Khadija Mwanamboka (pichani) ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa kampuni isiyo ya kiserikali iitwayo Tanzania Mitindo House (TMH) akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi ndani ya ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar.

Khadija alikuwa akitoa taarifa kufuatia mafanikio waliyoyapata kutokana na onyesho la mitindo ya mavazi lililofanyika mwaka jana wakati wa Siku ya Ukimwi Duniani. Onyesho hilo lililoitwa Red Ribbon Fashion Gala lilifanikiwa kuingiza kiasi cha pesa taslimu milioni nane (Tshs 8m) ambazo kwa asilimia kubwa zitatumika kuwasaidia watoto 30 ambao ni yatima na wenye virusi vya ukimwi.Mwanamboka ameongeza kuwa kupitia shirika lao wamenunua vifaa mbalimbali vikiwemo vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni 3.8 ikiwa ni msaada kwa ajili ya watoto hao.

Baadhi ya wabunifu wa mitindo wengine waanzilishi na wanaounda TMH ni Haji Mohamed, Jamila Swai,Ally Rehmtulla,Fatma Amour,Angelo Mlaki na Masoud Kipanya.

Mwaka jana tuliwahi kufanya mahojiano na Khadija Mwanamboka kuhusiana na Tanzania Mitindo House.Unaweza kuyasoma mahojiano hayo kwa kubonyeza hapa. Ukitaka kujua jinsi gani unaweza kusaidia au kushiriki unaweza kuwasiliana na Khadija kwa kutumia e-mail: vituvyakhadija at yahoo.com.

Picha kwa hisani ya MichuziJR

Feedback / Comments

4 Responses to “TANZANIA DESIGNS FOR LIVES”

  1. Comment by Upendo Furaha on January 3rd, 2008 11:33 am

    Dada Mwanamboka pamoja na NGO yako ya THM ninawapongeza kwa kuwasaidia “Walioathirika”. Ningeomba NGO nyingine zimuunge mkono katika kuinua “Wasiojiweza”.

  2. Comment by rehema on January 3rd, 2008 5:27 pm

    bravo khadija..

    move on iron lady we’ll support you tukujaaliwa.

    jaza yako itaikuta kwa M’Mungu Inshaallah

    da rehema UK

  3. Comment by wakunyumba on January 8th, 2008 1:12 am

    Hongera sana Hadija kwa kazi nzuri, ila du diet please,

  4. Comment by Alfonso on January 11th, 2008 11:59 am

    Hongera dada, lakini mbona haieleweki hao watoto wanatoka maeneo gani au kwa msaada huo unawafikia wakiwa wapi? Mfano hai ni wa misaada ya TACAIDS kupitia RFA, wengi wanatumia majina ya watoto yatima au waathirika, lakini misaada hiyo haiwafikii au inafika kiasi. Tafadhali kama umeamua kuwasaidia watoto hao wasaidie kwa moyo mmoja na uwazi utashangaa utakavyobarikiwa. UKIFANYA KWA MOYO HAKIKA BWANA ATABARIKI KAZI ZA MIKONO YAKO!

Leave a Reply