
Pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Sinde Warioba akiteta jambo na Miss Tanzania 2007,Richa Adhia, walipokutana jumamosi iliyopita nyumbani kwa Balozi wa Palestina nchini Tanzania,Yusufu Habab,huko Oysterbay jijini Dar-es-salaam.
Jaji Warioba na Richa Adhia walikuwa ni baadhi tu ya wageni walioalikwa kwenye chakula cha mchana nyumbani kwa balozi huyo ikiwa ni lunch maalumu ya kutunisha mfuko na pia kuwafariji watoto takribani 30 wanaopata msaada mkubwa wa kimalezi kutoka katika shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Mitindo House(TMH) shirika linaloundwa na baadhi ya wabunifu wa mitindo nchini Tanzania wakiongozwa na Khadija Mwanamboka. Kwa picha na habari zaidi juu ya tukio hili bonyeza hapa na pia hapa.
Picha kwa hisani ya MichuziJR.
Page 1 of 3 | Next page