NGOMA YA UKAE

 

Bila hiana wala ubishi, DDC Mlimani Park(Wana-Sikinde Ngoma ya Ukae) ni mojawapo ya bendi zilizowahi kutamba na kujizolea sifa kemkem nchini Tanzania. Pichani ni kikosi kizito cha Wana-Sikinde.Ili kupata majina kamili na nafasi zao katika bendi,tuliwasiliana na Fresh Jumbe ambaye siku za nyuma aliwahi kutamba na Sikinde. Biila kusita Fresh alitupa captioning nzuri kabisa ya picha hii ya Sikinde.Fresh hivi sasa anafanyia kazi zake za muziki nchini Japan.Mwaka jana tuliwahi kufanya naye mahojiano ambayo,kama yalikupita,unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.

WALIOSIMAMA NYUMA TOKA KUSHOTO:Habibu Abbas Mgalusi “Jeff” (Drums), Wa pili jina limenitoka, anayefuatia ni Shaaban Lendi (saxphone), Hamisi Milambo (Trumpet), Nyuma ya Hamisi Milambo ni Kalamazoo (Saxphone), Huruka Uvuruge (Rhythm guitar), Machaku Salum (Trumpet), Kassim Rashid “Kizunga” (Lead guitar), Charles Ngosha (Bass) na Ali Jamwaka au Ali “Tumba” (Congers).

WALIOCHUCHUMAA MBELE TOKA KUSHOTO:Wa kwanza simjui, wa pili ni Juma Shabani (Drums) (Huyu nilikuwanae Dar International, Anaefuata mwenye kofia ni Tino Masinge (Muimbaji) nae pia nilikuwa nae Dar International na nimeimba nae karibu nyimbo zote kule Super Bomboka, alijiunga na Sikinde baada ya mimi kutoka. Anaemfuatia Tino kwa nyuma kidogo simjui, anaefuatia mwenye viatu vyeupe ni Husein Jumbe (Muimbaji), nyuma ya husein Jumbe aliyeshikwa bega na Dede simjui, halafu Shaaban Dede (aliyegeuka nyuma na kumshika mwenzie bega (Muimbaji), baada ya Dede kwa mbele kidogo ni Adam Bakari “Sauti ya zege” (Muimbaji), Nyuma kidogo ya Adam ni Hassan Kunyata (Muimbaji), Baada ya Kunyata ni Joseph Bernard (Saxphone) na wa mwisho kabisa mwenye kipara simjui.

Picha kwa msaada mkubwa wa MichuziJR.

Page 1 of 3 | Next page