JOHN MJEMA HATUNAYE TENA.

Anga za muziki wa kizazi kipya zimefikwa na msiba mzito.Habari zilizopatikana hivi leo jijini Dar-es-salaam zinapasha kwamba mmoja miongoni mwa wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya au bongo flava,John Mjema,kutoka kundi linalojulikana kama Mambo Poa, amefariki dunia.

Bado taarifa kamili kuhusu kilichopelekea Mjema kufikwa na mauti hazijapatikana ingawa habari mbalimbali zinadai kwamba amejiua kwa kujichoma kisu.Mipango ya mazishi na shughuli zote za msiba zinafanyikia huko Mtoni Kijichi jijini Dar-es-salaam.Bado tunafuatilia kupata habari kamili kwa undani zaidi.

Kama mtakumbuka,miaka michache iliyopita mwanamuziki mwingine kutoka kundi hilo la Mambo Poa, Steve 2K naye alifariki dunia baada ya kuchomwa kisu.

Unaweza kumtizama John Mjema katika video hii hapa chini ndani ya wimbo Gumzo. R.I.P John Mjema.

You need to a flashplayer enabled browser to view this YouTube video

 1. Dinah, 11 February, 2008

  Dear Lord!….pole kwa yaliyopelekea kuchukua uamuzi huo. Mungu awajaalie uvumilivu ndugu, jamaa, mafariki na mashabiki ktk kipindi hiki kigumu cha kuomboleza.

 2. Edwin Ndaki, 11 February, 2008

  Duu…hakika ni suala la kusikitisha mwanadamu anapoamua kusitisha uhai wake.

  Binafsi nimesikitika sana kuona mtu anachukua hatua kama hiyo ya kukata tamaa.

  Kwa wengine ambao tunasoma haya maoni.Msikitake TAMAA hata siku moja.Amini yeye yupo nasi mpaka ukamilifu wa dahari.

  Nawapa pole ndugu,jamaa na mshabiki wake woote kwa msiba huu uliotukuta.

  Nakumbuka wimbo wake wa “wachumba 30”.

  Kwa mungu yote yana wezekana.

  Ene wie,tutafika tu!

 3. Majita, 11 February, 2008

  RIP Mjema.Umeacha wachumba wako 30 wanakulilia

 4. Mr. Upendo Furaha Amani, 11 February, 2008

  Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe.

 5. Angelina, 11 February, 2008

  RIP JOHN

 6. Pope, 11 February, 2008

  OOH MSIKINI KUJIUA KWA KISU!!!!!
  R.I.P JOHN

 7. ola, 11 February, 2008

  siamini aisee…
  kazi ya Mungu haina makosa,muda wake umetimia.

 8. Kekue, 11 February, 2008

  Da!! inasikitisha sana jamani, poleni sana mlioguswa na msiba huu!! Ni wachumba 30 wamekumix au nini sasa? Jameni 2sikate tamaa au kuchukua uamuzi usiofaa ipo siku nyota itang’ara tu Mungu yupo na anatoa kwa wakati wake labda wakati wako bado haujafika labda ni mwezi ujao ee, kwani hao waliofanikiwa unafikiri walianza wapi, ni kutokukata tamaa, Songa mbele!!! anyway RIP John!!

 9. Brother Hugo, 12 February, 2008

  Huu ni msiba mkubwa kwa familia, ndugu na marafiki haswa wanamuziki na sisi mashabiki wa brother John Mjema.
  Kilio chetu ni kundi linazidi kupunguukiwa na watu muhimu kama huyu na Steve 2K, si rahisi kuwapata kama hawa tena.
  Mwenyezi Mungu auiweke roho ya John mahali pema peponi amina.

 10. amina, 12 February, 2008

  Du noma mi sijui hat aniseme nini?hadi mtu kufikia kujiua basi yalimfika kweli

 11. Prosper Ditram, 12 February, 2008

  poleni sana ndugu jamaa na marafiki kwa msiba huu jamani maamuzi mengine yangeombwa ushauri. duu ghafla hatunae tena

  Prosper

 12. Matty, 12 February, 2008

  Ahahhh jamani Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi AMEN!nimesikitika sana maana ni shetani tu huyo aliyempa nguvu ya namna hiyo kujichinja…
  Masikini Kijana bado, niliupenda sana ule wimbo wake wa wachumba 30, lakini mwe Mungu amekupenda zaidi.
  Mungu awape uvumilivu ndugu,jamaa na marafiki!

 13. noah gondwe, 12 February, 2008

  IT IS SO SAD WHY THE MEMBER OF MAMBO JAMBO SUCCIDE COMITY? 2LIPOA KWA STEAVE2K NOW IS MJEMA. SO SAD. POLENI SANA NDUGU NA JAMAA AND THE FUNS OF J.MJEMA, PIA SPIDER POLE SANA KWA KUBAKI PEKE YAKO. MUNGU AKUEPUSHIE ILI BALAA LA KUJIUA KWA KISU.

 14. Rachel, 12 February, 2008

  Poleni sana wafiwa. Ni jambo lakusikitisha kijana mdogo na mwenye promising future kama huyu amekata tamaa. Lakini undani wa yote hatuwezi kuujua. (Nimesoma post kwa michuzi mkubwa kutoka kwa rafiki wa bwana huyu kuwa amefiwa na baba na mama recently nakuwa alianza kuchanganyikiwa na kufagia home kwake akiwa uchi nk.).

  Ni muhimu sana kwa nchi yetu kuanzisha councilling services (au labda zipo) kuwasaidia watu wanaokumbwa na matatizo ya kimaisha ambayo in someways yanapelekea kukata tamaa ya maisha Ingawaje ukweli uabakia pale pale kwamba yakikufika shingoni huwa uamuzi ni kumezwa na ardhi… lakini kuwa na huduma kama hizo saa ingine zinawakutanisha watu kushare yanayowasibu hivyo inasaidia kujua kuwa wapo wengi wenye shida mbali mbali na kubwa kuliko zako hivyo kufikiria mara mbili kabla ya kufanya maamuzi mabaya.

  Poleni sana wasanii na nchi kwa ujumla.

 15. jonh, 12 February, 2008

  nitamkumbuka daima,nilikuwa namkubali sana hasa wachumba 30.Hakika

 16. Niku kuhenga, 12 February, 2008

  mungu ailaze roho yake mahali pema peponi! its hard to believe

 17. salu, 12 February, 2008

  Hoo na tumuombe mwenyenzi mungu amsamehe kwa yote mabaya aloyafanya katika huhai wake. kwani wote njia yetu ni moja hiyo hiyo ila hatujui ni lini.

  M/Mungu ailaleze roho ya John Mahala pema peponi

  ameni

 18. BYE BYE, 12 February, 2008

  dear God,that is the most out of sync video I have ever seen

 19. Danny (UglyD), 12 February, 2008

  Kaka mkubwa umetutoka ila ulipoenda ndio makazi, mi nakutakia mema. Mziki wako hautaisha na wosia wako bado utabaki. Nina imani husingependa tukulilie bali tukuombee, nasi tutajikaza hivyo kaka. Bwana akupokee kwani amekupenda zaidi. RIP John

  Kutoka Kings Studio Disco Thech (London), mi c o mwakilishi.

 20. oprah, 12 February, 2008

  dah mm stii neno ila mungu amuweke mahali pema peponi amen

 21. LIZZIE, 12 February, 2008

  VERY SAD ANOTHER YOUNG PERSON’S LIFE GONE

  google the link below kumuhedhi

  http://www.2five5.com/index.php?option=com_content&task=view&id=942&Itemid=39

  http://www.eastafricantube.com/media/469/John_Mjema_-_Wachumba_30/

  http://www.eastafricantube.com/media/185/John_Mjema_-_Gumzo/

 22. Monica, 13 February, 2008

  Mungu amuweke marehemu Mjema mahali pema peponi, Amina. Kwa sisi tuliobaki tuache kukata tamaa mapema na mambo yakituwia magumu tusichukue uamuzi kama aliochukua Mjema kwani yote yawezekana kwa Mungu. Tupatapo changamoto tumkabidhi Mungu naye atashughulika nazo.

 23. reg, 13 February, 2008

  poleni sana ndugu, jamaa na marafiki

 24. Jennas, 13 February, 2008

  R.I.P JOHN MJEMA

  AMEN

 25. Mama wa Kichagga, 14 February, 2008

  Ni machungu sana kutokea kwa kifo cha aina hii tena kwa umri kama wake, tena msanii!

  Inawezekana kabisa wakati anafikwa na maswahibu yote hayo ya maisha ndugu, jamaa na marafiki walikalia kuchonga midomo na kushabikia badala ya kutia mwenzao moyo wa kuwa na matumaini!

  Tujifunze kutokana na makosa na daima tuepuke kuwahukumu wenzetu maana hujui sumu ya hukumu yako inamfikiaje mtuhumiwa kwani waweza kumkatishia maisha yake pia. HILI NI ANGALIZO “TUWE MAKINI”. TUWE MARAFIKI WAKWELI NA TUACHE UNAFIKI! TUPENDANE NA KUSAIDIANA.

  MWENYENZI MUNGU AKUREHEMU JOHN. AMINA.

 26. Joseph, 28 June, 2010

  VERY SAD ANOTHER YOUNG PERSON’S LIFE GONE

  Mungu amuweke marehemu Mjema mahali pema peponi, Amina. Kwa sisi tuliobaki tuache kukata tamaa mapema na mambo yakituwia magumu tusichukue uamuzi kama aliochukua Mjema kwani yote yawezekana kwa Mungu. Tupatapo changamoto tumkabidhi Mungu naye atashughulika nazo.
  MWENYENZI MUNGU AKUREHEMU JOHN. AMINA.

Copyright © Bongo Celebrity