NANI AMESAHAU?

 

Mwaka ndio unayoyoma hivyo.Kama ulijiwekea malengo mwaka huu ulipoanza,basi wakati wa kutafakari jinsi gani uliyafikia au hukuyafikia ndio ushawadia. Kama hukufikia malengo fulani usikate tama.Jipange upya.Tizama mbele na sio nyuma.

Kama tulivyosema, mwaka unapoelekea ukingoni BC inapenda kukumbusha kumbusha kwa chati matukio muhimu muhimu katika ulimwengu wa celebrities wetu ya mwaka 2007. Nani ambaye hakupata habari za “mrembo asiye na nywele au mwenye kipara”? Flaviana Matata(pichani) alipoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya Miss Universe huko Mexico City mwezi Mei mwaka huu, aliacha gumzo na kuwa “balozi” mzuri wa Tanzania.

Mahojiano yetu na Flaviana mara baada ya uwakilishi ule unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

Page 1 of 3 | Next page