





Kama bado hujapata muda wa kuisoma ripoti ya kamati teule ya bunge kama ilivyowakilishwa jana bungeni na mwenyekiti wa kamati hiyo,Mbunge wa Kyela,Dr.Harrison Mwakyembe,tunashauri uisome.Ripoti imeanisha mambo mazito na pia kutoa mapendekezo muhimu.
Baadhi ya majina ya wanasiasa maarufu(celebrity politicians) na watendaji wengine muhimu serikalini ambao wametajwa kwenye ripoti hiyo huku wakihusishwa,kwa njia moja au nyingine,na Richmond Saga ni PM,Edward Lowassa,Ibrahim Msabaha,Rostam Azizi,Karamagi,Daniel Yona,Arthur Mwakapugi na wengineo kibao au kama wanavyoonekana pichani juu.Unaweza kuisoma ripoti hiyo kwenye post ya hapo chini ukibonyeza pale kwenye (more).Ni ndefu lakini worth reading.Ni wazi kwamba hivi sasa swali sio tena tunakwenda wapi bali tumefikaje hapa?
Feedback / Comments
26 Responses to “WALIOTAJWA”
Leave a Reply


Ushahidi umeshapatikana hakuna cha kusubiria, waachishwe kazi kwa manufaa ya umma.
TANGAZO
NDUGU WATANZANIA WENZANGU NA RAFIKI ZETU WOTE,
BADO TUMEPIGWA BUTWAA NA TAARIFA YA WAZI YA KAMATI TEULE YA BUNGE ILIYOCHUNGUZA ZABUNI NA MKATABA NA KAMPUNI YA RICHMOND YA HOUSTON MAREKANI.
BAADA YA UCHUNGUZI WA KINA, TUMETHIBITISHIWA KUWA HATA BAADHI YA VIONGOZI WETU WA NGAZI YA JUU SERIKALINI WALIAMUA PASIPO AIBU WALA KUJALI MASLAHI YA UMMA NA TARATIBU ZA KIUTENDAJI KULAZIMISHA KUINGIA MKATABA NA HII ASASI FEKI .
TUKIO HILI LIMETUINGIZIA HASARA KUBWA KATIKA TANESCO NA ZAIDI KWA MWANANCHI AMBAYE BADO ANAENDELEA KUHANGAIKA KUKIDHI MAHITAJI YA KAWAIDA YA MAISHA YAKE.
AIDHA CHOMBO KAMA TAKURURU PIA KUSHINDWA KUWEKA HADHARANI HILI RADHI LA UFISADI, BADALA YAKE WAKATUELEZA KUWA MAMBO NI SHWARI WAKATI SI SHWARI NI DALILI ZA KUWEPO MNYORORO WA UOZO KATIKA KUZIMA NURU YA MWENGE WETU PINDI UFISADI UNAPOMILIKWA.
KWA NGUVU NA MAMLAKA YA UMMA TULIYONAYO SISI WANANCHI, LEO TUNASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAADILI YA UONGOZI NCHINI MWETU KILICHOTOKEA KUANZIA OFISI YA WAZIRI MKUU.
KWA UHURU WA KIKATIBA WA KUJIELEZA NILIONAO KAMA RAIA MMOJAWAPO NILIYEGUSWA NA HUU MSIBA, BINAFSI NAPENDEKEZA TUWE NA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO KATIKA BLOGU HII NA KWINGINEKO KOKOTE WAANDISHI WA HABARI NA WADAU WATAKAPOTUUNGA MKONO ILI TUTAFAKARI JUU YA HUU MSIBA NA ULE ULIOTUSIBU HIVI KARIBUNI WA BOT AMBAPO BADO TUNATAFUTA MCHAWI LICHA YA WATAALAMU KUTUELEZA WAZIWAZI SABABU YA KIFO NA JUU YA TAARIFA ZA MAHUTUTI MBALIMBALI TULIZONAZO AMBAZO BADO ZINAFANYIWA UCHUNGUZI.
TUKIWA KATIKA SIMANZI HII TUTOE MAWAZO YETU KWA HEKIMA KWA MIHIMILI MITATU YA NCHI (SERIKALI, BUNGE NA MAHAKAMA) NINI KIFANYIKE WAKATI WA MAZISHI NA KATIKA KUTUOKOA NA BALAA HILI LEO NA KWA VIZAZI VIJAVYO.
HIVYO NAPENDEKEZA KUWA TUKIWA KATIKA MAOMBOLEZO HAYA NDANI YA HIZO SIKU TATU, BENDERA YA LIBENEKE YA BLOGU IPEPERUSHWE NUSU MLINGOTI KWA KUPOSTI PICHA NA MAANDISHI YANAYOHUSU MISIBA HII TU NA SI VINGINEVYO.
AZIMIO LA ARUSHA LILIWEKA, AZIMIO LA ZANZIBAR LIKATWAA,
JINA LA MAADILI YA UONGOZI CHINI YA
NGAO ZETU ZA UHURU NA UMOJA LIDUMISHWE.
NAWASILISHA,
MDAU,
NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO
mi nakwambia wote wajjiuzulu na huyo karamagi ndo nilikua namtamani sana walimnyasinyasi zito bungeni sasa kiko wapi?miwani mbaya
Jamani jamani hawa watu hawana hata haya hivi hela zote hizo wanazipeleka wapi? yaani wananchi wa hali ya chini wanaishi bila hata kuwa na uhakika wa maisha wao wanakusanya mijihela yote hiyo, hivi wataenda kusema nini mbele za mungu? kwa kunyonya jasho za watu ambao hawajiwezi? sasa jamani muwe makini sasa hivi watu wamechoka wako tayari kwa lolote kwa hiyo nyie mafisi mjihadhari kwani mambo ya Kenywa yatakuja Tz na ya kenya itakuwa cha mtoto kwa maani tumechoka.
Yaani mtu unapokea kamshahara kadogo lakini katakatwa kodi hadi unasema hiki nini, matokeo yake wanakuwa watu ambao wameshashiba, hivi huu ni uroho gani? Ila kwa upande wangu nawapongeza sana wabunge, wanatupa matumaini wananchi, na bado uchaguzi ujao tunataka tuingize wasome zaidi huko bungeni ili waweze kutusaidia.Hongera Mwakyembe yaani wewe nafikiri utakuwa mbunge hadi wewe mwenyewe useme basi, kwa maana unatukosha sana wananchi kwanza unaongea kwa kujiamini na una wasiwasi kabisa sasa tungepata wabunge hata japo kumi kama mwakyembe tungesonga mbele kidogo. Lakini watanzania tuzidi kuomba mungu tu tutawapata wabunge kama mwakyembe.
Hongera sana Dr.Harrison Mwakyembe kwa kutueleza ukweli.
Watanzania tumekukubali kweli ulituahidi utafanya kweli leo yametimia.
Lowasa amejiengua tayari kesho anapandishwa kizimbani na atakuwa huko magereza kwa muda maana hakuna dhamana. Huyu ni mkosefu mbaya zaidi kuliko hata akina maumba maana athari zake ni kwa watu karibu millioni 40.
One step ahead in our liberation struggle, to gain independence toward accountability and Responsibility. We must know there is no one above the law. We must all know that no stone will left UNTURNED!
This is what we were waiting.Akina Msabaha, Karamagi, Yona, Mkapa wajumuishwe pamoja na Lowassa ili kuwajibishwa sasa. Kumbe tunaendelea vizuri sasa,tutafika tuu.Bado Kikwete tu kutumia lungu lake, i mean kukunja sura…
Kuna watu dunia hii wana roho mbaya sana kweli hawa jamaa walivyo na pesa bado wakaona ni poa kujiongezea pesa kwa kuwatesa wananchi.
Haya ndiy mabo yanayoleta ethnic violence duniani mimi sitaki kutabiri hilli ia the way it is now kama hawa jamaa hawapelekwi mahakamani then tunaelekea direction nyingine yaani violence inanukia and siyo jadi yetu but believe me hii itawakasirisa watu wengi sana
kumradhi maneno yameteleza kidogo nawasilisha edited version hapo chini.
Kuna watu dunia hii wana roho mbaya sana kweli hawa jamaa walivyo na pesa bado wakaona ni poa kujiongezea pesa kwa kuwatesa wananchi.
Huyu Lowasa mimi nina machungu naye personal maana namjua yeye na familia yake kwa undani zaidi sista wangu alikuwa anasoma na mtoto wake na pia jamaa alikuwa anakuja botswana kuzitumbua pesa zake yupo underground sana anaoperate like some sort of mafia hivi kwa hiyo he is not what people think he is. Haya ndiyo mambo yanayoleta ethnic violence duniani mimi sitaki kutabiri hili ila the way it is now kama hawa jamaa wote especially Lowasa hawapelekwi mahakamani then tunaelekea direction nyingine yaani violence inanukia and siyo jadi yetu but believe me hii itawakasirisha watu wengi sana
Waw!…..Lowassa has already tendered his resignation and I expect others to follow the suit…no joke in this 21st century! We need at least a clean government, which can bring obout tangible changes to the citizens…we are really tired of fake leaders!
Duu…mmhm..hii ndio tz.
Safari moja uanzisha nyingine.
Edo kajiuzulu,hio ni safari kaanzisha.Nafikiri itakuwa busara wengine kufuata nyayo zake .
PCCB ..aibu hiyo inawakuta ,kudondosha taulo ukweni.Edo hosea na wewe jiuzulu.
Yaani mwaka huu ni Edo Ndaki tu ndio nabaki madarakani nikitoa maoni.
Ene wei..tutafika tu.
naomba hao watu wahukumiwe kunyongwa
“Kioo, kioo, alikivunja nani?, sijui sijui, wa mwisho akamatweeeeee!”
Nawasilisha.
Fisadi karamangi anasubiri nini ku stepdown. I’m sick seeing his face. Fisadi mkubwa. mmenyonya jasho la wazazi wetu sana.
Inanishangaza sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kuwaona ninyi viongozi wetu tuliowachagua kwa kura zetu za siri kuwaona mnatabasabu hapa pichani wakati sisi twafa kwa njaa sababu ya uchu wenu wa utajiri.
Kabla ya yote naipa pongezi kamati ilioundwa kutuletea ukweki wote kuhusu Rich mond(richmonduli) kwani inaonyesha kweli hizi ni zama za uwazi na ukweli.
Mimi kama mkereketwa nawasi sana na majukumu walionayo baadhi ya viongozi wetu sijui ni kujisahau au ni kutokujua kilichowapeleka madarakani na kuanza kufanya mambo ya aibu kama alilofanya Lowasa na wenzake samahani kwa kumwita hivyo kwani mpak sasa sio PM tena kwa kashfa hii.
Lakini amejaribu kujitetea mi naona is 2 leti kama wanvyowakorapt wengine kwa nini asingeikorapri kamati mapema mpaka amedhalilishwa namna hii?kama anavyodai? halafu anatudanganya watu wazima eti hawakumtendea haki wangemuuluza. Yeye kwa mawazo yake anafikiri angeulizwa angekubali au? hii ndio maana kamati ikafanya kazi wangemuuliza ukweli usingepatikana lakini pamoja na hayo kuulizwa au kutokuulizwa hakubadilishi ripoti kama wewe fisadi ni fisadi tu.
SIKU ZOTE MFA MAJI HAISHI KUTAPATAPA.
Tujihadhari san na hizi ngozi nyeupe wengi wao hawtupendi hata kidogo nikujineemesha tu
Nawasisi hata na huu ujio wa raisi wa marekani tanzania kama sio kuwatafutia watu wake ambao amewachoka nchini kwake makazi nasi tuwapappatikie kumbe hawana lolote ni kama mateja wetu nao ni mateja marekani. lakini tungojee matokeo yake
Kwi kwi kwi tugawane mali zake mimi naanza na lile shamba la Ngómbe 3000 la Handeni….
Jamani nimefurahi sanaa sana tu,maana niliingiwa wasiwasi kwamba labda watanzania tumekua malimbukeni kulifumbia macho swala zito kama hili.
ni muhimu wahusika wote kuwajibishwa ipasavyo ili waliobaki wajue kwamba watanzania tumechoshwa na upuuzi wa muundo mzima wa serikali yetu,na mambo ya kiholela kama watu hawajaenda shule bwana!!!
its about time kilaza wastep down and watu wenye uchungu na nchi yao wastep in.
MWALIMU NYERERE ALIKUA NA MAANA SANA NA ALIONA MBALI WAKATI ALIPOKATA LOWASSA KUGOMBEA CHEO NYETI KAMA HIKI.
MWALIMU ALIONA MBALI SANAA JAMANI,MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.
Pamoja na hayo yote, tukumbukeni kuwa yalishasemwa na wapinzani tukabaki tunawashangaa. Sasa nadhani rais ivunje balaza la mawaziri lote na awaondoe wale wote wanaotuhumiwa na wanaonuka rushwa. Wananchi tukichoka hatutakuwa na subira tena. Kama TAKUKURU wanadanganya, je wanayoyachnguza sasa watayaleta kwa usawa?
huyu Dr. Harrosin Mwakyembe asipoangalia watamu-Amina Chifupa. Na wakimu-Amina Chifupa ndio hapo watakapokiona kivumbi chake
MUNGU mkubwa na leo hii ndugu zangu wote mmeyaona,ila hayo tisa na kumi yaja muda c mrefu,kuna watu wanaona wao ndio tanzania km yao,km huyu lowassa,na km tungewaacha huko mbeleni wasingeshikika kabisa mana ingekua km mafioso vile,tunamuombea MUNGU bwana mwakyembe ili wasimdhuru,mana sijaona jasiri kama yeye kwa kizazi hiki na kujiuzulu haitoshi tunataka kuona wanafikishwa panapostahili na watulipe hela zote walizochukua,km hawana wafilisiwe,ila km nimngekua rais nafikiri adhabu ya kwanza kufikiri ni kifo kwa hawa wote waliohusika,ndio mana mwl.jk nyerere aliuliza hawa wahindi wanatafuta nn bungeni,na leo tumeona ya rostam aziz yani kila soo kubwa linalohusu hela bongo lazima kuwe na wahindi,nafikri wkt umefika sasa kufanya km ya iddi amini dada hapo uganda,maombi ya wabongo sasa yanajibiwa na si ajabu siku hata rais ambae na yeye anajifanya msafi akavuliwa nguo bungeni,naomba tuwaombee wale walio kwenye kamati ya madini nao wawe na nguvu na kuthubutu km kulikoonyeshwa jana na dr.harrison,ahsanteni sana.
Siku zote uongo na ukweli vinajitenga, na siku za wezi ni arobaini, halafu bado na mengine yatakuja. Wanyan’ganyi wote lazima wafilisiwe na washtakiwe. AIBU KUBWA. Lakini afadhali tunaanza kupona. Na wabunge wetu safari hii wamekataa kupigwa sindano ya ganzi; Walikuwa wapi siku zote hizi jamani, mbona kuna watu wangepona au wangepeleka watoto wao shule kama wangekuwa makini namna hii miaka yote! Tusaidie kuwauliza hao walikuwa wapi siku zote wakati tunaibiwa na watu amabao wanatucheke kila siku. Ndugu zangu, mlikuwa wapi?, mlilishwa nini? Hebu mtujibu na nyie!! Kama wafidhuli wasingeiibia nchi hii kwa miaka 40 Tanzania ingekuwa mbali sana. Bara bara zote kubwa zingekuwa za lami, hospitali zingekuwa super, mashule yetu yangekuwa mazuri sana. Na ajira ingekuwa tele tele, wamachinga wangepungua kwa asilimia 80%. KIKWETE amaekuwa Garbachovu wa Tanzania, HONGERA SANA. JE NA CHAMA CHETU nacho je? mara ngapi kimekumbatia huo ududu? Je kinataka kujisafisha au nacho kijiuzulu? Haki bin Haki tu!! ??
waende zao….ila bado kuna safari ndefu kwa watanzania watakaoteuliwa nao watakua walewale
hehehheh….. hizo zote kelele za mbu nje ya neti
So guys, are you gonna bark all day or you gonna bite??!!
Bora nchi iuzwe tugawane mshiko!!!!!nawatania jamani eheeee.
Ona wanavyotabasamu??coz wanajua washatunyonya wanyonge, wengine hapo sura wamekunja!!!utafikiri wako serious na maendeleo ya nchi yetu kumbe wamejilimbikizia mimali ya kufa mtu!
WAFILISIWEEEEEEEEEEEEEE