbukumbu muhimu za Muhidin Issa Michuzi.

Feedback / Comments

6 Responses to “KUNA BINADAMU MBAYA?”

  1. Comment by Kekue on December 8th, 2007 1:00 am

    Sasa hivi KIUME PESA sio sura.Tehe tehe

  2. Comment by Edwin Ndaki on December 8th, 2007 6:31 am

    aaah hivi hamja ona sura mbaya au mnatania..

    Yaani huyo akija kwenye familia yetu mbona tunamwona Handsome…

    Msela uso soft mtaaam tei sura sura mbaya..au hayo setelaiti dish(masikio)

    ndio yaliwazengua majaji?

    bora ushindi wangenipa mimi maana sura yangu nayo UTATA..

    jmosi njema MASUDI sura nzuri..

  3. Comment by Majita on December 8th, 2007 8:59 am

    BC nashukuru mmeona maoni yangu pale kwa Pro.Lipumba.
    Hebu jaribuni kuweka hii picha ya Masudi na waziri Karamagi Buzwangi ili wadau waone nani sura mbaya au Handsome zaidi ya mwenzake.
    Kwi

  4. Comment by TanzanianDream on December 8th, 2007 10:38 am

    A celebrity is a widely-recognized or famous person who commands a high degree of public and media attention. The word stems from the Latin verb “celebrere” but they may not become a celebrity unless public and mass media interest is piqued. For example Virgin Director Richard Branson was famous as a CEO, but he did not become a global celebrity until he attempted to circumnavigate the globe in a hot air balloon. Another example is Al Gore whose environmental crusade has elevated him to celebrity status. On the other hand, mass entertainment personalities such as soap opera actors or music stars are likely to become celebrities even if the person deliberately avoids media attention.

  5. Comment by Subira on December 8th, 2007 12:22 pm

    Hakuna binadamu mbaya, wewe ukimuona mbaya wengine wamuona mzuri, jamani tuache utani hakuna mzazi anayemuona mtoto wake aliyemzaa mbaya, watoto wote kwa mama zao wazuri. Huyu naye kwa mama yake ni mzuri na kwa ampendaye pia.

  6. Comment by amina on December 16th, 2007 2:50 pm

    Hahahahahahahahaaaa Masudi jamani alijinyakulia usuperstar,kaka iyo ndo sura ya kiume ila kidogo maskio ndo yamecharuka ila unavutia hahahahaaa

Leave a Reply