Sifa moja ya muziki mzuri ni kwamba ukiusikia tu unajikuta na wewe unamumunya mumunya maneno yake huku ukitingisha kichwa,mguu,bega,kiuno,ukirusha mikono hewani na kutamani kunyanyuka ucheze.Muziki mzuri ni ule ambao tune yake hukaa kichwani kwako daima,haikutoki. Hata ukiusikia bila maneno au kwa ala tupu(acapella) unautambua.Isitoshe,wakati mwingine haijalishi kama unaelewa maneno yaliyomo au la.
Leo tunahama kidogo kwetu.Tunataka kuthibitisha kwamba muziki ni lugha ya dunia(Music is a universal language). Wimbo unaitwa Africa Mokili Mobimba.(Africa Worldwide/ Afrika duniani pote).Wimbo huu umeimbwa na kurudiwa na bendi kadhaa za DRC kiasi kwamba kuna utata fulani kuhusu nani hasa alikuwa mtunzi au mwenye wimbo huu.Pamoja na hayo wanamuziki kama Dr.Nico,Tabu Ley Rochereau(pichani) na Dechaud(kaka mkubwa wa Dr.Nico) ndio wanatambulika zaidi kuhusiana na wimbo huu. Bendi kama Rumbanella Band imewahi pia kuurudia wimbo huu na kupata nao mafanikio.Pata burudani.Ijumaa Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Shukrani F.T.Mtimkubwa kwa wimbo huu.
Page 1 of 3 | Next page