MH.MIZENGO PINDA NDIYE WAZIRI MKUU MPYA.

Rais Jakaya Kikwete amemteua Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi huo tayari umethibitishwa na Bunge kwa kura 279 za ndio katika jumla ya kura 283 zilizopigwa.Kura 2 zilisema hapana na kura 1 iliharibika.

Kabla ya uteuzi huu wa leo,Mheshimiwa Mizengo Pinda,ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mpanda Mashariki,alikuwa ni Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mizengo Pinda ambaye kitaaluma ni mwanasheria(alipata degree yake ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam mwaka 1974),alizaliwa tarehe 12 August 1948.Habari ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema Mpinda anatarajiwa kuapishwa kesho jumamosi huko Dodoma.

Wakati huo huo,baraza jipya la mawaziri linatarajiwa kutangazwa jumatatu ijayo.

Page 1 of 3 | Next page