Mwisho wa wiki umewadia.Baada ya wiki nzima ya mihangaiko,kupanga na kupangua,leo sio vibaya kama utachukua muda kidogo kutoka kwenye ratiba yako ngumu kupumzisha akili huku ukitafakari mawili matatu yaliyojiri na yajayo.Raha ya maisha ni kwamba kesho na leo ni vitu viwili tofauti.Ndio maana ni mwiko na ni dhambi kubwa kukata tamaa. Maliza wiki hii kwa matumaini na utaona jinsi wiki ijayo itakavyokuwa na mafanikio zaidi.
Kama kawaida yetu hapa BC leo ni siku ya zilipendwa au burudani kwa ujumla.Leo tunarudi tena kwa Patrick Balisidya na kundi lake la Afro 70.Wimbo unaitwa Weekend.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.
Audio clip: Adobe Flash Player (version 9 or above) is required to play this audio clip. Download the latest version here. You also need to have JavaScript enabled in your browser.
Page 1 of 3 | Next page