MWANASIASA mkongwe, Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Augustino Mrema amesema Rais Jakaya Kikwete, atakuwa amewatendea haki Watanzania endapo atawachukulia hatua kali viongozi waliohusika kweye tuhuma za Richmond kwa kuwafilisi mali zao ili liwe fundisho kwa mafisadi wengine. Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa.

Pichani ni Augustine Mrema(kushoto) akiteta jambo na aliyekuwa PM,Edward Lowassa,ndani ya viwanja vya Ikulu mwaka jana wakati wa sherehe za kumwapisha jaji mkuu mpya.

Feedback / Comments

30 Responses to “USHAURI KUTOKA KWA MREMA”

  1. Comment by don on February 14th, 2008 8:01 am

    yaani we fusadi walivyokupiga chini sawasaw kabisa’bado kufilisiwa tu’.lakini mzee hata kama suit huwa hawavai na raba kaka.

  2. Comment by XXX on February 14th, 2008 10:15 am

    HE jamani! mRema kavaa raba?

  3. Comment by Mama wa Kichagga on February 14th, 2008 3:48 pm

    Xxx,

    Mwache avae raba ndio aliyoichagua mwenyewe ili aweze kupangilia rangi ya mvao wa siku hiyo. Huoni shati, kofia na viatu vyote ni vyeupe?

    Pia kuvaa raba ni uamuzi wake wee tinga mkuki moyoni haya, mwingine raba nyekundu haya, mwingine nyeusi ili mradi dunia inapendeza namna hiyo.

    Mi naona anajua kupanga rangi nampa hongera.

    “LETS NOT JUDGE OTHERS TOO MUCH” INSTEAD WE SHOULD CONCENTRATE ON DEVELOPING OUR SOCIETY”

  4. Comment by grmavura on February 14th, 2008 9:29 pm

    WEWE UNAYESEMA SUTI HAIVALIWI NA RABA, NDUGU UNACHEKESHA MANA SIKU HIZI KUNA MITINDO MINGI WANGU, ANGALIA MADIZAINA NA MASUPER STAA WENYEWE WANAVAAJE, MREMA NAKUPA HEKO KWA USHAURI ULIOTOA NI KWELI KABISA INABIDI HAKI ITENDEKE.

  5. Comment by Matty on February 15th, 2008 3:06 am

    Jamani Mbona Mrema kajipendezea tu na raba yake! kwani kuna ubaya gani akivaa raba anawaumizeni Macho au???
    Safi Mrema Kesho ukiamua vaa hata buti kwa raha zako.
    Waswahili sie tuna mambo hivi kwanini tunamuingilia kwenye maamuzi yake te te te !!!!!!!!!!!!!yyyyyy kwanini?????

  6. Comment by kijiwe on February 15th, 2008 3:51 am

    washamba peke yao ndiyo wanaweza kusema hiki hakivaliwi na hiki maana hata kama kile kinavaliwa na kile si umeiga somewhere?doesnt he have the right to rock his own style au design?

  7. Comment by zawad haji on February 15th, 2008 8:19 am

    mh! jamani hata kama,suti na raba haipendezi,labda kwa vijana mabishoo sio kwa mtu mwenye heshima zake kama yeye.kuhusu maoni aliyoyatoa ni mazuri tuangalie utekelezaji.

  8. Comment by Dinah on February 15th, 2008 11:18 am

    Hamuwezi juwa huenda alikuwa akitangaza Raba (as u can c wote mmeona raba na sio kitukingine hahahaha).

    Msijisahau sakata bado linaendelea…

    http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/02/15/108417.html

  9. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 17th, 2008 4:35 am

    Du! Mrema:
    Suti na raba? sijui ni mvao gani huo. Angevaa kiatu cha ngozi cheupe kama alitaka kumechisha.
    Watu wengine pia mnamtetea Mrema kwa kuvaa raba na suti? jamani, nyie mtatetea hata mafisadi kwa vile ni ndugu zenu.

  10. Comment by Matty on February 18th, 2008 2:55 am

    Mr.Upendo Furaha Amani, tunatetea raba aliyovaa sababu kavaa kwa ridhaa yake na hakutaka kumfurahisha mtu,au ulitaka avae mkuki moyoni mzee mzima?? sasa mambo ya mafisadi yametoka wapi tena????au kwasababu kasimama na fisadi???

  11. Comment by amina on February 18th, 2008 4:45 am

    mrema kwa kifupi kachemsha hiyo miraba…kwenda na wakati gani huku?hao madizaina naonaga wakivaa koti la suti,jinzi na raba tena snikers siyo hiyo milakuchumpa…mfatilieni tid ndo anavaaga hivyo na anapendeza na siyo lakuchumpa nasisitiza tena

  12. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 19th, 2008 1:59 am

    Mrema nae fisadi. alipeleka lami kwao wakati akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani. Alipokimbilia upinzani ile lami haikutumika kujengea tena ila barabara, bali ‘ilioza’. Anatakiwa naye aundiwe tume.

  13. Comment by amina on February 19th, 2008 8:49 am

    Mr Upendo furaha usinichekeshe..kwakifupi hapa bongo kila mtu ni fisadi,kila alipokalia mtu anakula hapohapo,sema wengine wanakula vibaya kwa fujo..kama huyu karamagi mara buzwagi mara richmond…hata mi nikiwa na wadhifa na mipesa naiona nakula vizuri najilimbikizia,,ndo tulivo waafrika

  14. Comment by Dinah on February 19th, 2008 12:12 pm

    Hahahahahaha toka nimeanza kupitia hapa leo ndio nimecheka mapaka machozi baada ya kuzisoma comments from 9-12!

    Safi sana, u have made my day wandugu…asanteni.

  15. Comment by Stranger on February 20th, 2008 3:49 pm

    Huyu Mrema Nae, SUTI, KIBARAKA SHEKH NA LAKUCHUMPA (RABA). eh….wachagga kumbe mko hivi!?
    -Stranger.

  16. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 20th, 2008 6:10 pm

    Stranger acha Ukabila.
    Sisi sote ni Watanzania, hii ya kusema Wachagga mpo hivi au vile umelitoa wapi tena?
    Je unafahamu kuwa Tanzania kuna Makabila 125? Je kila mtu ukimtamka kwa kabila lake tutafika? Kama kuna Mtanzania mwenye asili ya Kichagga alikuudhi si useme basi?

    Watanzania tuitane kwa majina yetu na sio kwa makabila yetu.

  17. Comment by Mama wa Kichagga on February 21st, 2008 1:22 am

    Upendo
    Naomba nitofautiane kidogo na wewe ktk hoja #12

    Usipende kushabikia jambo usilolijua au usipende kushabikia kutoa zenye mwelekeo wa upotoshaji au chuki. KUMBUKA KUSEMA UONGO NI DHAMBI KUMBWA!

    Nakumbuka Mrema wakati huo akiwa Mbunge wa jimbo langu, wazee walimuomba awe MGENI RASMI kutia baraka ya Mbunge kwenye harambee ya ujenzi wa barabara ya lami kutoka Moshi Mjini kwenda Kibosho – International Schools hadi Kibosho Hospilal. Wakati huo michango ilishafanyika na uagiza wa lami baada ya wanakijiji kuona umuhimu huo hasa kwa ajili ya kufika Kibosho Hospitali na Sec (Nadhani unauelewa wa shughuli za serikali za Mitaa hii ndio protokali).

    Fedha ile ilichangwa na wananchi wenyewe kupitia mfumo wa kujiwekea akiba ambayo husimamiwa na KNCU – Kijiji (Mfuko huu hujulikana kama Baki – ambayo ni makato ya asilimia ya mauzo kwa kila kilo ya kahawa). Fedha kutoka ktk mfuko huu hutumika kwa ajili ya maendeleo ya jamii au wakati wa majanga ya njaa basi wanakijiji hupatiwa mgawa wa fedha kulingana na asilimia ya mauzo yao.

    Nakumbuka mradi ile ulikufa baada ya Mrema kutochaguliwa awamu iliyofuata na Mbunge aliyemrithi kutokuuendeleza miradi ya nyuma. Mabaji ya matanki ya lami yamehifadhiwa Kirima-Bora KNCU hadi leo tena lami yenyewe imekwisha muda wake na hapo ndipo jasho la mwananchi linapopotelea kwani ilinunuliwa kwa gharama kubwa.

    HAKUNA SENTI TANO YA MREMA KWENYE MRADI ULE WALA KUTOKA VYANZO VINGINE VYA UFISADI – FUATILIA UTAPATA TAARIFA KAMILI.

    Stranger:
    Hivyo ndivyo tulivyo ndugu yangu, kumechisha ndio deal ilimradi watu wanatoa rangi mbalimbali kama upinde wa mvua vile. NB: Ukibahatika kufika Moshi hadi raha utaiona kwani zile rangi kali ndio mvuto wenyewe hasa NJANO KALI, NYEKUNDU NA NYEUPE lol. Halafu hakuna anaemind umevaaje ilimradi binafsi mwenyewe uko huru. Ukifika sokoni au kanisani au msikitini ni raha tupu kwani kama unataka kufanya research ya rangi basi hutakuwa na kazi kubwa ya kutafiti.

  18. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 21st, 2008 5:14 pm

    Mama wa Kichagga,
    Vipi kuhusu ile lami iliyotakiwa kuwekwa kuanzia Marangu Mtoni hadi Kiraracha?
    Usimtetee mrema kwa vile ni kaka yako.
    Tetea Tanzania kwa vile sisi sote ni watanzania.

  19. Comment by Mama wa Kichagga on February 21st, 2008 10:57 pm

    Upendo,

    Nikuulize wewe mwenye taarifa nayo, hiyo mimi siijui. tufahamishe tafadhali .

    NB: Mimi sinaga mkataba na kaka wala nani isipokuwa na msema ukweli tuu bila kujali rangi, dini, kabila wala utaifa.

    Please be honest to yourself and bring true and well-reseached information here. Not only for Mrema but any information please. This will build our society. Gossipping cannot send us any further.

  20. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 22nd, 2008 7:20 am

    Mama wa Kichagga,
    Katika hoja yako #17 umesema mengi na kuonyesha kuwa mimi si mkweli; ninakunukuu: “Usipende kushabikia jambo usilolijua au usipende kushabikia kutoa zenye mwelekeo wa upotoshaji au chuki. KUMBUKA KUSEMA UONGO NI DHAMBI KUMBWA!”
    Mie ni Mtanzania mzalendo halisi, siwezi kuwa na Chuki au kusema uongo au kuwa na muelekeo wa mrengo fulani kwa ajili ya kufurahisha wasiofurahi.
    Mie ninaifahamu Tanzania vyema: Kuanzia Arusha hadi Ruvuma, kuanzia Dar-es-salaam hadi Kigoma na kuanzia Kaskazini-Pemba hadi Kusini-Unguja. Unaposema ninazusha mambo kwa ajili ya kupotosha au chuki hii imetoka wapi Mama wa Kichagga? au ni kwa vile Mrema amezungumzwa? Siku yeyote ninapochangia mada humu sipendi kuchangia ili kumfurahisha yeyote wala kumfanikisha yeyote bali ninatoa hali halisi ninayoifahamu.
    Katika hoja #19 inaonekana unakazia kuwa nililotoa kwenye huu mtandao ni jambo ambalo halina ‘research’ ya kutosha. Je una uhakika na uliloliandika?
    Mie ombi langu kwako ni hili: Usikimbilie kumshutumu mtoa mada yoyote, kabla hujajua undani wa huyo mtu hata kama amemsema ‘mumeo’.
    Tuipende Tanzania, na Tupendana Watanzania.

  21. Comment by Mama wa Kichagga on February 23rd, 2008 3:21 am

    Swala hapa jibu hoja na lete hiyo sera ya ufisadi wa lami wazi kwani itaisaidia jamii kuondokana na mateso, vinginevyo sidhani kama hapa tunahitaji kuzozani maana sio lengo wala mahala pake.

    Kuijua TZ na hata dunia ni muhimu ukizingatia somo la jiografia na historia hufundishwa mashuleni.

    Vinginevyo, naomba kusitisha huu mjadala iwapo hakuna taarifa kamili.

    Nawasilisha

  22. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 23rd, 2008 3:58 pm

    Hoja umeianzisha mwenyewe, kwa kujifanya unamtetea Kaka yako Mrema.

  23. Comment by Mama wa Kichagga on February 23rd, 2008 10:29 pm

    Off-point tusonge mbele. Mwenye akili ataelewa.

  24. Comment by Mr. Upendo Furaha Amani on February 24th, 2008 3:39 am

    Siwezi kusonga mbele na mtu kama wewe, ambaye “Hujui na hujui kwamba hujui”

  25. Comment by zawad haji on February 28th, 2008 4:31 am

    hahahaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!1 VIPI TENA?

  26. Comment by jomaeli on March 5th, 2008 4:02 am

    msumari huo……………unanawanini?

  27. Comment by xxxxx on March 8th, 2008 2:00 am

    mama wa kichaga unajifanya unajua kama nini

  28. Comment by Mama wa Kichagga on March 11th, 2008 11:21 pm

    XXXXX

    Jitambulishe tuopingane au tukubaliane kwa hoja. Ukijificha ujue wee unamatatizo au hujitambui. Mimi sijifanyi kama unavyodai ila najitahidi kujishughulisha, kuyajua mazingira ninamoishi na nasoma habari mbalimbali hivyo NINAELEWA. Kama sielewi sichangii jambo nisilolijua maana najua madhara yake kwa jamii.

    Karibu, ujieleze najifanyaje ili nikujibu kwa hoja ila ujiandae maana ukileta longolongo hapa hukatishi.

  29. Comment by zakayo wangwe on October 1st, 2010 6:27 am

    mrema mi ckuelewi we ni ndumila kuwili acha siasa.

  30. Comment by Mr.zakayo wangwe on October 1st, 2010 6:37 am

    Dr.kikwete usitufanye watanzani mataahila,hivi hizo ahadi unazozitoa kama mvua utazitekeleza vp? Ilihali zile za 2005 zimekushinda na zilikuwa chache. Maana kama ckosei mpaka kufikia sasa umeshaahidi ahadi zaidi ya thelathini na unaomba ridhaa ya kutongoza kwa miaka mitano tu!

Leave a Reply