Pichani ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais wa Marekani,George Walker Bush walipokutana jijini New York nchini Marekani mwaka 2006.Rais George W.Bush anatarajiwa kuitembelea Tanzania mwezi ujao katika ziara yake ya kutembelea bara la Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari cha Ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam, ziara hiyo ya Rais Bush, ni katika mpango wake wa kuzitembelea nchi tano za Afrika, ikiwamo Tanzania, kuanzia Februari 15 hadi 21 mwaka huu, kwa lengo la kudhihirisha ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Marekani na Bara la Afrika. Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Picha kwa hisani ya Ikulu ya Marekani.

Feedback / Comments

23 Responses to “RAIS BUSH KUITEMBELEA TANZANIA”

  1. Comment by Edwin Ndaki on January 25th, 2008 4:28 pm

    Itapendeza akipewa na taarifa jinsi BOT inavyojitafunia hayo madola ya misaada kila mwaka.

  2. Comment by Upendo Furaha Amani on January 25th, 2008 5:22 pm

    Karibu Rais George Walker Bush nchini mwetu Tanzania. Waswahili wanasema: “Mgeni aje mwenyeji apone”. Inawezekana Watanzania tukapona kwenye nyanja ya uchumi, pamoja na kuwa tuna madini kwa wingi kuliko nchi nyingi duniani.
    Bado ninalilia uhusiano wetu na Jamhuri ya watu wa China ambao walitujengea Reli ya Tazara wakati huo na kufanya mambo mengi mema hapa kwetu.
    Ninamuomba Rais wetu aangalie uwezekano wa kuingia Ubia na Wachina, na sio hawa wa magharibi, maana Wamagharibi hawa wanakupenda wakati wakijua kuna kitu fulani watakipata kwako, baadaye wakishatimiza haja zao wanakuacha hewani.
    Nawasilisha.

  3. Comment by Msukuma wa shy on January 25th, 2008 6:54 pm

    AKIJA MSISAHAU KUMWAMBIA UFISADIZ!!

  4. Comment by Matty on January 26th, 2008 3:01 am

    Mi naona bora akija awe ameongozana na ex gavana balali.

  5. Comment by Papin on January 26th, 2008 8:58 am

    Huyo jamaa anayekuja ni mnyama, si mmeona alivyoifanyia IRAQ

  6. Comment by mwalimuzawadi on January 26th, 2008 9:59 am

    Nimependa maoni yote kuanzia Ndaki, Upendo, Msukuma na Matty.
    Sasa mi naongezea na JK ajifunze jinsi ya kupanga ziara. Siku 7 nchi tano rais wa nchi tajiri, si siku 10 nchi moja raisi wa nchi masikini. Atupunguzie mzigo walipa kodi sisi, Bernad Membe umesikia?

    Ila kasheshe ni huo ulinzi, tutachoka ila poa tu… mtaka cha uvunguni shurti kubinua matanda…

  7. Comment by Kimori on January 26th, 2008 12:46 pm

    US President’s visit to Tanzania will make no any significant changes in socio-economic developments. After all US, UK and allies have totally different goals towards Africa. If you don’t believe it, please ask Mkapa, who ultimately found out towards the end of his second term of presidency that only Chinese are the ones who could construct a National studium for us!

    Bush and his cliques will atmost pet your back and shoulder and say, “well done boy”, simply because you have agreed to what they have instructed you to do!

  8. Comment by KionaMbali on January 26th, 2008 3:54 pm

    Basi hapo “Vasco Da Gama” si bichwa hilo! mpaka karibu lipasuke!
    Na bado kaahidi tena kumleta Papa Benedikt

  9. Comment by Mama wa Kichagga on January 26th, 2008 4:06 pm

    Katika mila zetu za Kiafrika wageni wote BILA KUJALI ITIKADI ZAO ilimradi ni mgeni hukaribishwa na mwenyeji wake.

    Mimi msimamo wangu hapa ni kwamba tusitegemee “Nchi” au “Rais” wa nchi nyingine atuletee maendeleo yetu. KAMWE KAMWEEE!

    Tuimarishe ujuzi wetu wenyewe bila kumtegemea mtu ndipo tutaendeleo. Vinginevyo tutauliwa kama mende na dawa ya “IT”.

    Bidhaa nyingi za hao wenzetu – macho mstatili zina sumu/lead ambayo husababisha kansa. Baadhi ya hizo ni pamoja na ndala za aina zote, vyuma, toy za watoto nk. Je, tuna utaalamu wa kuzikagua ili zisiendelee kutuzuru au BORA BEI POA?

    MI NAONA BORA TUCHACHARIKE WENYEWE LABDA MSAADA WA KIELIMU TUU ILI TUWEZE KUREKEBISHA TZ YETU WENYEWE.

    HAPA NI SHULE NA KUBADILI SERA NA MIFUMO YETU YA UCHUMI ILI TUSONGE MBELE MAMBO MENGINE YOTE TUTAKUWA TUNACHEZA MAKIDAMAKIDA TU.

  10. Comment by amina on January 28th, 2008 1:21 am

    linakuja kufanya nini hili?aje na osama basi

  11. Comment by Revo Kasikila on January 28th, 2008 1:43 am

    Karibu George W. Bush!

    George ni mmoja kati ya marais ninaowaheshimu kupita kiasi. Ujio wake [ambao ni wa kikazi] kwa namna yoyote ile utakuwa na manufaa kwa taifa bila kujali ni katika nyanza zipi.

    Karibu sana Mzee wa Texas.

  12. Comment by Nice on January 28th, 2008 2:23 am

    Mbona anamsalimia huku anaondoka …si heshma kabisa…tofauti akiwa anasalimiana na viongozi wakubwa wakubwa…..KIkwete anaonekana kufurahi zaidi kusalimiana na Bush kuliko Bush kusalimiana na Kikwete

  13. Comment by ANNA GABRIEL on January 28th, 2008 2:24 am

    Tunamkaribisha mgeni Tanzania.Ila kuna mambo ya kujifunza kuwa yeye ni Rais wa nchi tajiri ila atatembelea nchi nyingi kwa muda mfupi hilo ni zuri kwani anareduce cost.

  14. Comment by JOHNNIE on January 28th, 2008 3:28 am

    Oooh? apo wandugu kazi inakuja sio kwamba Ajira NOOOOOOOO. Wandugu wenzangu wale wakubangaiza mitaani, wamachinga sijuii kina nani uhamisho walazima uko visogoni yanii unakuta mtatimuliwa wote hapo mjini mkatafute pakujificha, kwani hamjuagii nyinyi akija mgeni wa Heshima Nyumbani watoto watukutu wote hukooooo chumbaniiii.
    lakini poa karibu sana Kaka Mkubwa, Upitie na huku Arusha,

  15. Comment by mdunger on January 28th, 2008 4:54 am

    Rais wa dunia anakuja kujangalia maendeleo ya miradi yao,madini nk…Lakini asije nuswa na mbwa wa Bwana mkubwa kama alivyofanywa Mzee Ben Arusha,itanisikitisha.

  16. Comment by Nene Ndefu on January 31st, 2008 2:19 am

    Jamani mbona kama Bush katika hii picha anakuwa kama ana haraka zake?
    Yaani kama kikwete anampotezea muda.KAma vile bush anajafanya ana mambo muhimu zaidi,si mnaona pozi lake? kama vile kikwete ndo kang’ang’ania mkono.

  17. Comment by Johnson Francis on February 1st, 2008 7:27 am

    mmmh,hivi yale mafuta yaliogunguluka pale sijui katewakaa,sijui mchuchuma…..,halafu nimesikia kuwa kuna mkoa fulani hapa Tanzania una madini mengi sana zaidi ya 12,pia Tanzania kuna potential nyingi mno,du,sijui jamaa kaja kuhakikisha?,kama kweli sijui atachukukua hatua gani,mmh i dont know ila ninachoomba asikae sana maana nasikiaga akitua tu,maeneo yale panakuwa hakuna network na mambo mengine mengi,huenda tukapoteza incomings nying mno akikaa sana,pia naona jamaa kila akitua nchi nyingi akiondoka tu,nyuma kaacha kivumbi,…..,lakini Tanzania yetu ya amani sidhani kama hilo laweza kutokea.

  18. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 2nd, 2008 8:28 am

    Dada Amina,
    Naona unataka na Osama aje.
    Hivi huyu Osama ni Rais wa Nchi gani? au unaendekeza Udini?
    Nchi yetu ya Tanzania haina dini, ila wananchi wa Tanzania wana dini zao. Na kila Mtanzania yupo huru kuabudu “Chochote” isipokuwa asivunje sheria.
    Ninachosisitiza ni kuwa, unapotoa maamuzi yoyote fikiria kwanza. Kutokana na kuwa Imani tulizonazo Watanzania wengi tumeletewa na Waarabu na Wazungu, na hizi Imani zinatufanya tuchukiane.
    Sisi ni Watanzania.

  19. Comment by samson on February 13th, 2008 2:32 am

    oooooohoo a don, karibu sana GEORGE, usisikilize mambo ya ufisadi mwachie jakaya atayamaliza tu mbona eddo mchizi wale kamwaga tu
    issue ni hii, AMERICA ina nafasi kuba ya kufungua mlango wa uwekezaji ndani ya tanzania hasa kwenye utalii hapo penyewe, madini ndo usiseme, kilimo ndo kabisa mali asili ndo mizuka sana
    achana na hiyo unajua nini nini george
    kuna vichwa tanzania viko fiti kwenye taaluma uliza ukrain na russsssia watakwakbia kama si mtz aligundua rada inayosoma usawa wa bahari

    haha usiache kula ugali wa kibongo utakua umeniangusha sana mtu wangu
    naku feel sana
    ma men BUSH karibu sana

  20. Comment by kimambo james on February 16th, 2008 7:40 am

    kwanza kabisa napenda nimfahamishe upundo kwamba Sikweli Tanzania ina madini mengi kuliko nchi yoyote duniani. Madini tuliyonayo haya fikii wingi wa madini yaliyopo marekani. Inatubidi watanzania tukubali kwamba marekani ni nchi yenye uwezo mkubwa katika kila fani kuliko nchi nyingine yeyote duniani. Kuja kwa rais wa nchi hiyo kubwa sana kiuchumi pamoja na kijeshi kutasaidia sana kuboresha na kupandisha uchumi wa tanzania.

  21. Comment by manka nkya on February 17th, 2008 5:04 am

    limekuja la nini aaaaaaagh

  22. Comment by kinambile on April 14th, 2008 2:14 am

    Yes off course, km hatuna mvuto hakuna haja ya kututembelea, km tunao basi nasi tuangalie km nao wanao. Then tuweke dili mezani………….wabongo tuache kujidai kuwa tunahitaji kupendwa bure…..tuangalie ni jinsi gani nasi tutawakamua na si kuwa na fikra duni za kulala tuu……….demu mwenyewe akichoka tunamkimbia…..men naye km hana hana mvuto hapaki kitu.

  23. Comment by kinambile on January 16th, 2009 4:00 am

    Bado namzimia huyu ex-rais wa ulimwengu hakuwa akipelekeshwa na vyomba vya habari wala kura za maoni za politiclaly correct idiots

    Our online tourism information portal be proud of it …kinambile

Leave a Reply