Leo ni mwaka mpya. Baada ya siku zaidi ya 365, mwaka 2007 umekatika.Leo tunaukaribisha rasmi mwaka 2008! Duniani kote shamrashamra za kuukaribisha mwaka mpya zimepamba moto. Ni muda wa maazimio mapya,matumaini mapya,misukosuko mipya na kwa vyovyote vile;tarakimu na takwimu mpya.

Bila kujali hali ya kiafya,kiuchumi,kisiasa wala kijamii, ukweli kwamba mwaka mpya umewadia huku wewe na sisi sote hapa BC tukiwa hai, ni jambo la kufurahia na kumshukuru Muumba.Ukivuka mwaka unakuwa umeandika historia mpya katika maisha yako. Vitabu vya kumbukumbu vitaandika kwamba uliuona mwaka 2008! Ni jambo la kumshukuru muumba kwani ni wazi wapo wengi sana waliotamani kuuona mwaka huu na wasifanikiwe.Kama huamini, fikiria kidogo tu ni watu wangapi ambao umehudhuria mazishi yao au kusikia habari juu ya misiba yao?Unaona? Hatuna budi kumshukuru Mungu.

Wakati huu tunapoingia mwaka mpya wa 2008,tungependa kwanza kukutakia kila la kheri wewe msomaji,mtembeleaji au mchangiaji wetu.Mwenyezi Mungu akuongoze na kukubariki katika kila jambo utakalolifanya ndani ya mwaka huu wa 2008.Kama mwaka 2007 haukuwa wenye mafanikio kwako,usikate tama.Fungua ukurasa mpya huku ukiwa na fikra chanya zaidi na utaona mabadiliko.

Tungependa pia kukupa shukrani zetu za pekee kwa kuwa mtembeleaji,msomaji au mchangiaji mzuri wa BC.Kama kuna mafanikio yoyote ambayo tumeyapata tangu kuanzishwa kwa blog/site hii,ni wazi kabisa kwamba mafanikio hayo yametokana na mchango wako wewe msomaji,mtembeleaji na mchangiaji wetu.

Maoni yako,michango yako,mapendekezo yako, mwitiko(feedback) wako nk. ndio mambo ambayo yanatufanya tuendelee kujitahidi kukidhi haja yako ya kupata habari mbalimbali,kujua kwa undani kidogo juu ya maisha na mienendo ya celebrities wetu nchini Tanzania na kila inapobidi, celebrities wengine barani Afrika na hata ulimwenguni kote. Tunaendelea kuamini kwamba habari na mienendo ya watu maarufu/mashuhuri katika jamii yeyote,ni vitu vyenye ushawishi fulani(kama sio mkubwa) kwa jamii husika.Hii ni pamoja na Tanzania yetu.

Kwa upande mwingine tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa celebrities ambao katika kipindi kifupi tu tangu kuanzishwa kwa blog/site hii,wamekuwa na imani nasi kiasi cha kukubali kufanya nasi mahojiano,kuturuhusu kutumia picha zao,habari zao binafsi nk. Tunapenda kuwashukuru kwa sababu kwa kuturuhusu na kukubali kwenu kufanya nasi mahojiano na kuandika habari zenu, mmeonyesha sio tu ukomavu wa kifikra na kimawazo bali mmetambua mchango na ushawishi wenu miongoni mwa wanajamii na hivyo kujitoa mhanga kwa minajili ya kuwapa fursa wanajamii wengine, kujifunza mengi kwa kuangalia na kusoma kuhusu maisha yenu kupitia kuzijua changamoto na mafanikio yenu.Huo ndio mfano halisi wa “kioo cha jamii”.

Isitoshe, ninyi mmetambua kwamba dunia ya leo inakwenda sambamba na mabadiliko mengi hususani katika nyanja ya habari na mawasiliano.Mmetambua kwamba uandishi wa raia(citizen journalism),kama zilivyo blogs, sio jambo la kubeza hata kidogo. Mmeungana na vyombo vya habari vyote vikubwa duniani katika kuthibitisha hilo.BC inaheshimu mchango wenu na tunaahidi kuendelea kuandika habari zenu kwa staha na heshima kubwa. Tunatumaini wasomaji,watembeleaji na wachangiaji wetu katika mwaka huu wa 2008,watatusaidia katika kutimiza malengo hayo.Asanteni.

Kwa upande wetu sisi hapa BC, tunachopenda kukuahidi wewe msomaji,mtembeleaji na mchangiaji ni kuendelea kukuletea habari zaidi,mahojiano zaidi,picha zaidi,videos zaidi na kila linalowezekana.Tafadhali ukiwa na maoni,ushauri, mapendekezo yoyote yale na ambayo ungependa kutueleza bila kuonekana na kila mtu,usisite kuwasiliana nasi kwa kutumia e-mail yetu ya bongocelebrity at gmail dot com au kutumia fomu ya kuwasiliana inayopatikana katika ukurasa wetu wa “Kuhusu BongoCelebrity” hapo juu.

Shukrani za pekee ziwafikie bloggers wenzetu mbalimbali,vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania na nje ya Tanzania,wapiga picha mbalimbali na wengineo wote ambao wanaendelea kushirikiana nasi katika jukumu hili zito la habari na mawasiliano.Asanteni sana.Bila ninyi,haiwezekani.BC inathamini sana mchango wenu.

Tunapouanza mwaka mpya wa 2008,tunakusihi uendelee kututembelea,kuchangia,kutukosoa tunapokosea na pia kumwambia mwenzako kuhusu uwanja huu ili naye asipitwe na yanayojiri.Kama msemo kwa Kiswahili unavyosema;Kizuri Kula Na Nduguyo.Tunaamini BC ni kitu kizuri,tafadhali kula na nduguyo.Wakati huo huo usisahau kwamba,It doesn’t take great men/women to do great things but just those who are greatly dedicated to doing them. That person is you.HAPPY NEW YEAR 2008!

Feedback / Comments

11 Responses to “KWAHERI 2007,KARIBU 2008!”

  1. Comment by Tarimo on January 1st, 2008 9:24 am

    Asanteni BC.Ninawatakia kila la kheri pia ili mzidi kutupa vitu zaidi.

  2. Comment by michuzi on January 1st, 2008 9:57 am

    Asante BC kwa salamu za mwaka mpya kwetu wasomaji wako. Nakutakia mwaka wenye mafanikio na mahojiano mengi zaidi na usichoke kuenzi bongo celebrity wetu ambao hawajawahi kuwa na uwanda wa kuonekana na kuenziwa kama hapa BC

    HAPPY NEW YEAR

  3. Comment by Upendo Furaha on January 1st, 2008 10:58 am

    Asanteni sana B.C. Nami pia pamoja na familia yangu; Tunawatakieni kila la heri katika mwaka huu 2008. Pia Ninamuomba Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema ili muweze kuendelea kutupa “Elimu” kupitia Blog hii.
    Pia ninawatakia wapenzi wote wa Blog hii Heri ya Mwaka mpya 2008.

  4. Comment by Kimori on January 1st, 2008 12:46 pm

    Thanks BC and keep it up!

    To all regular visitors of the blog, who have made it, my Best wishes and blissful moments in the year 2008! May The Almoght Lord bestow upon you abundant blessings, wisdom, integrity and positive mindset!

    Happy New Year 2008!

  5. Comment by Majita on January 1st, 2008 1:25 pm

    Asanteni BC.
    Huu ni mwisho wa Mwanzo Mpya 2007-2008
    epi new yr

  6. Comment by Edwin Ndaki on January 1st, 2008 2:53 pm

    Asante mola wangu kwa kunijaalia kuuona mwaka 2008.

    Poleni sana ndugu zangu mliopoteza wenzetu huko Kenya wakti mkijitahidi kutafuta sthili yenu.RIP

    Kila la kheri BC na watu wote mnaotembela ukurasa huu mola atuepushe na majanga mbalimbali.

    Tusikate tamaa…KWA MUNGU YOTE yanawezekana.

    Aluta kontinua..mapambano bado yanaendelea.

    Wasalaaaam

    Edo

  7. Comment by Nanii on January 1st, 2008 3:12 pm

    Asante Bc kwa info nyingi mlizotuletea humu ndani. tumejifunza mengi kutoka kwa wengi na tumejua mengi ya celebrities wa bongo. Kazeni buti na nawatakia the best and more kutoka humu ndani ya BC.

  8. Comment by mwalimuzawadi on January 1st, 2008 4:29 pm

    Shukran BC kwa kazi mwanana kabisa

    Sote tujaliwe kheri na yote mema tunayoomba

  9. Comment by Mama wa Kichagga on January 1st, 2008 7:00 pm

    BC

    Kila la kheri na asanteni sana kwa kutuhabarisha kwa njia hii kwani tunaelimika sana kwa michango ya celebrities na wachangiaji kwa ujumla.

    Uwanja huu ni mzuri sana wa kujifunza namna ya mawasiliano na utoaji wa hoja mbalimbali kutoka kwa wadau wote.

    Nchi hujengwa na wenye moyo, ambao ni wewe na mimi kwa kuangalia katika mtizamo tofauti na unaofaa kwa njia ya amani.

    Asanteni sana BC & namuomba Mungu mwaka 2008 uwe wa baraka kwetu sote tukijua kuwa maendeleo hayawezi kupatikana iwapo wewe, mimi na yule hatutusimama ipasavyo katika nafasi zetu iwe ni ngazi ya familia, Jumuia ama Taifa kwa ujumla “It can be done, play your part”.

    “JUST AS OUR EYES NEED LIGHT IN ORDER TO SEE, OUR MINDS NEED IDEAS IN ORDER TO CONCEIVE” – Napoleon Hill

  10. Comment by matty on January 2nd, 2008 5:26 am

    Asante BC kwa salamu za mwaka mpya na mimi napenda kuwatakia kila la heri BC na wadau wote kwa kuanza mwaka mpya ni jambo la heri na la kumshukuru Mungu kwani wengi walitamani kuuona mwaka 2008 lakini mungu aliwapenda zaidi.(mungu awalaze mahali pema peponi wote walioaga dunia kabla ya 2008).
    Tuuanze vizuri mwaka 2008 kwa amani na upendo na Mungu atatuongoza.

  11. Comment by robert on January 26th, 2008 1:39 pm

    hi i real like ur web site..

Leave a Reply