“ELIMU NDIO NGAO THABITI”-JOKATE MWEGELO

 

Jina Jokate Mwegelo (pichani) linazidi kutokuwa geni vinywani na vichwani mwa watanzania siku baada ya siku. Kama ambavyo tuliwahi kusema siku za nyuma, Jokate ni miongoni mwa vijana wa kitanzania wenye vipaji mbalimbali ambavyo wanavitumia ipasavyo. Mbali ya kujulikana zaidi kama mshindi namba mbili (2) wa shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania mwaka 2006 na Balozi wa kinywaji cha Redds, Jokate pia ni mwanamitindo na msimamizi wa shughuli mbalimbali (MC). Isitoshe mwaka huu ameingia pia kwenye ulimwengu wa uigizaji filamu kama alivyoonekana katika filamu ya Fake Pastors iliyoingia sokoni miezi michache iliyopita.

Kama hiyo haitoshi, Jokate pia ni mtengenezaji mzuri wa matangazo ya radio kwa kutumia sauti yake. Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo historia ya maisha yake, kazi zake, ushauri alionao kwa vijana wenzake nk.

Ungependa kujua role model wake ni nani? Kama angepewa nafasi ya kuwaalika watu watano kwa chakula cha jioni angewaalika kina nani? Kwa hayo na mengineyo, fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Karibu sana ndani ya BongoCelebrity

JM: Asante sana,nashukuru.

BC: Ni wazi kwamba watu wengi wangependa kujua historia ya maisha yako.Kwa ufupi tu unaweza kutueleza ulizaliwa wapi,lini na mpaka hivi sasa umesomea katika shule gani?

JM: Nimezawaliwa Washington DC nchini Marekani mwaka 1987 ambako wazazi wangu walikuwa wakifanyia kazi.Primary nimesoma Olympio Primary School,Dsm. Secondary nimesoma St.Anthony’s Secondary School na High school nimesomea Loyola High School. Kwa sasa nipo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam nasomea Political Science.

 

BC: Unakumbuka ulipokuwa mtoto ulitaka kuwa nani? Kama ndoto yako imetimia au inaelekea kutimia, nini kimechangia mafanikio yako?

JM: Kusema ukweli sikumbuki nilikuwa na matarajio gani nilivyokuwa mdogo ila ninachojua ni kwamba ninachokifanya hivi sasa kinaendana kabisa na purpose au dhumuni langu la maisha. Pia napenda kusema kwamba ndoto yangu haijatimia kwani bado najijenga kuwa a global personnel in either the political or social development field or as a serious TV show host.

BC: Ilikuwaje ukajiingiza kwenye fani ya urembo?Nini kilikuvutia? Na je wazazi wako walisemaje ulipowadokeza juu ya nia yako ya kushiriki mashindano ambayo mpaka hivi sasa bado yanapata upinzani kutoka kwa makundi fulani fulani ndani ya jamii?

JM: Kilichonivutia ni jinsi walimbwende walivyojituma katika kazi mbalimbali za kijamii zenye high profile na vile vile kupata exposure ya kutembea sehemu mbali mbali duniani, kukutana na watu na kujitambua zaidi nini ningependa kufanya katika maisha yangu.But above all it’s a year full of fun and entertainment with lot of public appearances and interviews…..its a chance to inspire others!!

Wazazi wangu walikubali wakijua ni sanaa tu kama zilivyo zingine na hawakuniacha na kila siku waliendelea kunisisitizia kwamba nifanye yote lakini nikumbuke kwamba elimu ndio ngao thabiti ya maisha yangu. Mengine yote yanapita.

BC: Nani ni role model wako kwenye masuala ya urembo hapa nchini? Na kimataifa ni mrembo au warembo gani wanaokuvutia zaidi?Kwanini?

JM: Kwa hapa nchini role model wangu ni Irene Kiwia kwani ana degree yake.Alikuwa Miss Temeke mwaka 2000. Pamoja na hayo ana kampuni yake ambayo inasimamia events na models. Anajituma kwa kweli na si mtu wa kukata tama, ana upendo na ni mwenye kutia moyo.

Kimataifa nampenda Tyra Banks. Kikubwa ni TV show yake ambayo naamini si kitu kirahisi kufanya ila yeye anaonyesha ujasiri na kuweza kubadili fikra za wengi kuwa hata yeye anaweza. Kama unavyoona, napenda wanawake wa substance na ninaamini she is one of them.

BC: Wengi tunajua kwamba mwaka 2006 ulishika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania.Sasa kwa sababu hukushika namba moja,namba ambayo wote huwa ndio mnayoiwania katika mashindano kama yale,unadhani kama ingekuwa inawezekana siku ile au kipindi kile kikarudishwa nyuma, ungebadili kitu gani ili kuibuka mshindi?

JM: Nisingebadili jambo lolote.Naomba ieleweke I gave it my all and did my best to the best of my abilities at the time. Mengine hayo ni matokeo tu.

 

Jokate Mwegelo(kushoto) akiwa na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu(katikati) na Lisa Jensen(kulia). Jokate alikuwa mshindi wa pili na Lisa mshindi wa tatu.Hii ilikuwa muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa mwaka jana. Picha kwa hisani ya Mroki.

BC: Baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania 2006 ulivikwa taji la Balozi wa Redds kwa muda wa mwaka mmoja. Unakumbuka nini zaidi katika “ubalozi” wako wa kinywaji hicho? Nini hasa maana ya kuwa “balozi” wa Redds?

JM: Naomba ieleweke kwanza kwamba sikuvishwa taji la balozi wa Redds baada ya kuwa mshindi wa pili.Redds Fashion Ambassador linajitegemea. Finalists wote wa Miss Tanzania wako liable kushiriki. Ndio maana kama mtakumbuka nilitangulia kutajwa kama balozi kabla ya kutangazwa mshindi wa pili.

Nikirudi kwenye swali lako. Kuwa balozi wa mitindo wa Redds inakupa jukumu la kuwa msemaji mkuu wa kinywaji hicho cha Redds katika maswala ya mitindo hapa nchini Tanzania.Redds Premium Cold imekuwa iki dhamini na kuwapatia wanamitindo na wabunifu wa mitindo kwa lugha ya kigeni platform ama jukwaa la kukuza zaidi vipaji vyao.Redds ni kinywaji cha kike na wanawake wengi wanapenda mitindo na kwenda kwa wakati hivyo Redds reflects exactly that.

Nitakachokumbuka zaidi ni jinsi nilivyoweza kupata uzoefu wa kufanya kazi katika idara ya masoko nikiongozwa na kiongezi wetu Mpeli Nsekela, Brand Manager wa Redds,Marketing Team ya Tanzania breweries Ltd na vile vile niliweza kuhost show zote za mitindo iliyofanyika kama Director of Ceremonies na hivyo kuniongezea uzoefu wa kuongea mbele za watu na kujiamini zaidi.

BC: Mbali na kujishughulisha na mambo ya urembo, mitindo na wewe pia ni msimamizi wa shughuli (MC).Unamudu vipi ratiba yako ya siku ili kufanikisha shughuli zote hizo na je vyote hivi ni vipaji ambavyo umezaliwa navyo au vingine umejifunza tu ukubwani?

Page 1 of 4 | Next page