PICHA YA WIKI # 01

 

Fukwe za jiji la Dar-es-salaam au maeneo yote yenye fukwe nchini Tanzania, yana mandhari zenye kuvutia sana hususani nyakati za jioni,jua linapoelekea kuzama, kama inavyoonekana pichani fukwe ya Kigamboni. Swali gumu ni je tunazitunza ipasavyo fukwe hizi? Serikali zetu zinawaongoza vipi wananchi katika kuzitunza fukwe hizi hususani wakati huu ambapo tishio la mabadiliko ya hali ya hewa linazidi kukua na kuwa wazi zaidi? Ukitaka kujifunza mengi kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani bonyeza hapa.

Picha hii ambayo ndio picha yetu ya wiki hii ni kwa hisani ya Pius Mikongoti aliyeko masomoni nchini Malaysia.

Page 1 of 3 | Next page