
Picha moja ni sawa na maneno elfu moja.Huo ndio msemo au imani ambayo ilifanya BC ianzishe utaratibu huu wa “picha ya wiki”. Picha ya wiki hii ni kama unavyoiona hapo juu.Picha inamuonyesha mama akivuka mto Lufilyo uliopo Kyela mkoani Mbeya kwa kutumia daraja la kuning’inia maarufu kama “kiteputepu”.Picha hii ni kielelezo cha jinsi maisha ya baadhi ya watanzania(walio wengi) yalivyo.Hii ndio picha yetu ya wiki hii.Tafakari.
Picha hii ambayo BC imeletewa na Maggid Mjengwa ni kwa hisani ya Mbunge wa Kyela.
Feedback / Comments
40 Responses to “PICHA YA WIKI #14”
Leave a Reply


sending...
HERI KUWA MBEBA BOX KWA KUTUMIA FOKU-LIFTI NA GLOVUSI KATIKA LAMI KWA MATUMAINI YA KUPATA UJIRA MZURI KULIKO KUWA MBEBA FURUSHI LAKO MWENYEWE ZITO JUU YA KICHWA CHAKO UKITEMBEA NDANI YA MAJI MACHAFU YENYE WANYAMA NA WADUDU USIOWAJUA NA KWA HOFU NA MATUMAINI YASIYOTABIRIKA KAMA UTAFIKA UENDAKO AU UTACHUKULIWA NA MAWIMBI YA MAJI!
jamani kweli ni hatari sana. watu mwengine wanapata tabu sana yaani ninamuonea huruma na huo mzingo mzito kichwani ukimponyoka ndiyo basi tena.
Kwa kweli hili si jambo la kusema eti ni bora kubeba mabox ulaya kuliko kuishi tanzania, ni bora sisi watanzania wote tuishio nje na wale walio nyumbani kukaa chini na kutafakali jinsi ya kupiga vita umaskini katika nchi yetu…kwa kweli hii picha ya huyu mama inanisikitisha sana , humo kwenye maji kuna wadudu waletao magonjwa ,vile vile kuna wanyama kama mamba, nyoka nk na hilo darala likikatika tu basi huyo mama na hilo daraja wote watazolewa na maji….mhhh hii ndio inadhihirisha kuwa Bongo siku hizi maisha tambalare????..10% ya watanzania wanaishi kwenye majumba ya starehe na kuendesha magari ya kifahari wakati 90% wanaishi maisha ya namna hiyo picha inavyojieleza?????
tulio nje tusisahau nyumbani ni nyumbani tu tujitahidi kufanya kazi kwa bidii na kuondoa aibu hii ya umaskini wa kupindukia…..
mungu ibariki Tanzania
Pole sana mama yangu hapo kwenye maji.Najua huwezi pataa nafasi ya kuyasoma maoni yangu au hata kuyatazama kama sisi tunavyokutazama kwenye hiyo picha.
Najua miaka 46 baada ya uhuru na kura yako uliyoitumia kuchagua viongozi ili japo wakukumbuke kwa kujengea hilo daraja wamekusahau.
Naamini rais wako angehahirisha safari ya wiki hii kwenda USA kupokea TUZO ya kufanikiwa kupunguza umaskini hiyo pesa ingetosha kabisa kujenga daraja la muda.
Nani atakukumbuka mama leo,wanaishi kwenye MAHEKALU,wenyewe daraja la Ruvu likipata hitilafu kidogo tu serikali nzima inaamia pale.
Lakini wewe Mbunge wako anakupiga picha na kwenda bungeni kupiga makofi na kuhalalisha ubadhilifu uendelee bongo.
Kwa niaba ya watanzania wenzangu woote tunaoishi chini ya mstari wa umaskini,tusikate tamaa…
Ipo siku historia itawahukumu hawa vibaraka wa wazungu.Poleni sana tupo pamoJAH.
Mama Pole sana.Shida kama hizi ziko Majita.I wish Mama KIKWETE angekuja kupita hapo na Matenge yake.BC kwa nini hapo usiweke kichwa kisemacho “AMENDEZA AMA HAJAPENDEZA?” ili tujadili.Niwasikie kina Abdallah,matty,loly na wenzao wanaojiita wa kariakoo wangesemaje.
Huyo mama Kuanzia furushi hadi kwenye kandambili zake gharama yake labda ni nusu ya gharama ya enjofesi ya Salma kikwete.Kibaya eti bado anatoa kodi.
Hiviiiiiiiiiiiiiii!!Msunyo
Majita
ilove u and ua coment majitaaaaaaaaaaaaaa
Maisha bora kwa kila mtanzania!
Viongozi wetu jamani jaribuni angalau kuwa na utu japo kidogo…Inauma sana kwa kweli kuona mama huyu na watu wote wanaoilitumia hili ‘daraja’ wanahatarisha maisha yao namna hii kwa vile tu eti viongozi wanatembea na mashangingi na hawana muda wa kutatua matatizo madogo kama haya!
Hilo daraja ni mtu tu kajitolea kulitengeneza kwa nguvu zake na si ajabu huyo mama katozwa hela ili aweze kupita wakati kila ndege inayoruka ikielekea ughaibuni imembeba rais wa huyu mama!
Kama mtu binafsi tu ambaye wala hana elimu ya uhandisi anaweza kutafuta ufumbuzi wa kivuko kama hiki, hivi gharama ya shangingi moja haiwezi kweli kuweka kivuko kinachoeleweka?
Wakati umefika sasa kwa watanzania kuamka ila bahati mbaya sana ninayoiona ni kuwa hapa kwenye mtandao watu wengi wanaosoma na kutoa maoni wanaishi ughaibuni na ukiwa bongo wala watu hawajui kuwa kuna sehemu kama hizi.
Watu wachache sana wanaoweza kusoma habari kama hizi maana wengi siku nzima wanahangaika ili mkono uende kinywani kwa hiyo hawawezi kupata muda wa kusoma habari kama hizi maana kwanza hata uwezo hawana!….Magazeti tu ni shida kusoma. Mungu ibariki Tanzania ila kuna siku nina hakika haya mambo yatafikia mwisho!
Hii picha inawakilisha safari ya Tanzania na watanzania wote. Itaendelea mpaka watu wachoke na watake mabadiliko. Kwani hakuna mtu anaumia kwa kuona hii picha? Sio lazima awe ndugu yako au mama yako. Tutafute ufumbuzi wa haya matatizo nyumbani. Unajua wengi watanzania wakipata uwezo wanasahau kama jirani yako hanashida au sio shida yako. Na hii ndio uwezo wa kufiria wa viongozi waliomadarakani na hao waliopita. Inakua ngumu sana mimi kuaona tofauti ya viongozi waliopita na wasasa ila ni majina tu. Tutafute solutions jamani, tunauwa watu kila sekunde na tunaweza kuzuia mengi. Kuna maswala mengi yanapitia kila familia na kila mtu yanamtokea, kwani hatuumiii.
Hivi hao wabunge na wafanyakazi serikalini wa tanzania kwa nini wasitumie magari ya aina ya toyota corolla ambayo hayatumii mafuta mengi na spea zake ni rahisi???? badala yake fedha zinazotumika kununulia na kuyafanyia service hayo mashangingi zikatumika kupiga vita umaskini na kuondoa fedheha kama picha hiyo hapo juu ?????
majumba ya kifahari, magari ya gharama, kujirusha kwa sana,mitungi kwenda mbele ……lakini mhhh hiyo Tanzania mimi na wasiwasi nayo!!!!!
Mungu wangu!!!!!!!!!!!
Hivi kodi zetu wananchi zinaenda wapi?au ni kupeleka wakwe hija na kufanya starehe – Magari na nyumba za kifahari?Hata sisi walipa kodi kipata japo huo mkopo tu ni hadi Yesu Arudi.Kila siku tunapewa misaada kibao lakini sijui pesa hizo zinatumikaje!Kwakweli hali ni mbaya sana Tanzania,tutaishi hivi hadi lini???? Mwenyezi Mungu kisikie kilio chetu sisi wanyonge!! Kweli hata huyo mbunge hajisiki dhamira ikimshtaki?Picha kama hizi zinatakiwa ziende direct kwa rais au hata mkewe tuone reaction yake itakuwaje.
Ni kweli jamani inasikitisha, serikali yetu kazi ni kuboresha maisha ya viongozi wake wala hawamuangalii mwanainchi wa kawaida ambaye anawpigia kura hao wavimba matumbo!!
Mi nafikiri siku moja tugome wanainchi wote wa kawaida kuigomea serikali, mbona wahindi wakitunyanyasa kwenye makampuni yao tunawagomea, kwa nini tusiigomee na hii serikali yetu ili angalau iboreshe huduma muhimu kama hii ya daraja.
Jamani hima watanzania tugome ili kuishinikiza serikali kuboresha huduma muhimu.
Huo ni mtazamo wangu mimi!!
Pole mama yangu, najua toka uzaliwe mpaka umri huo hujawahi furahia chochote kizuri cha nchi yako. Hapo ni kwa upande wa miundo mbinu tukija kwenye afya na elimu we acha tuu nataka kudondosha chozi.
Mimi nafikiri wakati umefika wa sisi wenyewe wananchi kujikwamua kutoka kwenye hizi karaha, mfano mzuri ni wanaichi wa kagera waliamua kuandaa siku ya KAGERA DAy ili kuchangia maendeleo ya mkoa wao, Huwezi amini hela zilizochangwa siku hiyo mi mwenyewe nilishangaa sana. Hivyo basi tukiwa na utaratibu kama huu tunaweza kukusanya hela kidogokidogo na kutatua matatizo ya daraja kama hili.
Jamani tupende tulipotoka, wanyakyusa wote mkijitahidi hili daraja mbona litakuwa bomba badala ya kubaki na kumpigia kelele mbuzi(serikali)mana haelewi kama tunashida.
Mbona Mkapa alikomaa na kujenga Daraja la Rufiji!! hivyo huyo mbunge wa huko awe mstari wa mbele kuhamasisha wenzake wa huko kuleta maendeleo, Jamani mbona kwenye maharusi tunachangia!! au sisi watanzania ni vichwa vya wendawazimu tunachangia harusi na upuuzi mwingine na kuacha vitu muhimu kama hili daraja analopita huyu mama.
inasikitisha sana jamani Mungu atusaidie jamani!lakini ni wanjibu wa serikali kupitia hao MP mimi sifikirii kama mama salma pekeyake ataweza ni vijiji au wilaya, kata nahata vitongoji vingapi vina shida kama hiyo du!!!!!!hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania?????
Kweli BONGO TAMBARARE!!
si Maisha bora ni BORA MAISHA!!! Kwa design hii,hatutafika!!
Huyo Mbunge wa Kyela alipita hapo huku amejifunga kanga na picha yake ilitoka gazetini akiwa anavuka hapo, naona alivyokwisha vuka ndio akapiga picha ya wanaofuatia nyuma yake.
Hivi kulikuwa na umuhimu wa kujengwa uwanja wa NDEGE WA KIMATAIFA SONGWE badala ya angalau kuwajengea wananchi miundombinu ya kuweza kutatua matatizo yao?
Nani anafaidika na huo uwanja wa kimataifa uliojengwa huko Mbeya? Na wana Mbeya wenye nafasi ya kulobby kwa nini waliloby wakapata kujengewa Uwanja wa ndege wa Kimataifa Songwe wakati wanashindwa kuloby miradi ya kujenga madaraja ya kuweza kupita watu kama hapo juu. Hapo wala hapahitaji gharama kubwa kama kujenga hata uwanja wa ndege wa kawaida sembuse wa kimataifa.
Ni nani awajibike kwa hili maana ukisema Serikali, serikali ni nani hasa? Kwa sababu nijuavyo serikali si Rais wa nchi peke yake.
Jamani mchakato wa kujenga daraja la Rufiji ulianza muda mrefu enzi ya awamu ya pili ya uongozi na funds zilitafutwa enzi hiyo ya Mzee Ali Hassan Mwinyi (Kuwait Fund). Kazi ya kujenga ilianza rasmi mwaka 1996 – 1997 ambako nguzo za daraja zilianza kuonekana. Mhe. Mkapa alipoingia alikazania na kuhakikisha kuwa hilo daraja linamalizika. Lakini ilichukua muda daraja limeanza kutumika rasmi mwaka 2004. Ila Mkapa alionyesha jitihada kubwa kuhakikisha kuwa watu wakusini hawalali Nyamwage kusubiri MV Rufiji iwavushe. Ni muhimu watu kujali kwao sio kujali maslahi yao, nianavyo mimi kama uwanja wa kimataifa wa Songwe unasaidia katika kuongeza pato la nchi basi pato hilo litumike kujenga madaraja (sio hili peke yake) katika Mkoa wa Mbeya na kuboresha miundombinu katika huo mkoa.
Mbona kule alikotoka ni kama msituni alitoka shamba au? Da namna hii ni hatari, haya jamani wana BC wote na mama unayevuka hapo nawatakia Idd, X-mass na Mwaka mpya wenye furaha tele!!! Naenda Moshi kuhesabiwa c mnajua zetu? Manka vipi unaondoka lini?
sikujua hapo ni tz nilijua nchi nyingine,duuuu serikali saidieni hali mbaya,punguzeni matumizi yasio na lzm saidieni wananchi.
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake, maana kama tutaanza kuonyesha barabara za vijiji vyetu hapa patakuwa hapatoshi.I love my country Tanzania.
CHAGUA JIBU SAHIHI THEN MTUMIE MCHUMBA WAKO
1)Ipi sahihi (a) Maisha bora kwa kila Mtanzania
(b) Maisha bora kwa WANA-MTANDAO
2) Ipi ni kweli?
(i) Miaka 46 ya uhuru
(ii) Miaka 46 toka waondoke wazungu?
3) Miaka 2 ya kikwete yenye dira au yenyekupoteza matumaini ya kuvuka hata kadaraja kadogo kama hako
Kwa ufupi kazi ipo, vijana wenzangu badala ya kukaa kwenye net nakutafuta website za ngono, Model na ubishoo mwingine, tutumie website kama hizi kujifunza na kujua mambo mengi zaidi ili siku wakati wetu ukifika tujue makosa yalipoanzia, lini yalianza, nani aliyaleta na nani aliyaongeza zaidi.
Tanzania sehem zenye shida kama hizo ni nyingi sana na kama wadau kama wenye site kama hizi badala ya kutuwekea kila siku picha na mahojiano ya warembo na wasanii wa bongo fleva, tusaidieni ili hata huko vijijini wawe “Bongo celebrities” kama na nyie chombo cha habari kama hiki mtawatenga wananchi, basi mtakua mmekomelea msumari.
“”Mapinduzi sitayaleta mimi, bali mtayaleta nyinyi wenyewe wananchi” (Cheguevara)
Hivi watanzania tutakuwa wajinga hadi lini? Mwaka 2010 tutakwenda tena luwapa kura hawa wauaji wa CCM inasikitisha. Lini tutachoshwa na wanyonyaji na kuwatimua kuanzia ikulu mpaka kwenye halmashauri za wilaya? Hima jamani hawa watu WMEIBA MPAKA KIPOFU AMEONA.
KWA SISI WA ULAYA TUKIONA HIVI TUNAONA URUMA SANA,LAKINI KWA WALIO BONGO NI MAISHA YA KAWAIDA.MUNGU ANGENISAIDIA NIMJUE HUYU MAMA NIKO TAYARI KUMTUMIA EURO 100 KILA MWEZI,BC TOA IMFORMATION ZA KUMPATA HUYU MAMA KWANI AMENIGUSA SANA MOYO.
Kama kawaida hatuishi kulalama na kuhukumu wenzetu. Naomba niwaulize:
1. Hivi Kikwetu ndie anayetakiwa kufanya kila kitu TZ?
2. Mama Salma kuvaa imekuwa dhambi?
3. Kwani huyu Kikwetu ametawala miaka mingapi? Wenzie walifanya nini?
4.Mbeya tena Kyela kuna matajiri wangapi? Wameifanyia nini jamii yao? au Kazi kuogopa kulogwa na kuvaa suruali mitundiko mjini na kujirusha?
Acheni hizo! Nawaomba sana muige mfano wa wachagga. Hakuna cha serikali wala nini lakini mambo ni mswano ile mbaya.
1. Kila watu wawajibike walikotoka. Sasa ikiwa hata kurudi home ni shida unategemea nani hata amkemee huyu Mbunge? Huyu mama anaelewa haki zake? Pengine hata shule hakwenda!
2. Tujenge nyumbani jamani na tuende kutembelea huko mara kwa mara ili kurekebisha mambo. Usione Wachagga na X-mass mambo mengi sana yanaenda kurekebishwa huku ikiwa ni pamoja na:
- Kusherehekea kukutano wanafamilia pamoja
- Kuchangia ukuta wa kanisa/Msikiti uliopasuka kwa mvua za masiki
- Kuchangia barabara iliyoharibiwa na masika (kama hukwenda X-mass lazima utume mchango bwana)
- Kuchangia madaraja yaliyobomolewa na mafuriko kwa kushirikiana kijiji hadi kijiji
- Taarifa za ndoa nzee
- Taarifa za ndoa tarajiwa
- kuandikisha watoto waliozaliwa
- kukutanisha wageni na wanafamilia kwa ujumla
- kupangiana mikakati ya kutunza wazee na kuchangia wanafunzi waliopo shule kulingana na mahitaji
Sasa nawauliza ndugu zangu wa Kyela mnafanya kitu gani huko home hadi huyu mama anaishi Jehanamu angali duniani?
Tuamke waTZ! Hata Marekani kila Jimbo linajitegemea Rais anapewa Taarifa tuu. Sasa nyie mnataka Kikwete na Salma aende kujenga daraja la Kijiji Kyela? Acheni ujinga na tuanze kufanya kazi. Je mara ya mwisho kwenda Kyela ilikuwa lini? Je ni hili tatizo tu liko huko au yapo na mengine? Mimi naamini umaskini mkubwa unachangiwa na namna na fikra zetu katika jamii. Jamii ya KiTZ haiko tayari kuutokomeza umaskini “INATAKA ETI RAIS NA MKEWE PEKE YAO WAKATOKOMEZE UMASKINI” Ujinga mtupu. Jikusanyeni muone kama mambo hayatabadilika, mbona sisi tumeweza bwana kwanini nyie mshindwe? Weka system in place halafu uone mote wa gesi ulivyo mkali. Maana hata huyu Mbunge anapeta tuu kwani hana hata mtu wa kumkemea. Angekuwa Moshi subutu yake angeonja joto ya jiwe hata gari isingepita home kwake ingekuwa mzagazaga.
Mbunge na watendaji wote wa hiyo sehemu wanahitaji kuwajibishwa maana hawaitendei haki jamii wala Rais kwa ujumla na wengineo wanaomfanania! Na mwisho nyio waathirika nanyi kuna hisa yenu kubwa tu isiyopungua asilimia 70% maana nyie hamtaki kuwa chachu ya maendeleo kwenye jamii zenu.
Hapa nalia sana maana nimepatwa uchungu sana moyoni kuhusu hii picha na sijawahi kuona au kuwaza umaskini katika hali hii maishani mwangu! JAMANI HARAMBEE IFANYWE ILI KUOKOA HII JAMII.
We mama wa Kichaga. Ni KIKWETE siyo KIKWETU
Hayo ndo matunda ya kura yako,
ONYO
“”Mama wa Kichagga”" nimekusamehe ila ukirudia ntakutukana mbele ya watu tusi ambalo lita-waaffect wote watakao kua karibu na wewe
Inaonekana hujui kazi za serikali (rais) ni zipi..
Tena na ujaribu kua na moyo wa huruma kwetu sisi ambao tumezaliwa kwenye shida na tunajua nini maana ya shida.
“”Uzalendo ni uungwana”"
Wananchi wanafanya kazi na hakuna motivation yoyote, nenda Tanga kaone matunda yanavyoozea mashambani, nenda Shinyanga ukaone wakulima wa Pamba wanavyo-nyanyaswa
Huyo unaemuita Kikwetu na Salima kazi yao katika kuondoa umasikini ni ku-facilitate economic activities na sio kwenda Marekani kuona Boys 2 Men.
“”Serikali ni nzuri ikiegemea upande wako”" 2pac Shakur
kwa upande wa Tanzania serikali imeegemea kwenu Mabeberu imetusahau sisi masikini unafikiri tumdai nani??
Tunaomba mtuhurumie jamani kama na nyie mnatutupa, basi ngoja labda tuanze kusubiri kale ka-bwana (Yesu) hadi katakapo rudi,, maana kalisema “”Nyie mabeberu na madalali wa Nchi, hamtauona ufalme wa mbinguni”"
Sawa Mama wa kichaga umetuonesha mfano wa wachaga walivyo kama ni hivyo basi kila mtu asifie kabila laike na mimi nawapongeza wahaya kwa kuchangia bil 4. on the spot du!!!!sijui yule prof nanihii alishikwa na mafua ghafla akasema mtu aende USA akachukue mil 40 na wengine sijui wamechelewa airport watatuma kesho….heeeeeee!!!! ni nyingi lakini wakikabidhiwa mafisadi wetu wapendwa sijui kama zitafika kule vijijini maana ndo wataanza kununua mavx kila mtoto na lake, imagine MP anajenga airport + good runway kwaajili yake akiwa anaenda kutembelea mkoa wake na si barabara na madaraja hivi anaakili kweli huyu???
Naomba Desert eagle nikusahihishe usimkashifu mtume wa Mungu kwa kumuita kafulani pls hata mimi siwezi kumkashifu mtume Moh’d.
Hapana ndugu yangu wala sijamkashfu bwana yesu,, asiri yangu ni kanda ya ziwa mtu mzuri tukiwa tunamsifia hua tunaanza na Ka- kwa kfano ka-Nyerere, ka-kikwete au
ka-jumanature, ka-website ka-bongocelebrity n.k
Kwa upande mwingine mtu akiwa hapendwi au ukitaka kumkashfu mtu sisi hua tunaanza na Li-
kwa mfano Li-Mama la kichaga,
Li-maximo, Li-wewe n.k
Samahani kama sikuyaweka haya bayana wala sikua na lengo la kumkashfu bwana yesu
kwakweli daraja hili sijawahi kuliona huku ukerewe………………. na laiti kama lingekua lnatumiwa na viongozi basi lingekua zuri tu lkn hawana wajualo wao watoto wao waku huku ukerewe na wao wenyewe wamebaki kwenye majumba mazuri kazi iko ka wananchi siku moja kwenye uchaguzi gomeni kupiga kura mpaka wajenge madaraja yote na kuongeza kuenga mashule ili watoto wapate elimu msikubali kudanganya kama tutafanya hivi na vile kwa fanya kisha tutakupa kura bila hivyo hakuna mtu hata mmoja kupiga kura yoyote ile halafu muone sasa itakuaje viongozi woooote ni waongo tu kazi kujinufaisha wao tu……………….
Kitenge cha mama kikwete kingechangia hili Daraja! Maskini ukipita pele ukipimwa lazima ukutwe na Bakteria! Poleni Nikiwa kama mtoto aliyekuwa kiongozi hapo tanzania naanza
kuona kama mzazi wangu alikuwa hapiganii haki za watanzania ametutoa watoto wote tunapata elimu nje na yeye
anakaa pazuri!
Mtu hakatazwi kuchangia hoja kutokana na maoni yake: Hoja ya kujenga na kuondoa umaskini. Ikiwa wewe mwenyewe hujaliona tatizo unataka mtu atoke mbinguni kuja kukushtua! Acha hizo ndugu yangu na jenga msingi wa maendeleo yako. Ondoa mawazo ya misaada na tengeneza future yako mwenyewe. Bado nasimamia hoja yangu kuwa Mh. JM. Kikwete na Salma hawawezi kuondoa umaskini wa kila MTZ kama wao hawako tayari kuuondoa. Hayo machungwa ni mfano mdogo tuu, je hata kuezeka nyumba yako huwezi? Acha uvivu ndugu yangu na jaribu kujituma uone kama huo umaskini hautaisha! Tenga ka-hela ka shule kwa ajili ya watoto kisha uone hao watoto watakavyokuwa chachu ya maendeleo (usiogope kuwa eti wakienda shule watalogwa hahahaaaaaaa). Kisha punguza kuchonga sana maana ni mojawapo ya sumu ya kuongeza umaskini!
Pili yaonekana unaubaguzi wa dini wewe! Mbona Mwl Nyerere hakutuachia hiyo tabia mbaya? Hivi ukifa ukakuta huyu Yesu na Mtume Muhamad ni ndugu tena wanapendana sana na sera zao ni moja utaficha wapi uso wako wewe?
Nasubiri ulete hoja/mapendekezo ya msingi kuhusu ni jinsi gani tutakavyohifadhi hayo machungwa hapa maana wewe ndie unayafahamu vizuri mazingira ya uzalishaji wake. Baada ya hoja na mapendekezo ya kutekeleza hizo hoja hapo ndipo serikali uichambue/uilaumu ila ni baada ya kuonyesha wewe utafanya nini. Unakuwa kama jamaa anayetaka kuoa kisha anaomba mchango hadi wa nguo ya bibi harusi/na yake! Loo pole.
Lete hoja maana ukinitukana umaskini upo palepale.
Tatizo la soko la bidhaa za wakulima liko wazi na halina mjadala kabisa, hapa serikali imeshindwa ama kulitatua tatizo hili ama kubuni mbinu bora za kumlipa mkulima. Hili ni tatizo la nchi nzima na ni chanzo kikubwa sana cha kinachopelekea kuwepo kwa umaskini uliokithiri (wa chakula na kipato). Je, serikali ikitafuta masoko mazuri, jamii iko tayari kubuni mbinu za kuondoa umaskini? Au pesa ikiongezeka ni mwanzo wa kulewa na kuongeza wake na watoto bila mpangilio na kuongeza umaskini?
Msingi mkubwa hapa wa kuondoa umaskini ni kutoa elimu kwa jamii katika ngazi zoteee!. Kisha kubuni mbinu mbadala za kupunguza umaskini unaotokana na ukosefu wa chakula maana kama mtu ana njaa sidhani kama akili itafanya kazi njema zaidi ya kufanya uhalifu!
Mapendekezo machache ya namna ya kufanya hapa tulipofikia ni kama haya:
1. Mkazo utiliwe zaidi katika kilimo cha mazao ya chakula na ufugaji ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa kila MTZ. Ranch nyingi za mifugo ama zimekufa/hazizalisha katika kiwango na hakuna maelezo yanayoeleweka. JWTZ linaweza kuchaguliwa kuwa mfano wa uzalishaji wa chakula na mifugo kwa ajili ya matumizi ya nchini na kusafirisha nje. Tuko fit sana hata ukija katika maswala ya ujenzi mambo ni mswano kabisa (Majumba na madaraja zote hizi ni baadhi ya fani zetu)
2. Mikakati ya kukuza mifugo iangaliwe upya na wafugaji wapewe elimu ya ufugaji bora ikiwa ni pamoja na kupatiwa masoko ya uhakika. Madalali wanaua nguvu za wakulima na naiomba serikali iwachukulie hatua kali sana! Kwanini ng’ombe auzwe kwa macho asiuzwe kwa kilo? Hivyo hivyo na mifugo mingine.
3. Ufisadi utafutiwe sumu ya kuua, ikiwezekana fisadi akibainika basi iwekwe sheria ya kifungo kisichopungua miaka 30 bila kujali kiwango cha ufisadi
4. Kila jamii ijitahidi kutoa changamoto zao za maendeleo na serikali iwe tayari kuchanganua/kusaidia na kuelekeza nguvu zake huko
5. Watanzania wenye umri wa miaka 30 nakuendelea kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2002 ni milioni 9.66 mimi nina mawazo yafuatayo:
- Katika hii jumla pafanyike utaratibu wa kuwaondoa wafanyakazi, wastaafu na marehemu kisha waliosalia (kwa makisio ya haraka labda ni watu milioni kama 4.3 hivi) serikali kupitia vyombo vyake vya utendaji watu hawa wakalipwa “Social Benefit Allowance” ya kati ya shilingi 10,000/= hadi 50,000/= kwa mwezi ili kupunguza makali ya maisha wakati mipango mikakati ikiendelea kufanyika ya namna ya mpango huu kuwa endelevu. Mifano mizuri ipo katika nchi zilizoendelea na hii itawezekana tu ikiwa kodi itasimamiwa kikamilifu.
- Hela za mfuko wa National Health Insurance Fund zinaweza zikatumiwa kama kianzio maana ni nyingi sana na pia wafanyakazi hawapati hiyo huduma ingawa wanakatwa pesa nyingi kwenye mishahara yao ya mwezi.
- Kila mfanyakazi akatwe asilimia 15% ya mshahara wake kwa ajili ya watu hawa (Kima cha chini wasikatwe maana hata wao inabidi serikali ifikirie namna ya kuwaongezea mishahara maana haitoshi)
- Asilimia 15% ya makusanyo ya kodi kwa mwezi inatosha kabisa kuwalipa hawa binadamu wenzetu kiasi kisichopungua shilingi elfu 40,000/= kwa mwezi na wao wakaweza kupunguza jehanamu ya mateso walionao
-Mfumo wa kuwalipa hawa milioni 4.3 ukitekelezwa kwa kupitia kwenye makusanyo ya kodi basi ninaimani utakuwa endelevu
- Watu wote wenye umri wa kuanzia miaka 30 na kuendelea (wakianzia na vitambulisho vya kupiga kura) waorodheshwe na wafunguliwe account bank na malipo yoye yafanyike kupitia bank.
6. Kiwango cha umaskini kinachangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi! Mfano katika kipindi hiki cha uongozi utakuta kuna mipango na mikakati mizuri sana ya maendeleo unapoingia madarakani uongozi mpya basi hakuna mwendelezo ya mipango mikakati iliyotangulia basi kazi inakuwa ni kupanga kila siku! Au pengine viongozi wanashindwa kutekeleza sera zilizotangulia ama pengine wanapoingia kwenye nafasi husika hawakuti taarifa kamili za mipango hiyo hasa zile za namna ya utekelezaji wa mipango hiyo.
7. Vijana wapewe ajira nyingi jeshini na wahusishwe katika uzalishaji na kupatiwa elimu
8. Kila mkoa na wizara ziwekewe kiwango cha kuchangia mfuko wa “Social Benefit Allowance”
9. Badala ya kwenda Bungeni kuomba serikali hela kila mwaka mikoa/majimbo yake ikae chini na kupanga namna ya kujitegemea. Kila mkoa uchangie asilimia itakayokubaliwa kulingana na mapato yake kwenda serikali kuu
10. Sekta ya sanaa ikuzwe kwani inaweza kutoa ajira kwa watu wa rika zote na viwango vyote vya elimu hivyo kupunguza umaskini wa kipato
11. Kila Mkoa utengeneze mall/plaza kwa ajili ya kufanya biashara katika mazingira mazuri na yanayokubalika kimataifa – kazi hii wapewe JWTZ vijana wa kazi
12. Foleni iliopo katika jiji la Dsm ni ishara tosha ya uzembe wa serikali!
- Ua vipanya vyote hata kama ni vya waziri na miondo mbinu mipya ya usafiri ianzishwe mara moja. Hii haihitaji vikao na makaratasi chungu mzima ya miaka mingi:
. Bunju, Tegeta, Msasani na maeneo ya mwambani wa Kigamboni weka usafiri ya boti ziendazo speed kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 3 aubuhi, saa 6 hadi saa 8 mchana, na saa 10 hadi saa 12 jioni
- Kuanzia Ubungo Tanesco upo muundo mbinu wa reli Hivyo mabasi toka Kipamba, Kiluvya, Mbezi, Kimara na Makongo yakomee Ubungo Terminal watu wapande Tren kuelekea mjini
- Reli ya kati toka G/mboto, Vingunguti, Ilala, K/koo itumike kusafirisha watu katika maeneo hayo
- Kuingiza gari binafsi mjini iwe ni shilingi elfu 30,000/= kwa mwezi au elfu 2,000/= kwa siku (hela hii iende kwenye acc ya “Social Benefit Account”
13. Serikali na wawekezaji wapangiane maeneo ya barabara na ujenzi uendelee mara moja.
14. Bado kodi haijakusanywa inavyotakiwa! tunahitaji kujitahidi katika hili.
15. Ndani ya miaka miwili umaskini utakuwa umebakia asilimia 2 na mwaka wa tatu tunaanza sasa kufanya uwekezaji wetu wenyewe kwani mjenga nchi ni mwananchi.
16. Kila sekta na kila mtu awajibike katka eneo lake la kazi na kuondoa mawazo ya kuvuna kuvuna bila kupanda! Historia inatuhukumu sasa hivi hasa wewe na mimi tulio na umri wa miaka 50+
Haya ni maoni yangu yanaweza kuwa tofauti na yako pia.
HATUJAWA SERIOUS KATIKA KUUONDOA HUU UMASKINI WAKATI UWEZO TUNAO! RASILIMALI KIBAO TUNALALAMA TUU NA KUCHONGA BADALA YA KUTAFUTA UFUMBUZI! NI AIBU SANA.
Kwa kweli nchi yetu inasikitisha sana lakini mpaka sasa hatujui
la kufanya! kama anavyosema majita lilokuwa kubwa lilianza dogo! ukiangalia tanzania iko na wabunge lakini pia hujui wanafanya kazi gani na bajeti ambayo inapangwa sijui inakuwa
hailezi pesa ambazo wanapanga bajeti watafanyia vitu gani!
CCM pesa ambazo watumia kufanya sherehe zao zingejenga
hili daraja hata kama watu wangejitulea kivalantia sababu wako
watanzania wengi wana penda nchi yao iwe na sura nzuri
Nakumbuka bibi mmoja wa kinorwigian ambae alikuwa anaishi congo mission alisaidia kukusanya pesa za kusaidia kujenga Daraja huko congo na watu ambao wanaishi kwenye kile kijiji walijitolea kubeba zege kwahiyo naamini na watanzania wapo ambao wangifanya hivyo!
Bandari ya Tanzania inakusanya kodi zaidi 100% mtu akileta gari yake tofauti na serikali ilivyoweka mtu tu wa TRA anakupangia na hujui nani wa kukutetea hata umuonyeshe risiti ulionunulia hata kama ilitoka kwa mungu lakini anaamua alivyopanga yeye sasa hizi pesa ziko wapi hawajengi sehemu ambazo zingewaingizia pesa zaidi? wanasubiri wazungu wajekuwajengea lakini mzungu si mjinga! akiweka jiwe moja anachukuwa kumi! watanzania wengi wako nje na wengine wako na kazi nzuri tu nafikiri wanauchungu na tanzania na wangekubali kukata tex zao 2% zikajenga kama airport barabara na hospitali ikiwa wangejua hizi pesa zinafanyiwa vitu vinavyotakiwa sio kula tu wakubwa na watoto wao! na watanzania hao wakiwa na wao wanapewa kipa umbele! kama
wenzetu wa ilitrea! Watanzania tuijenge tanzania kwa moyo mmoja ilijeneresheni ijayo iweza kula matunda yetu!Mungu ibariki tanzania! Majita gombea Ubunge nikupigie Debe!!
Mama wa kichaga naomba contact yako naona unahitaji ushauri Nasaha maana hoja yako ya kwanza haioani naya pili wala ya Tatu,
Nakua na wasiwasi kama wewe ndie mchangiaji yuleyule maana unajikanganya sana mara uruke huku mara kule sasa tunashindwa kukuelewa kama wewe ni nguzo imara au ki-fuata upepo..
Mjadala huu unafuatiliwa na watu wengi hadi watoto sasa unaporukaruka watu hawatakuelewa point yako ni ipi hasa. Pole kwa kushindwa kujibu hoja yangu kwa utashi kama mtu uliekomaa na kula chumvi nyingi (mtu-mzima).
Anyway tutakamatana katika hoja zijazo maana watu kama wewe tunawatafuta ili tuwa-Mao Tse Tung kwa ajili ya maendeleo ya kizazi kijacho.
“Alie shiba hajui njaa” amakweli wachaga ni wabinafsi sana
D Eagle wee waonekana mchonganishi sana tena wa kidini na kikabila. Kama unataka vita si uende voluunteer huko mashariki ya mbali?
Huishi kunisakama kila nichangiapo hapa! Unafikiri kila mada ni lazima ifanyiwe kazi au iungwe mkono na kila mtu hata kama haijengi? Mimi binafsi sipendagi hoja zako kabisa, niwie radhi kwa hilo ila inabidi nikuambie wazi. Hoja zako zote zimejaa chuki, hasira, kinyongo, ukabila na udini. Tena hoja zako hazina maadili kabisa! Sana sana naweza kusema hii ni mojawapo ya tabia ya debe tupu haliachi kutita! Which school did you went? What was your position in the class? Is hatress and judmental one of the subjects that you scored A+ go ahead man you what be bless in you life by this expertism.
Tena nakushauri uache tabia ya kutishia utawatukana watoa hoja wenzio mara kwa mara kwani wewe ni nani hapa duniani bwana? Inaelekea Wachagga wanakuuma sana roho, nakushauri oa au olewa huko nyongo yako itulia na ujenge nchi yako! Kama unatatizo lenye ushahidi kuhusu tatizo la mchagga aliyekukera nakushauri nenda mahakamani ukapate haki yako ndugu na hakikisha hakimu atakaeamua kesi sio mchagga ili usije kuleta za kuleta hapa baada ya kushindwa kesi.
Iwapo mlikwaruzana shuleni au kazini sioni kama hapa ni mahala pake au sehemu ya kumwagga sumu yako badala yake hapa leta sera na mikakati ya namna ya kupunguza hiyo njaa uliyonayo tukupe mawazo na namna ya kufanya wacha ujinga wewe.
Kwaheri ila nakuambia “Kifo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu” na kama wewe lengo lako ni kuwa Mao wenzio haya kila la kheri na endelea maana wewe unabahati maana uliambiwa wewe utaishi miaka milioni moja! CONGRATULATIONS
http://www.youtube.com/watch?v=R5k5J2iMacE&feature=related
Eagle, Sorry huwa siwapi wehu anwani yangu maana kama hapa hujaweza kuni-impress kwa hoja zako hakuna sababu ya kuwa na wewe karibu naogopa utanitukana au utani Mao Tse Tung wakati mwenzio nataka kuishi!
NB: Angalia njaa yako ya siasa itakufikisha pabaya! Usikariri kina Mao angalia hali halisi iliyopo hivi sasa na soma vitabu vinavyoweza kukujenga kuliko hivyo vya chuki chuki na hasira hasira vitakuharibia. Nenda pale UDSM idara ya Political Science kuna reserve kubwa sana ya documentation na pia nunua kupitia amazon.com hii itakusaidia kuwa na fikra sahihi. Hizi ulizonazo sasa hivi ni hovyo sana wala hupati kitu hapo sana sana D- ya mwandiko1
picha hiyo ukitazama vizuri utaona masansa
YOTE MAISHA LKN NI VIPI SIASA IKAWA JUKWAA LA MIPASHO?.WANASIASA TUBADILIKE
picha ni kali sana sasa je wale wameiona