EXCLUSIVE CHITCHAT WITH FINA MANGO

Kila mwaka,tarehe 14 February(Siku ya Wapendanao),yeye hukumbuka au kusheherekea siku yake ya kuzaliwa. Alipozaliwa wazazi wake walimuita Fina.Leo hii wengi tunamfahamu kama Fina Mango(pichani),mtangazaji maarufu wa kituo cha radio cha Clouds FM.

Yeye ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watano(5) kwa upande wa mama yake, Fortunata M.Mango na watoto saba(7) kwa upande wa Marehemu baba yake,,Joseph Mango.Anaye dada mmoja na kaka watatu(3) wa kuzaliwa tumbo moja na dada mmoja na kaka mmoja wa kambo.

Alianza pilikapilika za masuala ya elimu mkoani Arusha katika shule ya Mtakatifu Constantine(St.Constantine) na baadaye kujiunga na shule ya sekondari Jitegemee jijini Dar-es-salaam kwa ajili ya masomo ya O-Level.Kisha akajiunga na shule ya Shaaban Robert ya jijini Dar-es-salaam kwa masomo ya A-Level na kuhitimu mwaka 1999. Baada ya hapo akajiunga na Clouds FM ingawa kimasomo hakuishia hapo kwani baadaye alijiunga na FTC(Financial Training Centre) ambapo amesomea masuala ya biashara.Bado ana mpango wa kuendelea zaidi kimasomo.

Leo hii yeye ni Brand Manager wa kipindi cha Power Breakfast ambacho anakiendesha kwa kushirikiana na Masoud Kipanya (KP).Kipindi kinarushwa kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12 alfajiri mpaka saa 3 asubuhi.

Fina Mango pia ni mjasiriamali, yeye ndio mmiliki wa kampuni ijulikanayo kama One Plus Communication ambayo inashughulika na masuala ya Usimamizi wa Shughuli na Matukio ya Mashirika mbalimbali na Uhusiano wa Jamii (Corporate Events Management & Public Relations (PR). Ofisi za One Plus Communication zipo maeneo ya Victoria ilipo Victoria Gas Station pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi.

Hivi karibuni tulipata fursa ya kufanya naye mahojiano ambapo tuliongelea mambo mengi kuhusiana na kazi yake ya utangazaji,maisha yake binafsi na mipango yake ya baadaye.Kumbukumbu na uwazi alionao Fina ni jambo ambalo limetuvutia sana. Unataka kujua Fina anasemaje kuhusu maendeleo ya kisayansi na kitekinolojia ulimwenguni? Asingekuwa mtangazaji angependa kuwa nani?Je umeshawahi kuona picha za utotoni za Fina? Fuatana nasi katika mahojiano haya ya pekee.

BC: Unakumbuka nini kuhusu siku yako ya kwanza kama mtangazaji? Ilikuwaje na wapi uliposikika hewani “live”?

FM: Ki ukweli, the first time nimekwenda hewani haikuwa kama mtangazaji, nilikuwa kama mgeni kwenye kipindi cha M.L. Chris cha usiku – ‘Cruise to Midnight’. Lakini my first show ilikuwa on a very rainy day, nilipitiwa home, tukaja studio gorofa ya 14, Kitega Uchumi hapa, jumapili asubuhi, nikiwa napiga classics. Kipindi kilianza saa tatu asubuhi, sikumbuki for how many hours lakini nadhani kama 2 hours hivi kilikuwa. Kumbukumbu yangu ndogo yaniambia sikutetemeka wala kupanic, nakumbuka ilikuwa easy tu… the rest is history.

 

A long history indeed…Fina Mango akiwa na miezi kadhaa tu.

BC: Ni wazi kwamba kazi nyeti kama ya utangazaji inahitaji maandalizi na pia kuwa up to date na matukio mengi ya kitaifa na kimataifa. Unaweza kutuambia kabla ya kwenda hewani,huwa unafanya maandalizi gani ya msingi? Kwa mfano kabla hujaanza kipindi chenu wewe na KP cha Power Breakfast?

FM: Format ya PB ‘Power Breakfast’ ni ya mazungumzo zaidi – baina ya wenyewe yaani sisi watangazaji na wasikilizaji kupitia msgs, emails au barua nk. Kwahiyo katika hali ya kawaida ninakuwa maandalizini saa 24. Kila ninachokiona na kukisikia chaweza kuwa topic ama sehemu ya kipindi the following day… kila ninachokisoma vilevile. Kwahiyo maandalizi kwetu ama kwangu hayana muda, saa zote mie niko katika maandalizi. Ila inanilazimu kuangalia au kusikiliza ama kusoma japo gazeti, radio ama TV kupata habari za siku hiyo, ziwe za ndani ama nje ya nchi. Lazima ujue dunia ikoje kwa siku hiyo japo kwa muhtasari.

Ukweli ni kwamba 5, 6 years ago, sikuwa mtu wa kusoma sana, kipindi kimenifanya nimekuwa msomaji wa vitu mbali mbali, kuanzia siasa za ulimwengu, uchumi hadi social matters. And I tell you, as a friend of mine likes to say it is ‘food for thoughts’. Knowledge is a beautiful thing. Maisha yangu kwa sasa yazungukiwa na kipindi unajua, nikiona kitabu, ama nikisoma journal ama article nitakachokipata nikidhani ni cha manufaa basi huwa nawaza watu wangu tu kwenye PB kwenda ku share the knowledge… kwa style hii najikuta nina hamu ya kujua vitu kila nafasi ninapoipata!

 

Fina Mango na Masoud Kipanya katika kitambulisho rasmi cha Power Breakfast.

BC: Kuna rafiki yangu mmoja amewahi kuniambia kwamba watangazaji wa radio ni watu wenye imani kuliko makundi mengi sana ya wafanyakazi.Yeye anasema watangazaji,bila kujua kama kuna mtu anasikiliza mnachosema huko nje,bado mtaendelea kuongea tu.Imani hii inatokana na nini kwa upande wako? Na je tekinolojia za kisasa zinawasaidia vipi kujua kwamba hampo “wapweke”?

FM: Unajua nilianza kwa kucheka baada ya kumaliza kusoma hili swali lako, kuna mwaka bwana wakati Jimmy Kabwe bado yupo Clouds, aliongea for a whole HOUR!! Kumbe fader (hii ni kama button ya sauti, ikiwa juu ndio wasikika ikiwa chini ume mute) iko chini bwana na ye kilema, anachojua akija ana bonyeza on air button kwenye mixer anaanza zake kupiga domo… sasa watu wakaanza leo vipi?? Maana muziki wasikika ukishuka na kupanda, kumbe mwenyewe Jimmy akishusha anavyoongea na kuupandisha akimaliza… alisusa, hakufanya tena kipindi. Ukweli tulimcheka sana… unajua unaamka saa kumi na moja uje uanze kipindi saa kumi na mbili halafu kitu kama hicho, kinakutoa mood kabisa.. anyway moral of the story!

Ni kweli aisee, hata kama hujui wangapi au wapo hata wanaokusikiliza we utaongea tu… ila with advancement of technology, its easy to know wasikilizwa au lah. Nitakupa mfano; sms’s sawa, tunapokuwa na topic we prompt people to participate na kuchangia kupitia msg, kama topic ni hot, twaweza pata hadi 1000 msg kwa saa mmoja. Na hatuzifikii zote… zingine mnasoma off air twazijibu hewani, au zingine baada ya kipindi twazipitia, sometimes tunajibu mara nyingine ngumu inabidi ufute tu zote uanze upya. Hiyo inasaidia unajua hamko pekee yenu. Halafu kama nilivyosema mfumo wa PB ni wa mazungumzo zaidi.Unajikuta mtu unachukua tu simu yako unaongezea kutokana na kitu Fina au Masoud amesema na kwa vile tuna ruhusu hali hii, ikiingia msg kama inanipa mie uzito basi naishadadia kama yaampa masoud naisoma vile vile na mara nyingine kwa style ya kuibeza unajua kama inavyokuwa katika mazungumzo mkiwa ana kwa ana… so that helps you see… mnajua mko pamoja!

BC: Je kama mtangazaji,ukiwa “live” redioni, imeshawahi kutokea ukasema kitu ambacho baadaye ulijutia kwanini ulikisema? Kama jibu ni ndio,ilikuwaje? Kama jibu ni hapa,unahakikisha vipi kwamba unaepuka vipi hali kama hizo?

FM: Imeshanikuta, eeh he tena usinikumbushe, ya mwisho mpaka kikaoni niliambiwa! Halafu sasa kumbe mie mwenyewe hata sikujigundua kama nimefanya hivyo.. siku bisha kwa vile najua yawezekana, unapokuwa caught up in the heat of the moment… it happens, lakini rarely kwa kweli. Kama umejipanga plus uzoefu mara chache itakutokea. Ukiwa makini zaidi haikutokei kabisa. Ila kwa sisi ambao twazungumza na si kutangaza, kuzomoka kupo kupo.LOL. Ila pre-production itaepusha sana kuzomoka kwa vile mtakuwa mmeshajipanga na mwajua mwataka nini mwisho wa kipindi kiwe ndio kama outcome…

Come on, I can’t tell you ‘exactly what it was… he pengine wasikilizaji hawakuistukia?? Halafu ndio ni wastue now? Aku!! LOL. Kiukweli sikisemi… kwanza umenikumbusha tayari umenipa chills tumboni… nikikisema ndi kama kulianza upya na mie nilishajisahalia zangu!! NO WAY… SISEMI!! Pole BC…

 

Fina Mango utotoni akiwa na mama yake mzazi.

BC: Watangazaji wa radio(kama wewe) na wale wa luninga(TV) mnao ushawishi mkubwa sana kwa jamii. Kwa upande wa Tanzania unadhani watangazaji mnatimizia wajibu wenu ipasavyo wa kuhakikisha kwa mfano wananchi wanajenga na kulinda afya zao,wanachagua viongozi wanaofaa,wanaepuka maambukizi ya maradhi nk? Nini ungependa kuona kinaongezwa katika wajibu wenu?

FM: Kutimiza wajibu; nadhani kwa kweli ni ngumu kwa mimi kutoa tamko ama a general analysis ya wana habari kwa vile wajibu si wajua watofautiana bwana.Kila mtu ana malengo yake mwisho wa siku… lakini nikisema nizungumzie upande wangu mimi na hasa kipindi changu kwa vile I only do one show -PB. Naweza kusema kwa kiasi kikubwa tunajaribu kutoa miongozo na taarifa rasmi kwa msikilizaji wetu, sasa maamuzi ya kuchukua ama kufuata kile ambacho sisi twadhani ndicho sahihi ni juu ya msikilizaji. Bahati nyingine nzuri bwana waTanzania wanajua wanachotaka, we wazema sema wee lakini mwisho wa siku mazingira yake ndio yatakayompa mwongozo halisi.

Ntakupa mfano eh twasema siku hizi mikopo iko nje nje, hii macro loans and salary loans ziko nyingi, but how u choose to make use of them is up to you… ukiamua kununua gari inayofanana na mtoto wa bosi fulani halafu ukalala njaa na kutengeneza madeni mengine ya ziada that would have been one’s choice, but I gave out the right information kwamba kuna mkopo kule tena wa riba nafuu uongo??? The same applies every where else katika mazungumzo ya kipindi. Lakini mwisho wa siku mimi naamini tunatimiza malengo yetu sisi kama PB ya Clouds fm.

 

Mango’s family. Hapo Fina alikuwa hajazaliwa bado.Alikuwa ndio kwanza yuko tumboni.Can you see her?

BC: Maendeleo ya kisayansi na tekinolojia yanazidi kupamba moto kote ulimwenguni.Hivi sasa inawezekana kuwa na radio hata kutokea kwenye kachumba kadogo tu au hata bila ofisi. Kwa mtizamo wako nini faida na hasara za maendeleo haya? Unadhani yanatishia kwa namna yoyote ile radio kama hii yenu ya Clouds FM?

FM: Hiyo safi sana, tena mimi nataka ma redio kama kwa wenzetu, nyie mlio huko mwajua, ukiwasha radio, frequency karibu zote zina wamiliki uongo?? Ndio nataka mie, ushindani is something so beautiful and powerfull. Hatuna washindani hapa bwana, tuna wafuasi tu and sometimes actually most of the times ina dumaza! And besides for my case ina mpa hata jeuri Kusaga, LOL (bosi wangu huyu wa ukweli hana noma) but seriously faida ni nyingi zaidi. Lets see;

(1) Ajira zitaongezeka,

(2) Ushindani utaongezeka hence quality of the products on air

(3) Maslahi yetu pia yatabadilika sana kwa vile mtu mzuri atakuwa ananyemelewa na washindani, sasa itawalazimu wamiliki wa vyombo vya habari kusumbua kichwa ku sustain good people.

(4) Itamaanisha pia mahitaji ya teknolojia, better technology better quality products …

(5) Choice. wasikilizaji watapata a wider range of choices za radio ama tv ama magazeti ya kusoma. Dar saivi kuna magazines kama vile kuna mahala yafyatuliwa bure… and asilimia kubwa excellent quality. In terms of material not content though… now tell me who doesn’t want that?? I certainly DO!!

BC: Ni watangazaji gani Tanzania na ulimwenguni kote ambao unazipenda zaidi kazi zao ikiwemo ya utangazaji? Kwanini?

FM: Humu ndani Tanzania, sina mmoja specifically ambae naweza kusema napenda zaidi kazi zao ila wako a handful ambao nathamini michango yao kwa namna tofauti. Mfano ni wafanyakazi wenzangu pale Clouds… nimejaaliwa kuwa nafanya kazi na kundi la watu wabunifu, wasio na ubinafsi wala hila!! Kutoka KP, mpaka Dina Marios ambao ni wageni zaidi pale kwetu lakini wa me blend in very well na utadhani tumefanya kazi wote miaka na miaka. I am blessed with a second family and I cherish na kuthamini michango yao wote kwa ujumla katika kufanikisha kazi yangu mimi na ya kituo chetu kwa ujumla!

 

Fina Mango(kushoto) akiwa na Lady Jaydee(katikati) na Monalisa siku ya harusi ya Marehemu Amina Chifupa(R.I.P)

BC: Ratiba yako ya kila siku ikoje? Na siku “kamili” (perfect) day kwako huwa ikoje?

FM: Well, alarm yangu goes off at 4:50am. Naiacha ina snooze for another 10mins ikilia 5:00am ndio naamka. Naingia bafuni naoga kwa kama nusu saa, then navaa (of course hatua ya mafuta na nini inatangulia) nabeba vyangu naingia kwenye gari natimka. Hiyo inakuwa kama 5:50am hivi, kwa vile ni dakika 5 tu kutoka nyumbani mpaka ofisini, asubuhi hiyo hakuna traffic bado. Kawaida nguo ya kuvaa asubuhi nakuwa nimeshatayarisha kabla sijalala na handbag nitakayoibeba siku hiyo inakuwa imeshakamilika na vitu vyake, so mimi asubuhi nafanya kuibeba tu.

Nikifika mara nyingi namtangulia Masoud, namkuta Jackie anamalizia kusoma habari, then me naingia napanga jingles zangu na matangazo akimaliza anayapiga nachukua kiti changu cha enzi nyuma ya mixer tayari kwa kuliendesha li PB.

Wakati wimbo wa kwanza waenda nitamsikia masoud anaingia kwa vile huwa naacha mlango wa studio wazi, kawaida yake lazima aingie na makelele basi namsikia huyoo anaingia, atanichokoza pale, anakuta nshamwekea mahitaji yake (as in casuals ama mentions za sponsors ambazo anafanya yeye) twaenda zetu hewani! The rest is 3hours of entertainment! Me nadhani na enjoy kama msikilizaji tu. Maana baada ya hapo 6:45 nasikia kele za Gerald anaingia nae, anakuja fanya kaa chonjo and its all a bliss.

Baada ya kipindi, twafanya mazungumzo kidogo kuhusu kipindi na mipango na marekebisho then wanaotakiwa kufanya production wanafanya n.k. Then me nachukua viporo vyangu (kama vipo) I move to my office at Victoria.

Nimefungua ofisi nafanya Corporate Events management and Public Relations (PR). Depending on the current job, I do logistics, make plans for the event in question, sometimes meeting with clients, do presentations and the like. This can go on for like until 9 or 10pm depending on the work load… na ndio twaanza kwahio its always hectic.

A perfect day kwa kweli I guess would be getting my work done and satisfying a client. Hii ni kuanzia kwenye kipindi, huwa tunajua tukimaliza kipindi ambacho tumekipatia kuanzia saa 12, kwahio twamaliza na nafsi zetu kuwa safi kabisa, tukiamini msikilizaji nae kamalizia hivyo hivyo and the same through out the day na kwenye kazi zangu binafsi ofisini kwangu.

Hakuna raha kama kumkamilishia mteja hitaji lake na akaridhika. Of course mara nyingi huambatana na malipo kwa hiyo, you know… Lol.

 

Fina Mango in a commanding entrepreneurship look!

BC: Usingekuwa mtangazaji unadhani ungekuwa nani hivi leo?

FM: Kama radio isinge work out for mimi nadhani ningekuwa Mwanasheria!! Bado lakini nafasi ninayo au siyo??… you never know.. maana nikikwambia ambitions zangu za tangu enzi za primary, we acha tu, kwahio bado naamini nina nafasi ya kuwa so many other things!!! Only time will tell… and my efforts!

BC: Ni sinema gani uliyoiona siku za hivi karibuni zaidi?

FM: Mimi ni mpenzi sana wa TV series – from drama, thriller and a little bit of action, inategemea ni ya aina gani. Ni mpenzi sana wa; (chronological): Friends (I miss those guys), Alias (Loved Jennifer!), 24, LOST, Grey’s Anatomy (Love Meredith & Mcdreamy), SmallVille, Justice, Criminal Minds, Sex & The City (I wish ingeendelea, nina season zote 7 so kila mara nazirudia rudia!) na sasa hivi naangalia One Tree Hill but also enjoyed Veronica Mars and many others. Ki ukweli natazama sana TV. Series nyingi tu, ninapopata nafasi.

Ila upande wa big screen… ya mwisho nimeona ni Shooter ya Mark Wahlberg (was ok), kwenye pirate a.k.a DVD ya ki ‘china’ (not that am proud of that).. ila cinema nilienda mara ya mwisho kuangalia… kuangaliaaa…. honestly sikumbuki. Ngoja niendelee na maswali mengine nikikumbuka ntarudi kujibu..

Ok I remember, mara ya mwisho cinema nimeenda kuangalia BOURNE ULTIMATUM!! So that’s the last movie I saw, in a cinema! And I loved it, The Bourne(s) as in zote 3 fabulous! I hope watatengeneza the fourth, fifth and eventually iwe kama James Bond movies… nimetingwa sana na shughuli mpaka hata sijui sasa hivi sinema mpya ni ipi… apart from American Gangster, kuna rafiki yangu kaiona kaibonda so amenipunguzia munkari wa kwenda kuiona!

BC: Tungependa kukuuliza swali binafsi kidogo kama hutojali.Umeolewa? Ukiolewa ungependa kupata watoto wangapi? Na pia tuseme nini mipango yako katika miaka mitano ijayo?

FM: OK! SIJAOLEWA!! Ningependa kuwa na watoto watatu (3), haijalishi ni wa jinsia gani. Mipango yangu kwa miaka mitano:

-Nifikie na kuvuka malengo niliyonayo na nitakayojiwekea siku za baadae kidogo kwa shughuli za kampuni yangu – OnePlus Communication ambapo for the next 2years nataka niwe ndie ‘The Ultimate Solution to Corporate Events Management & Public Relation needs in Tanzania’.

-Nirudi shule. Want an MBA.

-Niwe nimeshapata watoto wangu ninaowataka! Inshallah kama mambo yatakwenda nitakavyo pengine mwakani nitaanza safari hii!!

-Live a full life!!

 

An MBA is a possibility.Hapa ni siku ya kwanza shuleni kwa Fina(katikati).

BC:Kila la kheri Fina Mango katika kazi zako.Happy Holidays and New Year too.

FM: Ahsante BC na mie nawatakia kila la kheri katika shughuli zenu pamoja na wasomaji wenu. God Bless!!

 1. Mama wa Kichagga, 27 January, 2008

  NINI MAANA YA MTU ASIYEKUBALI WENZAKE/MKANDIAJI WENZIE (JUDGEMENTAL PERSON)

  A judgmental person is somebody who thinks they know everything about you when they really don’t know shit. Judgmental people basically just live in their own little bubble of delusion and have no patience for the superstitious nonsense formally know has “open-mindedness & quot;.

  Why do people have to be so judgmental? Why is it so difficult to just accept people as they are? This is something that drives me nuts! Passing judgments on someone because of the clothes they wear, or the vehicle they drive, where they shop or don’t shop or the music they listen to, their relationship and blablablaa ………… I just don’t understand this!

  I raised my boys (4 OF THEM) to be accepting of other people because of their differences. If everyone were created to be the same person, what kind of world would this be? A VERY BORING ONE!
  Different lifestyles (relationships, likes & dislikes), fashion sense, hairstyles, values, cultures. Its what makes the world go around. And just what makes these JUDGES the perfect ones anyway (chuki binafsi, wivu, majungu,… nk?

  I think it is more important to reach out to differences than to push them away. Differences can make life much more fun, not to mention interesting. SMALL, SHALLOW MINDS. They must increase their awareness. Value the opportunity to know something different from your norm. Life is what we make it. This is not a cookie cutter world and things are far from erfect. All we can do is to make our little corners of it a little bit nicer.

 2. haika mcharo, 28 January, 2008

  Yaani fina unatisha mwanangu kaza buti kwani ni wanawake wachache wenye kipaji kama chako.mimi pia natamani kuwa kama wewe au mwanangu awe kama wewe lakini nafikiri ni vigumu kwani kila mtu ameumbwa na uwezo wake mwenyewe.
  mpe hi sophy.

 3. eve, 28 January, 2008

  i just like phina so much. i just wish her all the best

 4. Ofuneka, 29 January, 2008

  Kwakweli pb iko juu nawakubali! Pliz copy and paste maelezo ya namba 87 anajiita dmb, kweli nawapenda sana pb crew, but tafadhali phina acha kucheka na kuweka muziki ok sikwamba usicheke mana iyo ni sehemu ya vivutio navopenda kwenye utangazaji wako! But kuna kicheko kimeongezeka siku izi kinapoteza maana hasa ikitokea mtu alikuwa ajawackiliza akakutana nacho! Lol inakuwa kituko! Ndo mana nimesema rejea 87 mana amegusa kila nilichopenda kukueleza! Otherwise keep it up! Pia Ninakubaliana na mawazo ya wengine yote +ve and_ve sababu nakukubali sana tu ila ckujui undani wako kwaiyo kama izo neg comments ni kweli zifanyie kazi tu kwakiwango utachoweza! Mana ni ngumu pia kumfuraisha kila binadamu dunia hii! Take it easy! Mamak ars.

 5. Yusuph Mcharia, 19 February, 2008

  Si haba rafiki,wanasema UKIMAKINIKA HUTAADHIRIKA.Pongezi kwako,tangu mwanzo wa ndoto maana halisi ni kwamba siku moja lazima ukae mahali pazuri,japokuwa jitihada zaidi na kutokata tamaa (ni kuacha uoga tu).

  Wengi hushindwa hata kuthubutu.OLE WAO.
  Karibu ktk http://www.mtayarishaji.blogspot.com.

  UBARIKIWE MPENZI.

 6. Yusuph Mcharia, 19 February, 2008

  Kwa kutafuta tunatafuta mara kwa mara,yaani nina maana mara zote.Pole ni neno zuri liletalo faraja,ni sawa,lakini zaidi ipi ni stahili ya mlengwa?

  Kama ni matatizo yapo na hayakomi kama ni kudanganywa kimapenzi inafanyika kwa wengi si kwa wa kiume tu hata wa kike.Najua wapo wenye nia lakini hawapati wa kuwaoa/kuolewa unadhani tatuzi ni nini.

  Kila mtu anamaumivu aliokutana nayo,hata mimi yamenikuta.Hapa najiuliza,MAISHA SI SAFARI YENYE RAHA NA KARAHA?? Pengine labda.Tumuombe Mungu atusaidie jamani.
  Kila mtu acheke cheko analolitamani,au Unasemaje MPENZI?

  Ridhia bac sherehe isiyo na pombe wala nyama ifanyike kama ukikubali.

  UBARIKIWE MPENZI!

 7. famo, 04 March, 2008

  fINA NAKUPENDA SANA

 8. KH, 19 June, 2008

  Dada Fina nakupa hongera kwa hatua uliyofikia, Mungu akujaalie msimamo wako…Endelea kusoma kwani Elimu ni kwa Age zozote zile japo sijasoma ulipoandika umri wako lakini usikate tamaa malengo uliyoyaweka endelea nayo ukizingatia unamsingi/ fedha zakukuwezesha kusoma na elimu ya sasa ni nzuri kwani hata ukiwa na kazi unaweza kusoma….Nategemea baada ya miaka kadhaa km 7 nikusikie unafani nyingine tena kubwa zaidi…. Hongera sana sana Hi to Masoud….

 9. christine apiyo, 25 June, 2008

  kwaio umepumzika, na utangazaji?nawafahamu pia ndugu zako dina, na wale kaka zako wawili, hongera pia, umejieleza vizuri, kip it up

 10. Leonard, 10 October, 2008

  The future is very clear to U sister! Big Up.

 11. newayne, 29 November, 2008

  siku hz atleast umejirekebisha maana ulikuwa unajishebedua sana had unaboa ukiwa on air….al in al unajitahid.

 12. Ray, 07 March, 2009

  FINA UPO JUU SIYO SIRI NAKUPENDA SANA,UR SO GUD JAMAN,I REAL MIS UR VITUKO ON POWER BREAKFAST……ANY WAY UPO JUU ZAIDI KWA SASA

 13. merchant mtandika, 14 March, 2009

  Fina Mango,you have met almost all the attributes of a nearly genius. Your power of reasoning&inquiry makes u among great ladies. I will keep being adamant of you. Please mail me on mtandika2001@yahoo.co.uk

 14. merchant mtandika, 14 March, 2009

  you are arguably among the most visionary ladies to become.your vision and reasoning are open-ended.keep it up fina.best of luck in all your plans.that reflects one’s positive power of thinking.

 15. Mage, 03 April, 2009

  Hey Fina you were like part of family to me and my mum durign PB,. as i said to KP we miss you. very happy to know you are busy with your life, as the ngoni song goes ” ukiondoka kidogo…” the rest ndo hayo.

  hold your head high and you will see the distance things.
  bye

 16. Mjololo Ng,ughuya, 02 May, 2009

  Ok.
  Mjololo

 17. Juliet, 06 July, 2009

  I am proud of you cousin. well done! Your dad will be proud of u! R.I.P uncle Joseph

 18. MZUNGU, 02 September, 2009

  mambo vipi fina kwa kifupi we mtoto ni mzuri me nasema kutoka moyoni alafu unaongea kwa kujiamini kama mama wa familia me naomba tuwasiliane tuongee vizuri kuhusu maisha nadhani utanisaidia mawazo labda uwe mke wangu maana nimekukubali mama ilove so much you are so sweeeeet

 19. MZUNGU, 02 September, 2009

  jitahidi kwa hilo mama nangoja majibu yako nikupe zawadi yako

 20. Moses N. Kassanje, 03 September, 2009

  Fina you so biutiful i have somthing to tell you i;m one of fermas bisness man .for now ilive in canada but my home land in tanzania z;bar posiable to open love rilationship with if you say yes i promis you real love.and i pripere good present for you i give you sport banz verry new as speciol for you make contact with me throue my e;mail.mussa-426@hotmail.com

 21. maria, 06 September, 2009

  To Moses N. Kassanje
  tafadhali andika messeji yako kwa kiswahili unatutia aibu Watanzania.

 22. Loliwichi, 11 September, 2009

  The problem with her is that she is talking so much

 23. halima libani, 15 September, 2009

  yaani fina nakupenda sana lkn kwani nini hutangazi tena Pb tunakumis kipindi kina boa sasa sana tu rudia mama

 24. Anna, 17 October, 2009

  Fina, your so cute. Mungu amekupa sauti nzuri sana na una vipaji vingi sana. i am proud of you much. i love any program ur in. keep it up…

  i also see u can do designing better., since, u look so natural,and so stylish always.

 25. mrs njoni, 04 November, 2009

  hi sister,uko wapi dada yangu Fina mbona kimya?hiv unajua kutokusikika kwko unaniumiza roho. nakupenda sana fanya vile utukumbuke watu wako,mic u

 26. nzwallah, 06 December, 2009

  FINA ILIKE YOU VERYMUCH.
  ARE YOU MANGO FAMILT INCLUDING ,MANGO OF SWISSPORT?MANGO OF CHANEL TEN?IF YES WERE CAN WE MEET?

 27. Asumpta Nsato, 22 December, 2009

  Safi saaanaa dadangu,wacha walonge kazi yako yasikika sana tu achana nao wanafiki hao(usengwile),mi mngoni mwenzio tuko juu south,au siyo wa kwetu? keep it up!

 28. abou, 15 March, 2011

  saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaafi sanaaaaaa mama

 29. Twange Lazaro, 26 July, 2011

  Uko wapi siku hizi na unafanya nini? Tayari nikuzoea masikioni mwangu katika kipindi chenu cha Power Brkft lakini ndio hivyo tena. Ubarikiwe sana ingawa ninauhakika unafanya yaliyomema huko uliko,ahsante.

 30. washola, 12 November, 2011

  namzimia sana huyu mdada sijui kwa nini na sijui kwa nini ukiwa star usijali mashabiki wako…

 31. Mashida, 27 January, 2012

  Wapi dada yak Diana na kaka yak Jardin.

Copyright © Bongo Celebrity