“USIOGOPE KUCHELEWA,MUHIMU NI KUANZA”-KP

Kwa wengine bado anaendelea kuwa mchora katuni aliye maarufu zaidi nchini Tanzania.Kwa wengine ni mtangazaji maarufu wa redioni ambaye kila asubuhi huwapa wasikilizaji habari mbalimbali na pia burudani. Lakini kwa wengine,yeye ni mbunifu wa mitindo(fashion designer) ambaye anakuja juu kwa kasi ya aina yake.Huyu si mwingine bali Ali Masoud,(pichani) maarufu kama Masoud Kipanya au ukipenda KP.

Leo hii yawezekana kabisa kusema kwamba Masoud ni kijana mjasiriamali ambaye anajaribu kutizama mbali kushinda maelezo. Ni kijana anayependa kujishughulisha kwa bidii na maarifa bila kuchoka wala kukata tamaa.Mwaka jana alitimiza mojawapo ya ndoto zake za muda mrefu kwa kuzindua lebo/nembo ya KP iliyokwenda sambamba na KP Wear.Hivi leo sio ajabu kukutana na watu mitaani waliovalia nguo zenye nembo na ubunifu kutoka kwa KP!

Kwa mara ya pili,hivi karibuni BC ilifanikiwa kupata fursa ya kufanya naye mahojiano kuhusiana na sio uchoraji katuni wala utangazaji bali ubunifu wa mitindo. Nini kilimsukuma kuingia kwenye fani ya ubunifu wa mitindo?Unataka kuijua falsafa inayomuongoza katika fani hii?Je anahofia kitu gani zaidi linapokuja suala zima la ubunifu wa mitindo?Nini mipango yake ya sasa na baadaye kidogo?Kwa hayo na mengineyo mengi zikiwemo picha za baadhi tu ya viwalo vilivyosheheni ubunifu wake,fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Masoud Kipanya,karibu kwa mara ya pili ndani ya BC.Tofauti na tulipofanya mahojiano nawe kwa mara ya kwanza,safari hii tunataka kuongea nawe kuhusu na kazi zako za ubunifu wa mitindo.Kwanza hongera sana kwa kuanzisha lebo ya KP.Mambo yanakwendaje mpaka hivi sasa? Watu wameipokea vipi KP?

KP: Namshukuru sana mola, watu wameipokea vizuri sana sana sana KP ingawa bado kuna wachache ambao wangali wamepigwa na butwaa wakiamini kwamba ninachofanya ni kununua nguo na kuweka lebo. Naomba nitumie nafasi hii kuwaambia kuwa sisi sote, hasa watu weusi, tumepewa uwezo wa hali ya juu kifikra, kinachotukwamisha ni kutojiamini na kujidharau.

BC: Unaweza kutuambia nini kilikusukuma kuanzisha lebo ya KP?Ulifikiaje uamuzi wa kuiita KP?

KP: Ni muda mrefu sana nimekuwa nikitamani kuona mtu ama watu wakiwa wamevaa kitu nilichotengeneza mimi.Na hili lilipata msukumo zaidi katika miaka hii ambayo nimekuwa nikichora. Mara zote tunapochora watu lazima uchore na nguo, hili lilipelekea kutamani kuona mtu wa kweli akiwa amevaa nguo niliyoibuni.

KP imetokana na KIPANYA, na huwezi amini, Marehemu Amina Chifupa ndiye aliyekuwa akinikatisha kwa kuniita KP tulipokuwa katika vipindi vya watoto miaka ya nyuma, hivyo nikaamua kulisajili na kulitumia kama lebo ikiwa na kichwa cha Kipanya mwenyewe.

BC: Kumekuwepo na maswali mengi sana kuhusiana na mchango au involvement nzima ya mbunifu wa mitindo(fashion designer) kama wewe katika zoezi zima la kutengeneza nguo,yaani kuanzia mwanzo mpaka inapofika dukani.Unaweza kutuambia kwa kifupi jinsi wewe mwenyewe, kama Masoud Kipanya, unavyoshiriki katika zoezi zima.

KP: Asante kwa swali zuri ambalo litazidi kuweka wazi mchakato mzima.Ninachofanya ni hivi; kichwani nakuwa na aidia ya dizaini ya kitu husika, iwe ni shati au tshirt au jeans au chochote, kisha nachora katika karatasi na ku-save kwenye cd, kwa kuwa huwa natengenezea nje. Nikifika kule huwa naenda katika masoko makubwa ya material, kisha nachagua huku nikijua kuwa kila material ninayonunua itakwenda kutumika katika mchoro fulani.

Baada ya hapo nakwenda katika factory zinazotengeneza lebo, kuanzia vigozi vya jeans mpaka vifungo vikubwa vya jeans vikiwa na logo ya KP. Then nakwenda viwandani nikiwa na lebo na dizaini ninazotaka.Within a week wananitolea sampo, nikiipitisha wana-produce kwa idadi ninayotaka.Ni zoezi gumu linalohitaji commitment ya hali ya juu.

Mtaka cha uvunguni sharti ainame.KP akiwa kazini.

BC: Kila mbunifu wa mitindo huwa na falsafa au mwongozo wake kuhusiana na sanaa ya mitindo.Unaweza kutuambia yako ni ipi?

KP: Falsafa inayoniongoza au ninayoitumia katika sanaa ya ubunifu wa mavazi ni ukweli usiofichika kwamba fashion design has no rule, one can branch out to where no one has ever thought of reaching.

BC: Ni wabunifu gani wa mitindo,ndani na nje ya Tanzania,ambao unadhani kwa njia moja au nyingine wamechangia kuikuza sanaa yako ya ubunifu wa mitindo?Kivipi?

KP: Wabunifu wa ndani walionitangulia wamenisaidia sana kwa ku-pave the way.Hawa, akiwemo khadija Mwanamboka na Mustafa Hassanali, wamewafanya watanzania wengi japo kwa taratibu kuanza kutuamini. Wa nje wengi wao wamekuwa wakinipa usongo wa kutamani kufanya wanayoyafanya, (sio kutamani kuwa shoga ohooooo!!!)

BC: Nini unakipenda zaidi na nini usichokipenda kuhusiana na kazi yako ya ubunifu wa mitindo?

Page 1 of 5 | Next page