Profesa Issa Shivji,mmoja miongoni mwa wasomi na wahadhiri wanaoheshimika sana nchini Tanzania.Wale waliopitia Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam wanatambua zaidi mchango wake.Swali gumu ni je tunawasikiliza kwa makini wasomi wetu wakitoa shauri mbalimbali za kujenga na kuendeleza nchi?

Picha kwa hisani ya Bob Sankofa

Feedback / Comments

10 Responses to “PROF.ISSA SHIVJI”

  1. Comment by Gervas on February 4th, 2008 12:09 pm

    Mimi nafikiri kulikuwa na haja ya kuwa na chombo maalum kikawa kama ndo kisima cha busara ambapo development plans za nchi na swala zima la kuutokomeza umasikini zingekuwa zinachukuliwa toka chombo hiki, kwani ni wazi kuwa mbali na kusoma sana wana experience inayojengwa na tafiti mbalimbali. Tatizo utaratibu wetu wa kukiachia chama kinachotawala kuplani maendeleo ni hatari maana siasa siku zote inafuata interest na sio maslahi ya wote. wasomi kama hawa wanatizamwa tu mpaka wanakufa na knowledge zao walizozijenga miaka mingi, ukitizama kuna research, report,seminar nyingi lukuki zilizokwisha fanywa na wasomi wakapendekeza, haya yote huishia dust bin. Maana ukitizma siku zote ushauli wa wasomi huwa haufuatwi bali politics ndo inatawala. watu wanakalia ku-focus ni kitu gani wafanye ili wachaguliwe tena uchaguzi ujao!! Haina maana watu hawa kuachwa tu, it is at this point where they have to be fully utilized!!

  2. Comment by Mwana wa mkulima on February 5th, 2008 12:47 am

    Kwa kweli huyu bwana ni hazina ya taifa sema tuu watawala wetu hawalijui hilo na hata kama wanalijua ni mafisadi hawawezi kulikubali hilo. Shivji Is just an incredible professor. Ni mtu ambaye yuko katika ulimwengu wake kwa kutetea haki za wanyonge na wakulima. Ohh Issa, be blessed and Iam sure Almighty will reard you for your untiring efforts to wrestle the syatem..

  3. Comment by NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO on February 5th, 2008 2:26 am

    PROF. SHVIJ,
    HESHIMA YAKO!

    GERVAS NAKUBALIANA NAWE KABISA!

  4. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 5th, 2008 11:09 am

    Tatizo la Taifa letu la Tanzania ni SIASA. Wasomi watasikilizwa pale ambapo “wana muelekeo fulani” ambao utawanufaisha wanasiasa fulani. Kuna tafiti nyingi zimeshafanyika, kuna shauri nyingi zimeshatolewa na wasomi mbalimbali hapa Tanzania, lakini kama kuna 1% zilizo fanyiwa kazi, ni kushukuru, maana nyingi zinaonekana kunyang’anya baadhi ya Wanasiasa TONGE mdomoni. Mie kwa ujumla ninaunga mkono hoja kwa kusikiliza kwa makini shauri wanazotoa wasomi wetu na kuzifanyia kazi.

    Samahani BC.; nichekeshe kidogo:
    Hivi wale wanaosema Miss Tanzania 2007 Richa Adhia si Mtanzania;
    Je huyu Mheshimiwa Profesa Issa Shivji ni wa wapi?

    Watanzania Tupendane, Tusibaguane kwa lolote iwe ni kwa Asili, Dini, Rangi, Kabila au kwa lolote. Sisi sote ni watoto wa Mama Tanzania.

  5. Comment by juma Rioba on March 6th, 2008 12:12 am

    Issa Shivji simtofautishi sana na wanaharakati wengine kama hayati Seithy Chachage, Haroub Orhman na wengine. Elimu ya kweli haimtenganishi msomi na jamii yake. Hawa wamethibitisha haya kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa kwa kutumia silaha kali ya “mawazo yao”.
    Wengine wakishapata elimu kiduchu tu ama senti kiasi basi hawana ‘shirika’ tena na wananchi walio wengi.
    Kumbuka kwamba kwamba ‘mafanikio’ yanakuwa mafanikio pale ambapo kuna mafanikio.mafanikio ya mtu mmoja katika jamii ni sawa na punje ya haradari katika dimbwi kwani hayaonekani na pia,mara nyingi, hayadumu.Tupiganie utaifa na tuambiane ukweli.

  6. Comment by NYANGE MTORO on July 18th, 2008 10:24 am

    Mzuka sana napenda kuwapa big up viongozi wa awamu ya nne kwa kiwango kikubwa wamechemka kwani hata kidogo hawatumii mawazo ya wasomi wetu mfano prof Issa Shivji ni miongoni mwa wasomi ambao selikari inayo tuongoza kwa kufurahia kuona wananchi hatuna elimu haimtumii vizuri Issa ni mkali mi nakili hilo angalia bunge letu vilaza wamejaa angalia baraza la mawazili vilaza pia wamejaa wakuu wa mikoa na wilaya ndo usiseme mjomba akikujua unakupa.

  7. Comment by Kongamano la Katiba Mpya - Nkurumah Hall Jan 15, 20011 on January 5th, 2011 6:46 am

    [...] KONGAMANO LA KATIBA MADA KUU: MCHAKATO NA MAUDHUI YA KATIBA MPYA WAZUNGUMZAJI WAKUU: 1. PROFESA ISSA SHIVJI 2. NDG JENERALI ULIMWENGU TAREHE: JUMAMOSI, 15 JANUARI 2011 UKUMBI: NKRUMAH, CHUO KIKUU CHA DSM [...]

  8. Comment by Ukombozi daima: Kongamano la katiba mpya tanzania 2011 - udsm on January 5th, 2011 10:41 am

    [...] KONGAMANO LA KATIBA MADA KUU: MCHAKATO NA MAUDHUI YA KATIBA MPYA WAZUNGUMZAJI WAKUU: 1. PROFESA ISSA SHIVJI 2. NDG JENERALI ULIMWENGU TAREHE: JUMAMOSI, 15 JANUARI 2011 UKUMBI: NKRUMAH, CHUO KIKUU CHA DSM [...]

  9. Comment by Kongamano la katiba mpya tanzania 2011 on January 6th, 2011 2:43 am

    [...] KONGAMANO LA KATIBA MADA KUU: MCHAKATO NA MAUDHUI YA KATIBA MPYA WAZUNGUMZAJI WAKUU: 1. PROFESA ISSA SHIVJI 2. NDG JENERALI ULIMWENGU TAREHE: JUMAMOSI, 15 JANUARI 2011 UKUMBI: NKRUMAH, CHUO KIKUU CHA DSM [...]

  10. Comment by Winnie Michael on January 15th, 2011 7:24 am

    I really respect this person because he’s unique n he always knows what he’s doing! I wish to meet him once n my life! He’s looking forward and not backward! Let all young people learn from him for the betterment of our national develepoment!

Leave a Reply