Ilipoanza mwaka 1964 ilijulikana kama NUTA Jazz.Baadaye wakaitwa JUWATA Jazz na kisha OTTU Jazz.Pamoja na yote hayo ukitaja jina Msondo Ngoma,kila mtu atakuelewa kwamba unaongelea ile bendi kongwe ya muziki nchini Tanzania.Haishangazi basi kusikia kwamba wanajulikana pia kama “Baba ya Muziki”.

Hivi sasa wanaitwa Msondo Ngoma Music Band. Leo hii ndani ya Landmark Hotel-Ubungo wanazindua albamu yao ya kwanza waliyoipa jina KICHEKO.Albamu ina nyimbo sita ambazo ni Maisha Mzunguko,Ndoa ya Manyanyaso,Majonzi Moyoni,Baba Gift na Mafao pamoja na wimbo uliobeba albamu wa Kicheko.Imeandaliwa ndani ya Metro Studio chini ya mpikaji Allan Mapigo.Uzinduzi umedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) chini ya mwamvuli wa kinywaji chake cha Safari Lager.

Kwa mujibu wa kiongozi wa bendi hiyo,Muhiddin Maalim Gurumo(mmoja wa waanzilishi wa bendi hiyo 1964) uzinduzi huo utasindikizwa na bendi ya Afigo kutoka Uganda ambayo pia ni bendi kongwe.Ilianzishwa 1974. Ukitaka kuburudika ipasavyo hivi leo,elekea Landmark Hotel.

Sasa kwa sababu leo ni ijumaa na kawaida ya utaratibu wetu ni kwamba tunawapa midundo kidogo. Nyimbo za leo ni kutoka kwa Msondo (aka Nuta,aka,Juwatta,aka Ottu,aka Msondo Ngoma Band.Sikiliza Binti Maringo(sikia sauti ya marehemu TX Moshi),Shukrani kwa Mjomba na Kuchacha Kubaya. Shukrani za pekee kwa Emmanuel Byuzura wa Kings Studio Disco Theque-London na Reading (UK) kwa miziki hii. Ijumaa Njema.

Binti Maringo

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Shukrani kwa Mjomba

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Kuchacha Kubaya

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Feedback / Comments

6 Responses to “KICHEKO-MSONDO NGOMA MUSIC BAND”

  1. Comment by Senyandumi on December 14th, 2007 1:03 am

    BC unajithibitishia kwamba wewe ni msondo poa!Lakini nyimbo ni za kutufurahisha.Hongera na mungu awe kwetu kwa wikiendi hii.Nitakuwa dar wiki hii nitakutafuta!

  2. Comment by Dj Emmanuel on December 14th, 2007 2:07 am

    Hapo mwenyewe nimekubali BC baba yao.Msondo ni bendi ya wakongwe na hizo sauti ulizotuwekea hapo ni za watukufu,Malenga na Mahiri wa sanaa hii ya muziki.Kwa wapenda muziki wa dansi hapo umezikonga nyoyo zetu.Hongera BC na mdumu haima

  3. Comment by Edwin Ndaki on December 14th, 2007 5:13 am

    Ijumaaa ipo paleeeeeeeeeeee paleeee.

    Yaani USISEME MSONDO sema SONDO yaaani jamaa hao ni balaa..shughuli yake waulize NGINDE au sikinde.

    Hapo bado ujagusa vitu kama TUMA,AJALI nk.

    Ijumaa njema…wale tunaoelekea TGI naomba kujua majina yao..mwambie FATUMA na ATIKA wa CBE club au Rose wa Mwl Nyerere memorial walete kama kawaida.

    Chwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap..

    KIITOSI

  4. Comment by Isoliwaya on December 14th, 2007 6:52 am

    Hizi nyimbo zimenigusa hasa, tafadhali wadau naomba mniwekee nyimbo iitwayo Selina piga konde Moyo! pamoja na Talaka ya hasira nadhani ni mlimani park waliipiga hii iliimbwa na muhidini gurumo pamoja na bitchuka

  5. Comment by sinzia on December 14th, 2007 12:07 pm

    BC naomba nirekebishe kuhusu nyimbo za leo
    Wimbo wa kuchacha kubaya nakumbuka jina lake hasa ni FAULATA,na wimbo shukrani kwa mjomba si wa msondo kama ulivyosema…ni mali ya band ya OSS wana NDEKULE…wakati ule Mzee Gurumo na Bitchuka walikuwa kule.
    Tunashukuru kwa kutupa nyimbo hizi kwani zinatukumbusha mbali sana.
    WKND NJEMA

  6. Comment by DUNDA GALDEN on April 3rd, 2008 6:59 am

    MARADHI YA NYUMBANI HAYO
    AHHHHHHHH ILIKUWA KINONDONI KUNA BINT MMOJA ALIIKANGA NAFSI YANGU WE ACHAAA SIKUMSIKIA HATA NANI LAKINI YOTE MAISHA AHSANTE KAKA SAID NIMEAMINI MPENDE AKUPENDAE NINAKUMBUKA SANAAA AMANI KWA WOTE UKO BONGO HASWA JIJINI KWETU BANDARI SALAMA
    DUH WE ACHA TUUU MJOMBA MUHIDIN UNASALIMIWA HAPA AUSTRALIA NA MKWEO ANAKUPA ONGERA SANA
    NA chafosa chai goda(KAPTEN KORICHI SOKO JIPYA)

Leave a Reply