Baraza la Kimataifa la Usafiri wa anga limemteua mtanzania Omari Nundu (pichani) ambae ni mtaalam wa masuala ya anga kuwa Rais wa tume yake ya ufundi inayoundwa na magwiji wa fani hiyo duniani. Bwana Nundu ataiongoza tume hiyo kwa mwaka 2008 na anakuwa ni mwafrika wa kwanza kushikilia wadhifa huo mkubwa katika duru za anga duniani.
Tume hiyo ndio chanzo kikuu cha sheria, hatua na viwango vya kufuatwa katika utengenezaji wa ndege, viwanja na vifaa vya kuongozea ndege na pia ndio inayotuinga na kusimamia sheria za usafiri wa anga duniani.
Nundu ni mzaliwa wa Tanga na safari yake ya Urais wa tume hiyo ya magwiji wa anga ilianza mnamo mwaka wa 2005 wakati nafasi ya wajumbe (makamishna) zilipoongezwa kutoka 15 hadi 19 ambapo Tanzania ilimteua Bwana Nundu kugombea nafasi hiyo iliyogombewa na nchi tisa na kuibuka na ushindi mkali dhidi ya mataifa mengine. Alianza kutumikia nafasi hiyo mwaka huo huo na makamishna wenzake wakamchagua kuwa Makamu wa Rais wa tume hiyo mwaka huu.
Bwana Nundu anakuwa pia ni rais wa kwanza kuchaguliwa akitokea katika nafasi ya Umakamu wa Rais.
Tume hiyo inaundwa na wataalam wa hali ya juu duniani katika fani ya usafiri wa anga na kila kamishna huchaguliwa kwa vigezo vya umahiri na mchango wake mkubwa aliowahi kutoa katika fani hiyo duniani na kila kipindi huwa na waombaji wengi kuliko nafasi ambapo makamishna hao huishia kuteuliwa kwa ushindani mkali wa kura.
Habari hii na picha imeletwa kwenu kwa hisani ya Saidi Yakubu,London.
Feedback / Comments
20 Responses to “MTANZANIA KUONGOZA TUME YA ANGA DUNIANI”
Leave a Reply


sending...
Samahani Sijaelewa vizuri.Huyu ni mmoja wao kati ya wanaojulikana humu kwenye blogs kama wabeba maboksi????
Simply Congrats….Do wat u best at…….
Hongera sana bro.najua ungekuwa umeshinda BBA hapa tungeona mapongezi kibao.
Inapendeza unazidi kuwatumia ujumbe hao wabaguzi kuwa black bongo zao zipo juu..ni wanasiasa tu ndio zipo ndivyo sivyo
Majita sasa unaboa.Hapa BC hamna hizo habari za wabeba mabox.Mpe hongera yake Nundu.Wivu tu.Hongera Omari Nundu.All the best.
Watanzania wengi walioko huko nyumbani wanafikiri kuwa mtu yeyote aliyeko ughaibuni ni mbeba mabox.Sasa bwana Jumanne nimeandika hivyo nikafikiri na wewe somo la fasihi ulifaulu,kumbe laa.
Huo ni uthibitisho wa waishio ughaibuni wanafanya nini.Siyo kuwa na akili mgando tuu za kufikiria maboksi japo mimi ni mpiga boksi mashuhuri hapa boston
Kama humu kwenye BC hakuna maboksi nenda hapo juu kwenye picha ya wiki usome maoni.J4 humu inaonekana ni mgeni eeh,karibu.By the way nimesema humu kwenye blogs,sasa kama BC ni blogs au siyo blogs utajiju.
Heheh mwanaume anasema Utajiju!!!!
Tena ni mwanamme wa wanaume wa TMK…..Juma Nature na wsimbo wake…”Utajiju..”remember?????
Oooh !hivi mwanamke ndo anaanza kuandika kwa kusema heheh au nimekosea??
Majita
Kweli hapo kazi kama Juma Nature ndo idol wako sio ajabu unaongea hivyo….Mungu ibariki Tanzania usitukomboe kutoka Umaskini kuna mengi zaidi hapa…..
wewe tanzaniadream ulitaka idol wa majita awe nani. Karamagi au richa.It seems u like being in control eeh!are you one of the big upper crust mother f****r executives eeh! Go Majita.Nakupa shavu Majita.Kumbe wewe ni mwanamme halisi.Tanzaniadreams favourite yake ni taarabu.Bullshit!
Hapa ni Hongera tu Mr. NUNDU!!!! I wish ningekuwa ndo mimi tehe tehe!!
Afadhali Mr. Nundu umewaonesha hao white people kwamba watz sio wakuchezea maana wanatuona kama hatuwezi, many congraturations sio wakina nanihiiii kila siku wanakuwa wasindikizaji tu.
Kekuu hi!!!!!!
Heri niumwe na mbu JKNI Aiport nikisubiri kumlaki huyu Guru kuliko Richard wa BBA. Maana huenda kuna siku huyu anaweza kubadili sera na taratibu ambazo indirectly zitakuwa na athari chanya katika viwanja vyetu vya ndege na hata usafiri wa ndege zetu Tanzania ambapo nami nitafaidi.
Hivi ndivyo unawezaona jinsi ambavyo umma na vyombo vya habari vinavyoweka vipaumbele vyao. Yaani Mshindi wa kutongozwa, kuvua na kuchokonoa anapata fulu kavareji na gumzo kila sehemu; Mshindi wa dunia katika kutambuliwa mchango na taaluma yake nyeti kavaleji na komentiz kiduchu!!!
NA MUNGU HAKOSEI, NCHI INAPOWEKA KIPAUMBELE NDIPO NAYE ‘ANAWABARIKI’ HAPO ZAIDI.
Nundu-Hongera sana.
Mkataissue
Mkata issue hata mm wakisema kuna mapokezi for sure i’ll go na hili jua linalowaka no prob.nitachukua mwamvuli!!! Tushtuane basi.
Wewe Matty, mbona unamajungu na white people? To be honest I don’t think they even care! Best man for the job! Congrats bro
Mkata, nitajiunga na wewe kungatwa mbu!
Poa keukeu, nitakutonya. Lakini nawe ukisikia mapema usisahau kunishtua. Halafu natamani hafla ya kumpongeza badala ya kuwa ngoma na misosi iwe ni kongamano litakalo wahusisha jamii ya wasomi na wasio Wasomi. Na yeye pamoja na magwiji wengine Watanzania katika nyanja ya usafiri wa maji na usafiri wa nchi kavu ndio wawe wachokoza mada! Kisha Watendaji wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Anga, Maji na Barabara nchini Tanzania watueleze ni mikakati gani waliyonayo ya muda mfupi na mrefu kuhakikisha kuwa Mtanzania anasafiri salama na kwa huduma ya kuridhisha.
Du ! hapo niko tayari kutembeza mic ukumbini na kugawa vipeperushi bila malipo!!
Baba Koku hujaona hata pale kiwanda cha urafiki wazawa wanaonekana hawawezi (kwa kupewa low sarary) na white ppl wanapewa kitu kinono hata kama hawajasoma, sasa what is the problem au wewe ni white ppl?
Hee Makubwa!!! Baba Koku tafadhali sina majungu nasema ukweli tumeshaona white race kibao wanajidai wao ndo wanajua kila kitu lakini kumbe hata sie tunaweza, what is Majungu baba Koku?????????kwanza ulikuwa wapi?mbona sijakusikia siku nyingi au ndo maandalizi ya x-mas, id na new year tualikane.
Wishing you all the best, peace and joy within these holidays.
Hongera sana sana bwana Nundu! Nafurahi sana nikiona watu wetu wanangara ulinguni.
I kew it was just a matter of when and never if. Hongera sana bwana Nundu. Umeweka mfano ambao wengi wetu inabidi tujifunze na kuufuata. Wa-Tanzania wenyako tuko nawe na tunakutakia kila la heri.
Asante Rita Kwa kunijibia Wishing you all a merry x-mas and happy new year.