MY TANZANIA   |   PLACES TO GO   |   MEDIA   |   ONLINE ENTERTAINMENT    

 

Ukizungumzia wanamuziki waliowahi kutamba nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla huwezi kuacha kumtaja Marehemu Patrick Balisidya(pichani). Mpaka hivi leo baadhi ya vibao vyake kama vile “Harusi” ni vya kuotea na ni moja ya nyimbo zinazopendwa sana hususani wakati wa sherehe za harusi.Nyimbo nyingine zilizowahi kutamba ni kama vile Wikiendi,Dirishani na Tausi.

Patrick Balisidya alizaliwa tarehe 18 Aprili mwaka 1946 huko Mvumi mkoani Dodoma.Baada ya kumaliza shule alifanya kazi ya ufundi kwa muda mfupi kabla ya kuanza rasmi shughuli za muziki mnamo mwaka 1967 akiwa kama mpiga gitaa wa bendi ya Dar-es-salaam Jazz Band. Kufikia mwaka 1970, Patrick Balisidya alikuwa ashaanzisha bendi yake iliyojulikana kama Afro 70,bendi ambayo ilitokea kuwa moto wa kuotea mbali. Afro 70 walitamba sana na mtindo wao uliojulikana kama “Afrosa”. Mtindo huu ulitumia zaidi vionjo na ala kutoka mkoani Dodoma hususani kabila la wagogo.

Patrick Balisidya alifariki dunia tarehe 7 August mwaka 2004 huko Kibaha mkoani Pwani.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Burudika na kibao Harusi hapo chini.Hii ni maalumu kwa wote wanaojiandaa kufunga ndoa wikiendi hii.

Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.

Wimbo huu kwa hisani ya Bongo Radio.

Share and Enjoy:
  • Digg
  • Sphinn
  • del.icio.us
  • Facebook
  • Mixx
  • Google Bookmarks
  • email
  • LinkedIn
  • Live
  • Spurl
  • Technorati
  • Yahoo! Buzz
  • YahooMyWeb

Feedback / Comments

4 Responses to “BADO TUNAKUKUMBUKA”

  1. Comment by Edwin Ndaki on January 10th, 2008 3:23 am

    Duu.leo kweli mmenikumbusha selebriti halisi wa kibongo.

    Mwenyezi Mungu ilaze roho yake mahali pema peponi.Siku zote zinapotoea rabsha,maonevu,matumizi ya nguvu kupita kiasi,usisafi namkumbuka mzee huyu kwa wimbo wake “DUNIA YA MASHAKA”…

    Anasema kwenye moja mstarii..wemaaaaaa hawanaaa maishaaa…..

  2. Comment by Freddy Macha on January 10th, 2008 7:18 pm

    Nakumbuka nikicheza Afrosa pale hoteli ya Princess, Dar…mtaa wa Mnazi Mmoja. Enzi hizo tulikuwa na mabugi. Madensi ya vijana saa za mchana, maana wanafunzi mashuleni hatukuruhusiwa kwenda dansi za usiku.
    Balisidja alikuwa mmoja wa waanzilishi rasmi wa mseto wa ngoma zetu za asili na blues/ funk. Kitu hiki kilienezwa na wanamuziki wa Afrika Magharibi akina Osibisa, Fela Kuti na Manu Di Bangu.
    Afro 70 lakini waliangushw ana ukosefu wa studio za muziki Bongo. Siku hizi wanamuziki wa kizazi kipya wanarekodi tu kirahisi. Enzi hizo mastaa wetu waliishia tu kapuni. Moja ya tatizo la bendi kama Afro 70, Sunburst, Marijani na Mbaraka Mwinshehe kutojulikana sana kimataifa ni hilo. Kutorekodi.
    Heko BC kwa kumtoa Patrick.
    Mungu ailaze roho yake pema peponi.

  3. Comment by Kajura Hamisi on January 15th, 2008 1:44 am

    Hongera Bongo Celebrity….hawa ndio ma celebrity wa kweli sio hawa kina yakhe mavi ya nani (Fleva). Leteni raha na kupaisha muziki wetu wa asili si wa kuletewa kwenye sahani na kubatiza jina kuwa ni wetu.

  4. Comment by Simon Kizito on January 31st, 2008 2:24 pm

    Hongera BC…hawa ndo ma celebrity wa kweli si hawa wababaishaji wa fleva. Lete raha BC!

Leave a Reply